Watu wa Dar ni wachoyo sana.

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,343
2,000
Hivi karibuni nilikuwa Dar es Salaam kwa safari ya kikazi, nilikaa huko Dar kwa muda wa wiki mbili, hivyo nikaamua kuwatafuta ndugu jamaa na marafiki ili niwasalimie kabla sijarudi kwetu.

Majibu niliyokuwa napata yalinishangaza sana, kila niliyempigia simu na kumwambia nipo Dar aliniambia yupo safarini Bagamoyo mara Zanzibar, nikabaki kujiuliza ina hawa watu wote walipanga kwenda Bagamoyo mimi nikija Dar, nimejaribu kushare jambo hili na watu mbalimbali wameniambia hata wao yaliwahi kuwakuta hayo.

Jambo lingine ambalo nimeligundua watu wa Dar wana maisha magumu tofauti na wanavyojikweza hivyo wanaona ukiwatembelea au ukikutana nao wataumbuka.

Watu wa Dar acheni uchoyo, mbona nyie mkija huku Mwanza na mikoani tunawapokea vizuri na kuwakarimu vizuri kwanini tukija huko kwenu mnaanza visingizio vya safari.
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,130
2,000
Ikiwa assumption yako ya kwanza kabisa ni kwamba hao jamaa ni wachoyo basi ni kweli ungekuwa kimeo... I mean, ulikuwa prepared kuwaongezea watu bajeti kwahiyo the best shot ilikuwa kukuambia wamesafiri!!! Hata mimi ningekuambia nimesafiri!!

Kwanini huku-assume kwamba Dar watu wapo busy sana kiasi kwamba wakigundua upo Dar na utawatembelea basi wanajifanya wamesafiri ili usiwaharibie ratiba zao!!!
 
24hrs

JF-Expert Member
Dec 8, 2016
2,595
2,000
Hivi karibuni nilikuwa Dar es Salaam kwa safari ya kikazi, nilikaa huko Dar kwa muda wa wiki mbili, hivyo nikaamua kuwatafuta ndugu jamaa na marafiki ili niwasalimie kabla sijarudi kwetu.

Majibu niliyokuwa napata yalinishangaza sana, kila niliyempigia simu na kumwambia nipo Dar aliniambia yupo safarini Bagamoyo mara Zanzibar, nikabaki kujiuliza ina hawa watu wote walipanga kwenda Bagamoyo mimi nikija Dar, nimejaribu kushare jambo hili na watu mbalimbali wameniambia hata wao yaliwahi kuwakuta hayo.

Jambo lingine ambalo nimeligundua watu wa Dar wana maisha magumu tofauti na wanavyojikweza hivyo wanaona ukiwatembelea au ukikutana nao wataumbuka.

Watu wa Dar acheni uchoyo, mbona nyie mkija huku Mwanza na mikoani tunawapokea vizuri na kuwakarimu vizuri kwanini tukija huko kwenu mnaanza visingizio vya safari.
ugumu wa maisha kitu kibaya sana...
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
15,060
2,000
Hivi karibuni nilikuwa Dar es Salaam kwa safari ya kikazi, nilikaa huko Dar kwa muda wa wiki mbili, hivyo nikaamua kuwatafuta ndugu jamaa na marafiki ili niwasalimie kabla sijarudi kwetu.

Majibu niliyokuwa napata yalinishangaza sana, kila niliyempigia simu na kumwambia nipo Dar aliniambia yupo safarini Bagamoyo mara Zanzibar, nikabaki kujiuliza ina hawa watu wote walipanga kwenda Bagamoyo mimi nikija Dar,Jambo lingine ambalo nimeligundua watu wa Dar wana maisha magumu tofauti na wanavyojikweza hivyo wanaona ukiwatembelea au ukikutana nao wataumbuka.
Dar kuna maisha magumu balaa watu wanalala barabarani huku ulitaka wakukaribishe wapi ?
- Wengine wanalipia Tsh 400 kulala kwenye mabox kwenye korido za maduka, Dar njaa kali sana. Wengine wanaotoka huko mikoani ni WALINZI ( Tena ulinzi wa Tsh 150,00 ) kwa mwezi na wanawadanganya huko mikoani kuwa ni MAASKARI. Huku Dar kumejaa MATAPELI tena utapeli wenyewe wa akili ndogo. Wewe take it easy !
 
agata edward

JF-Expert Member
Nov 25, 2014
6,676
2,000
Uku tupo bize ndomana tembea yetu tofauti na ya Wa mikoani! unakuta mwanaume anatembea polepole kama anasukumwa..
 
Queen of Sheba

JF-Expert Member
Feb 5, 2016
735
1,000
Hahaaaaaa watu wanaogopa bajeti ya chakula itaongezeka, uwe unaenda kwa watu na furushi lako la chakula uone kama utaskia ya bagamoyo.
 
