Watu wa ardhi manispaa ya Kinondoni walisoma chuo gani?

Sikujui

New Member
Mar 26, 2019
2
1
Wasaalam wana JF.
Nashangazwa na watu wa ardhi wa Manispaa ya Kinondoni kama walisoma vizuri mambo ya ardhi. Kuna hii barabara iliyowekwa lami kutokea External kwenda Kisukuru inayopita jeshini. Upande wa kushoto ukishamaliza makazi ya watu unakutana na kona kali moja inaelekea makazi ya wanajeshi na nyingine inaendelea kuelekea kisukuru. Kwenye hiyo kona kali tena bondeni wamempa mtu anajenga pale sijui ni maduka au kituo cha mafuta maana hata bango hakuna. Kwa uelewa wa kawaida utaona ni bonde kubwa maana anayejenga anapambana sana kujaza kifusi. kama unadhani hapo walipitiawa, sasa endelea mbele ukishavuka shule ya Secondari Makamba unakutana na eneo ambalo ni bonde haswa upande wako wa kushoto. Hapo pia wamewapa watu viwanja wanapishana kupajaza vifusi na eneo lenyewe ni bonde hasa.
Suali kwa hawa maafisa ardhi, kwani haiwezekani eneo hili likabaki bila kujengwa nyumba ukizingatia ni sehemu ya bonde na hasa ile sheria ya mazingira ya mita 60 sijui kama zipo pale. Kama mliwabomolea watu wa jangwani na Kinondoni, eneo hili lina utofauti gani na kule?
 
Watu wengi wa ardhi wanasoma pae chuo cha ardhi karibu na Savei. Labda walifundishwa kuwa kila sehemu ni lazima iwekwe jengo. Who knows?
 
Mleta uzi kabla ya kutoa shutuma,nakushauri nenda ofc za Ardhi kinondoni ukapate ufafanuzi kuhusu hayo maendelezo yanayofanyika ktk maeneo uliyoyataja.Ukipata majibu uje utujulishe na wengine.Huko pia utapata majibu kuhusu elimu zao!!!
 
Wasaalam wana JF.
Nashangazwa na watu wa ardhi wa Manispaa ya Kinondoni kama walisoma vizuri mambo ya ardhi. Kuna hii barabara iliyowekwa lami kutokea External kwenda Kisukuru inayopita jeshini. Upande wa kushoto ukishamaliza makazi ya watu unakutana na kona kali moja inaelekea makazi ya wanajeshi na nyingine inaendelea kuelekea kisukuru. Kwenye hiyo kona kali tena bondeni wamempa mtu anajenga pale sijui ni maduka au kituo cha mafuta maana hata bango hakuna. Kwa uelewa wa kawaida utaona ni bonde kubwa maana anayejenga anapambana sana kujaza kifusi. kama unadhani hapo walipitiawa, sasa endelea mbele ukishavuka shule ya Secondari Makamba unakutana na eneo ambalo ni bonde haswa upande wako wa kushoto. Hapo pia wamewapa watu viwanja wanapishana kupajaza vifusi na eneo lenyewe ni bonde hasa.
Suali kwa hawa maafisa ardhi, kwani haiwezekani eneo hili likabaki bila kujengwa nyumba ukizingatia ni sehemu ya bonde na hasa ile sheria ya mazingira ya mita 60 sijui kama zipo pale. Kama mliwabomolea watu wa jangwani na Kinondoni, eneo hili lina utofauti gani na kule?
Uache kukariri dada yangu. Ukiwa na teknolojia lolote linawezekana hizo mita 60 ukienda hata ulaya huzikuti.
 
Siyo kwamba unawaonea hao maofsa ardhi wa Kinondoni? Hilo eneo ulilotaja halipo ndani ya manispaa ya Ubungo?
 
Uache kukariri dada yangu. Ukiwa na teknolojia lolote linawezekana hizo mita 60 ukienda hata ulaya huzikuti.
Hiyo teknolojia tunayo? Tungekuwa nayo yale mabasi ya mwendo kasi yasingekuwa yanapiga mbizi pale jangwani kila mwaka.
 
Back
Top Bottom