Watu wa mabondeni tunateseka, msaada tafadhali

Ebu pisheni mnagandana mabondeni huko kwani nyie vyura muishi kwenye madibwi na wewe ukipigiwa simu unawambia niko dar hahaha kama mjini hukuwezi rudi baba si lazima wote tuwe mjini
 
Dawa ya kuwahamisha watu wa mabondeni/sehemu hatarishi ni kubomoa tu nyumba ni sio vinginevyo, ni vyema wakabomoa wenyewe kuliko kusubiria hatari itakayo wakumba, hata wakipewa miaka 10 kamwe hatohama!
 
zinashughulikiwa kero za serikali kwanza, kero za wnanchi 2017
 
Kwanza we hata hukumchagua.
 
Ukiona mtu yeyote anaefurahia hali hii ujue hana uchungu na mzazi wake
We ukikuta mzazi wako huyo unayejifanya kumpenda kasombwa na kafa kwa mafuriko utaionaje hii serikali?
 
nakushauri ufuate taratibu za nchi kwani wakati unaamia hukumuuliza mwenye nyumba kama amejenga kihalali, nyumba hzin namba za mitaa, nyumba ni maficho ya wezi, majambazi vibka, wauza madawa wote wanakaa huko, kajiongeze upate maisha bora na afya njema sio kuishi kwa tishio la kipindupindu, kwa kuwa vioo vyote ni vya ghorofa, gari la maji taka haliwezi fika, zimali moto pia, nyumba hazina upepo wa kutosha, watoto wanazaliwa kwenye mazingira magumu wanoota sugu za matusi kwa sababu ma mama wengi hawana kazi, wao kusuka, umbea kupika chapati, kujifunza kucheza vigodoro, bora kama umeshindwa uombe nauli kwani kwenye hujaiba kuliko kutufia mjini kwa jari ya kipindupindu.
 
Kuna mtu aliniambiaga kuwa akili za watanzania wengi ziko nyuma.zile nyumba kwenye yale maeneo zipo kuanzia miaka ya 71 huko,wengi waliobaki mle ni wajukuu na wajane,ambao hawajui waende wapi kosa ni wazazi wao waliotangulia pia ni kosa waliofanya wasimamizi wa sheria wa enzi hizo,so tufanyeje na hawa wajane na mayatima.je wabomolewe na kuwachwa kama wadudu barabarani? Lazima mambo haya yafikiliwe mara mbilimbili
 
Nilipita Kinondoni wakati tingatinga linapita, ni huruma sana. Nadhani Serikali ingewapa muda baada ya kutoa agizo hasa ikiingatiwa January ni mwezi wenye majukumu mengi kwa watu wengi...
Nani aliwapeleka pale bonde la mkwajuni na jangwani? mi nimezaliwa Dar na umri wangu ni wa kutosha tu, sikuwahi kuona mtu anajenga maeneo yale tangu miaka ya 80 hata ya 90, iweje leo wakurupuke kutoka bush huko wanunue mabonde ya mpunga wajenge nyumba? kwani wenyeji wazaramo walikuwa hawapaoni humo mabondeni? Huo ndio ujuha.
 
acha hizo huyu mjne akisombwa na maji ujane wake si ndio unaishia hapo, hatuwezi kumpoteza kwa sababu za kijinga, kuna siku kova na medisadick walitaka kufa kwa helkopter kisa kutembelea wahanga, bora kubomolewa kuliko kusumbua serikali, hatutaki kuona vifo vya maji bora vifo vya kupigwa na baridi ukinusurika unaomba nauli unarudi kwenu. kama ulikuwa huna mazoea kwenda kwenu anza kujipigisha simu kwa wajomba na wababa wadogo lakini kubomolewa ni tarehe 5 tu hkuna namna nyingine.
 