Juanfrani

New Member
May 23, 2017
3
45
USAFI WA MWILI UCHAFU ULIOKUBUHU MAENEO WANAYOKAAA.
SISTA DUU MABRAZAAA MEN SEHEMU MUHIMU KAMA VYOO BAFUU HATA MAZINGIRA YA NYUMBA ZAO NI BORA CHOO CHS KIJIJINIIII.
POLENIII SANA
 
for life

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
2,522
2,000
Hebu waamchimbie nakuja na mchele na samaki kama hawatakumiss mwaka mzimaa
 
darubin

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,419
2,000
Dar life tough sana mkuu asikwambie mtu, ubize wa kazi ni uongo wanahofia mbwembwe za kwamba wakon dar kumbe wanaishi vichochoroni. hata wewe ukihamia dar utakuwa kama wao amini usiamini huo ndo ukweli unless uwe na mkwaja mrefu sana
 
EBBAH

Member
May 8, 2017
75
125
DAR TATIZO SIO CHAKULA...TATIZO NI MALAZI..IKUMBUKWE DAR NI JIJI NA SIFA ZA JIJI ZINAFAHAMIKA..MALAZI HUWA JUU KUTOKANA NA WINGI WA WATU..HUDUMA ZA KIJAMII HUWA JUU PIA PAMOJA NA USAFIRI HII KUTOKANA NA UKUWAJI WA MAKAZI KUELEKEA NJE YA MJI.

SASA UKIONA MTU ANAKUKWEPA PENGINE WEWE NI MTU WAKUBEBA MIZIGO..UNAKUJA DAR NA GUNIA LA MAHINDI WAKATI MAHINDI YAPO TANDALE...UMESHUKA UBUNGO NA SUPER NAJUMNISA NDUGU/RAFIKI ANAISHI KITUNDA KIBEBERU....HIVI USHAWAZA HILO GUNIA LA MAHINDI AU FURUSHI LA VIAZI LINABEBWA WAPI? GHARAMA ZA KUCHUKUA BAJAJI ZITAZIDI HATA NAULI YAKO ULIYOKUJIA MJINI.HAPO LAZIMA UTAKWEPWA TU.

HUDUMA ZA KIJAMII..KUNA MAENEO MENGI HAYANA MAJI SEHEMU ZINGINE LITA 20 SH 500..ZINGNE SH 1000..HIVYO KUONGEZEKA KWAKO NI JIPU KWA WENYEJI TENA KAMA WANA KIPATO CHA CHINI.

MALAZI..CHUMBA CHA 50,000 DAR NI TAKATAKA..AMBAPO MKOANI UNAPATA ROOM MBILI TENA NZURI.SASA MTU ANA ROOM MOJA..LABDA TENA ANAISHI NA MWENZA..AU NA NDUGU MWINGINE..INAKUWA TABU..NA HATA KAMA KAPANGA NYUMBA NZIMA..ROOM ZITAKUWA CHACHE HIVYO UJIO LAZMA UTOLEWE TAARIFA MAPEMA.

KUMKURUPUSHA MWENYEJI PALE UNAPOFIKA MJINI NA KUMWAMBIA NIPO TU MJINI HAPA TUONANE..DAR KUBWA..KUFIKA SEHEM MOJA NI MUDA UNAHITAJIKA.UNAMSHTUKIZA MTU HATA KAMA ANA USAFIRI WAKE UMEFIKA UBUNGO NA YEYE WAKATI HUO YUPO KIGAMBONI LAKINI ANAKAA TABATA LABDA..NI WAZI ATAKUAMBIA KASAFIRI MAANA SIO KWA USUMBUFU HUO.

CHAKULA TU ..UTAPATA MAANA DAR CHAKULA NI RAHISI SANA UKIWA NA 1000 UNASHIBA VIZUUURI..UKIHITAJI MATUNDA MPAKA TIKITI LA TSH 200 UNAPATA..MIHOGO TEEELE..SAMAKI TEEELE N.K.HIVYO CHAKULA KWA MWENYEJI SIO ISHU.

NAULI YA KUTOKA SEHEMU MOJA KWENDA NYINGINE..MWENYEJI ANAISHI BUZA..UNATAKA AKUPELEKE COCO BEACH..GHARAMA ZOTE HIZO NI HESABU YA MEZA KWA SIKU..BADO HAPO KAMA KUNA MAENEO POSTA WATAKA KWENDA UKIHITAJI MWENYEJI..HIVYO UTAKUWA UNAKULA UNITS ZA MWENYEJI..MUDA PAMOJA NA SALIO.

ANGALIZO: UKIJA DAR USIJE NA MZIGO ZAIDI YA KIBEGI CHANGUO (HII ITASAIDIA KUDANDIA DALADALA KWA URAHISI)

UKIJA DAR UWE NA PESA YAKO KWAAJILI YAKUJILIPIA MAMBO MADOGO KAMA NAULI..KUTOKA SEHEM MOJA KWENDA NYINGINE HII ITAFANYA MWENYEJI AWE MCHANGAMFU KIDOGO

UKIJA DAR UJUE DAR NI KUBWA SI KAMA MKOANI UKIMHITAJI MTU BASI DAKIKA MBILI AMEFIKA..UKIAMBIWA SUBIRI UBUNGO SUBIRI TU HATA KAMA NI MASAA MATATU..USIKASIRIKE
 
LUCKDUBE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
2,126
2,000
USAFI WA MWILI UCHAFU ULIOKUBUHU MAENEO WANAYOKAAA.
SISTA DUU MABRAZAAA MEN SEHEMU MUHIMU KAMA VYOO BAFUU HATA MAZINGIRA YA NYUMBA ZAO NI BORA CHOO CHS KIJIJINIIII.
POLENIII SANA

9a2ba99a5db65120d1647f1f78385641.jpg
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom