Watu waliokufa wakiwa na siri kubwa

Watu waliokufa wakiwa na siri kubwa

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
2,101
Reaction score
5,442
Ogle Carburetor
Mwaka 1970, Jamaa mmoja huko Marekani aliyekuwa akijulikana kama Tom Ogle aliamua kutengeneza carburetor yake mwenyewe ambayo alilenga kupunguza kiasi cha unywaji wa mafuta wa gari lake. caburetor yake ilifanya kazi kwa kukandamiza mafuta na kuyabadiri kuwa hewa kisha kusukuma hiyo hewa kwenye chemba za mlipuko. Aliiweka kwenye gari lake aina ya Ford Galaxie na aliweza kutembea Maili 113 kwa kiasi cha lita 3.8 za mafuta tu.
Bahati mbaya ni kwamba hakuna kampuni yoyote iliyokuwa ikijihusisha na utengenezaji wa magari iliyo vutiwa na uvumbuzi wake hivyo alifariki mwaka 1981, bila kuacha ameandika namna alivyotengeneza carburetor hiyo. Gari lake liliuzwa kwenye maskrepa hivyo hata carburetor iliyokuwemo ilisagwa sagwa.

Kadinali wa mwisho kuchaguliwa na Papa John Paul wa 2
Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kuchagua na kutomtangaza Kadinali ikiwa anaishi kwenye nchi ambayo kuna ukandamizaji mkubwa wa dini, na kutangazwa kwake kukawa kunaonekana kama kunaweza kuwa chanzo cha tishio kwake,
Utaratibu huu ni pale papa ndiye anayekuwa anajua majina ya makadinali hao peke yake na yeye ndiye ana mamlaka ya kutangaza majina yao kwa watu. Kuna makadinali wanne ambao kabla ya Papa John Paul kufariki aliwateua, watatu kati yao aliwataja majina lakini mmoja hakumtaja mpaka alipofariki. Swali limebaki kuwa je huyo wa nne atakuwa ni nani?

Nikola Tesla Death Ray.
Katika wavumbuzi na wanasayansi ambao waliwahi kuishi, huyu jamaa ni kiboko maana alikuwa na akili ya ajabu sana. Kwangu mimi ni best and ana simama at the top of my list.
Huyu jamaa bwana kabla hajafa alidai kwamba amegundua njiainayoweza safirisha umeme mkubwa kupitia njia ya anga yani kama ambavyo mawasiliano ya simu za mkononi yanavyo safirishwa wirelessly.
Lakini kwa wakati huo hakuwa ameshaanza kutengeneza kifaa kwa ajili ya kazi hiyo, na bahati mbaya akafariki jambo la kustaajabisha karatasi zilizokuwa na michoro na notisi za vumbuzi zake zilipotea katika mazingira ya kutatanisha.

Plastic isiyo unguzwa na moto
Mhandisi na mgunduzi wa Uingereza aliyejulikana kama Maurice Ward , baada ya kushuhudia ajali ya ndege iliyosemekana imesababishwa na vifaa kushindwa kuhimiri joto hivyo kuyeyuka, aliamua kuingia maabara na kutengeneza plastic ambayo ilikuwa inaweza kuhimili joto mpaka la kiwango cha nyuzi joto 10,000 huku ikiwa na uwezo wa kuhimili mgongano unaoweza kusababisha na mlipuko wenye ukubwa wa lile bomu lilidondoshwa Hiroshima, sasa yajumuishwe yowe 75 halafu yadondoshwe kwa pamoja bado hiyo plastic ingeweza kuzuia nguvu ya mlipuko huo usiguse kitu kilicho upande wa pili.
Baada ya ugunduzi wake Ward aliamua kutafuta watu wa kununua ugunduzi wake, na NASA walivutiwa sana na ugunduzi wake wakamuita katika awaonyeshe ugunduzi wake. katika kuwaonyesha uwezo wa ugunduzi wake, Ward alichukua yai bichi akalipa uji uji wa ile plastic yake kisha akachukua bunsen burner akalichoma moto kwa dakika 15. baada ya hapo akalipasua na watu wote walipigwa butwaa kwa kuona lile yai bado liko vile vile japokuwa lilikuwa limewekwa kwenye moto mkali.
Ward alishindwa kufikia makubariano na NASA na akagoma kuwauzia ugunduzi wake, na bahati mbaya alifariki mwaka 2011 bila kumwambia mtu yeyote alivyo tengeneza plastic hiyo. Jambo pekee alilosema ni kwamba mchanganyiko wake ni wa aina organic polyster za aina 21, copolymers na kiwango kidogo cha ceramic
 
Na yule aliye gundua gari ya kutumia maji alitisha mbaya
Hiyo inafahamika jinsi ya kutengeneza, kwakuwa maji ni h2o so kinachofanyika ni kwamba kuna process inaitwa electrolysis inayoweza tenganisha hydrogen na oxygen, kama ujuavyo hydrogen ni gas yenye nguvu inayowaka moto kirahisi na kulipuka so inaweza tumika katika kuendesha gari, lakin jambo hili linahitaji nguvu kubwa kutenganisha maji upate oxygen na hdrogen.
Nguvu hiyo kuipata utatumia chanzo kikubwa cha energy kuliko matokeo ya hydrogen utakayopata hivyo basi gari linalotumia maji ni kama freud flani hivi.
 
Ila mungu alivyo wa ajabu, chlorophyl kwenye jani inaweza kufanya hydrolysis ila nahisi kiwango kidogo sana cha energy kinatumika ili kupata H+ na OH-
 
Safi mleta mada....
Nikola Tesla alivumbua vitu vingi mno ....infact...alikuwa ana program ya kutengeneza umeme kupitia mwanga/hewa...namquote "there will be a free energy for every one everywhere"...but kabla hajamaliza hii project.... maana alishaanza kutengeneza mnara....akafa.... bahati mbaya hakuwa mtu wa kuandika sana formula za uvumbuzi wake....hata hizi simu android tunazotumia ni idea yake....
 
Ningependa kujua uhusiano wa mwanasayansi tesla na ellon musk
 
Safi mleta mada....
Nikola Tesla alivumbua vitu vingi mno ....infact...alikuwa ana program ya kutengeneza umeme kupitia mwanga/hewa...namquote "there will be a free energy for every one everywhere"...but kabla hajamaliza hii project.... maana alishaanza kutengeneza mnara....akafa.... bahati mbaya hakuwa mtu wa kuandika sana formula za uvumbuzi wake....hata hizi simu android tunazotumia ni idea yake....
Asee na kwa kizazi hiki cha kisingeli sidhani kama kuna atakae malizia pale alipoishia,tumekwisha
 
Mimi baada ya kuona avata yako nikasahau hata topic.. Dah huyu jamaa sijui nae atakufwa lini
Uyu mjomba bado yupo sana tu... turudi kwenye mada hata hapa Tanzania tuna mtu alikufa na siri nzito ndugu Gavana Billali
 
Back
Top Bottom