Mkuu ukianza ku-trace nani kakosea, wote wana makosa. Serikali ilikuwepo wapi wakati wanajenga? Kuja kwa Serikali mpya haimaanisha uozo uliolelewa na awamu zilizopita hauwahusu, wamerithi mikataba ya kifisadi ya kufua umeme na taka nyingine za wababe, kwanini waanze na watu wasio na ubavu!

All in all siafiki watu kukaa sehemu hatarishi lakini waangalie namna bora ya kutatua, wakimpa mtu waliempigia X miezi 3 ajipange ahame wanapungukiwa nn! Unampa mtu masaa 48! Sometimes ubinadamu na busara hutangulia rula ya sheria...
 
Hujui historia ya hao watu wa jangwani na bonde la mkwajuni. Nikurudishe nyuma kidogo, kwanza alianza cpt Ditopile aliwaambia wahame na wakaelekezwa pa kwenda na viwanja wakapewa. Walichofanya baadhi waliuza tena zile nyumba huku wameshapewa viwanja! na waliobaki waligoma na kwa kuwa ni mzaramo mwenzao akamezea. Akaja Makamba, akawaamuru wahame tena! huyu wakamjibu kwa kebehi sana na kumuita wakuja! hawakuhama! akaja Kandoro akawaamuru wahame na wengine wakakubali na wakapewa usafiri wa vitu vyao na magari ya serikali yakawabebea vifaa waliowengi wakamwambia hawatuhami umetukuta town nenda na ushamba wakon Hawakuondoka akaja Said Merk naye akawaamuru wakagoma! sasa unataka notice ipi, ya miazi mitatu au ya miaka 10 naa iliyopita? kwani unafikiri hawajui,? sheria ziheshimiwe bana.
 
Mkuu ni kweli sijui historia ya muda kidogo, Pinda na Kikwete wameshawahi kuzuia bomoa bomoa ya Magufuli wakati yuko ujenzi. Watu hao wawili walikua wana madaraka makubwa wakati wao kuliko wote uliowataja.

Watu hao uliowasema kwa namna moja au nyingine ofisi zao ziliwezesha huduma muhimu kufika hayo maeneo waliotaka wahusika wahame. Watu wa mabondeni, hifadhi ya barabara na maeneo mengine yasiyoruhusiwa ni matatizo ya muda mrefu sana na wengine wana nyaraka za kuishi maeneo husika tena si kwamba wamecheza mchezo kuzipata lakini kwa taratibu halali. Serikali ya Magufuli imeweka sheria pembeni Zenji na kutanguliza busara ya majadiliano, Magufuli aliwapa grace period ya siku saba wafanyabiashara wezi wenye hela zaidi ya walalahoi wa mabondeni, kwann awape walalahoi masaa 48!
 
The world is unfair,kuna watu humu ni mabingwa wa kuropoka bila evidence.ukiuliza ni lini na nani na wapi mtu alikufa kwa mafuriko hawawezi kujibu,mijitu imekalia kukalili tu,ila mnaofurahia sawa furahieni ila waza ingekuwa ni wewe ungejisikiaje?
 
Mnamkumbuka mzee lowasa mfuateni monduli atawasaidia ana roho nzuri sana yule mzee
 
The world is unfair,kuna watu humu ni mabingwa wa kuropoka bila evidence.ukiuliza ni lini na nani na wapi mtu alikufa kwa mafuriko hawawezi kujibu,mijitu imekalia kukalili tu,ila mnaofurahia sawa furahieni ila waza ingekuwa ni wewe ungejisikiaje?
hivi lile jengo lililojengwa Jangwani pale halitafikiwa na maji! kwa nini serikali isifanye reclamation au kuongeza kina cha mto!
je hayo maeneo yatabaki matupu au tutaona mijengo inaporomoshwa!
 
mtoa mada,ada mshafutiwa ,kwa hiyo usiitaje kabisa yani!!!
 
Na usishangae kabisa baadae kukaja kuwekwa mijengo
 
Watanzania wenyewe ni JIPU WANAHITAJI KUTUMBULIWA.......................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…