Bigbootylover
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 2,847
- 1,826
Umeshawahi kukaa na mtu ambaye anakutegemea kwa kila kitu hasa ndugu au watoto wa ndugu zako, yaaani we unampa sapoti katika kila kitu na anaelewa shida unazopitia, lakini ikitokea siku unashida au unanjaa yaani hapo home umekwama na unajua kabisa jamaa yuko vizuri na anaweza kukusapoti kwa siku hiyo au akakuazima japo hela kidogo ili MLE WOTE hapo hapo nyumbani LAKINI jamaa anakuwa tayari hata mlale njaa au udhalilike yaani hayuko tayari kuchangia au kutoa chochote. Hawa watu sijui huwa wanawaza nini, mtu unamsapoti kwa kila kitu lakini ikitokea siku umekwama hayuko tayari kuchangia hata buku mbili ya Unga, na anaweza kwenda kwao(kama mnakaa mjini yeye akaenda kuwaona wazazi kijijini) na asirudi hata na kadebe ka mahindi au mpunga na unajua kwao wanavyo hivyo vitu! UBINADAMU KAZI WAKUU