Alfred Masesa
Member
- Nov 2, 2016
- 71
- 146
Wakuu salamu.
Ipo imani mbaya sana miongoni mwetu vijana, imani iliyopofusha akili zetu na kutufanya tuamini ujinga usio na kichwa wala miguu, imani ya kivivu kabisa na imani yenye roho ya mauti ndani yake.
Ya kwamba, kijana ukifikisha umri wa miaka 40 na bado unateseka kimaisha, yaani huna pa kulala na kula yako ya taabu sana basi kamwe huwezi kufanikiwa tena kimaisha.
Wakuu, imani hii ni ya kijinga kuliko ujinga wenyewe.
Kwanza kabisa nataka kuwaweka wazi ya kwamba, mafanikio namba moja hapa duniani ni "Afya ", kuwa na afya ndo baraka za kwanza kabisa ambazo Mungu humjalia mwanadamu.
Huwezi kuwa na mabilioni ya pesa benk halafu upo hospitali miaka mitatu umelazwa unaumwa ugonjwa ambao hauna tiba halafu ukawa na amani na au ukaifurahia pesa yako.Kiuhalisia maskini atakuwa na amani na furaha kuliko wewe Tajiri.Sasa twende kwenye mada.
Swali nalowauliza na ningependa sana wanijibu wanaosema kwamba ukifikisha miaka 40 huwezi tena kufanikiwa, nataka wanijibu, Kwa hiyo ukifikisha miaka 40 hujafanikiwa utakaa na kusubiria ufe?
Utakata tamaa kiasi kwamba hautajishughulisha kwa lolote kisa tu umefikisha miaka 40? Bahati mbaya ni kwamba kuna watu wana imani kabisa juu ya msemo huu haramu kwamba, "life starts at 40".
Henry Ford, mwanzilishi wa magari ya Ford alianzisha kiwanda cha kutengeneza magari hayo akiwa na umri wa miaka 45,hakuwa na pesa taslimu, alikuwa na mawazo tu, kupitia mawazo yake gari la Ford likatengezwa hadi kuwa kiwanda kikubwa na magari hayo kusambaa kote duniani, leo hii familia ya Ford ni matajiri wakubwa, alianza mwaka 1908,miaka 14 kabla Nyerere hajazaliwa.
Jack Weil, alianzisha biashara ya mavazi ya Cowboy akiwa na miaka 45 na alikuwa na mtaji mdogo sana, leo hii Cowboy ni maarufu pote duniani, Jack Weil amekufa mwaka 2008 akiwa tajiri mkubwa na akiwa na umri wa miaka 107.
Harland Sanders, akiwa na umri wa miaka 62 alistaafu kazi akiwa na mafao kidogo Sana, alichanganyikiwa kabisa akataka kujiua, alikuwa na hali ngumu mno kimaisha. Baadaye alipata wazo la kukaanga kuku na kuwawekea viungo vya kuvutia, na kisha akawa anawaweka kwenye makopo, alianza kuwatembeza nyumba hadi nyumba, mtaji ukakua akafungua kampuni, inayoitwa "Kentucky fried chickens "ndani ya miaka 12 alikuwa tayari ana dola mil mbili.
Mzee huyu amekufa akiwa tajiri.
Mzee Sanders enzi za uhai wake.
Kama huyu mzee aliweza inakuwaje siye vijana tunashindwa? Tunaona aibu kufanya biashara flani eti tutachekwa, huyo anayekucheka hawezi kukupa hata sh 500 ya chai.
Mwaka 2009 nilikuwa na rafiki yangu mwenyeji wa shinyanga, huyu jamaa alikuwa na miaka 48, aliishi maisha magumu sana, nyumba yake Ilikuwa ni ya tope na nyasi, baadaye Siku moja aliniambia, "Masesa, mimi pamoja na kuwa umri umeenda lakini siwezi kukata tamaa, hapa nimepata mbuga ya kulima mpunga hela tano ".
Na kweli msimu ulipofika alilima Kwa kujituma hasa, alipovuna akasubiria msimu wa mazao kupanda bei, aliuza kisha akaanzisha biashara ya duka kubwa, kila baada ya miezi kadhaa akipata faida anaongeza duka jingine, kufikia miaka miwili baadaye alikuwa na maduka 15. Alijenga nyumba nzuri sana kahama, tayari alikuwa amepata mafanikio. Bahati mbaya aliuawa na majambazi."Pumzika Kwa amani rafiki yangu Maduhu Ngeleja ".
Hakuna umri maalumu wa mafanikio, kinachomzuia mtu kufanikiwa ni ugonjwa na kifo au ulemavu basi. Zaidi ya hapo hakuna. La kuzingatia hata Kama una shida kiasi gani, tambua kuwa, hakuna usiku usio na mchana.
Naandika waraka huu siyo kwamba tayari nimeshafanikiwa, la hasha, nipo napigana kiume kutafuta mafanikio.
Naandika ili tupeane moyo kwa wale wenzangu na mimi waliokata tamaa kabisa, mara nyingi tunajifunza kwa watu waliofanikiwa na siyo walioshindwa.