Watu Muhimu katika Historia ya Nchi yetu

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,958
Wakuu zangu ningependa sana kujua kwa nini nchi yetu haikuweka record za kumbukumbu ya watu muhimu ktk Historia ya nchi yetu. Watu ambao leo hii wangeitwa mashujaa wa kweli. Watu ambao sisi wengine hatuwajui wala tusingewajua kama sii kuulizia kwa watu.

Mbali na majina tunayoyafamu sote nimepewa majina haya kuwa hawa watu walikuwa muhimu sana ktk mchango wa kupatikana kwa Uhuru wetu.

Kwanza kuna Mzee Tambaza wa Magomeni Mikumi ambaye shule ya Tambaza imepewa jina lake, na Pili kuna Mzee Sheikh Amri Abeid naye wa Magomeni Mikumi ambaye pia uwanja wa mpira wa Arusha ulipewa jina lake.. Huyu mimi nilifikiria jina hilo limetokana na Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Amri Abeid Karume, kumbe huyu ni mtu mwingine kabisa.

Je, kuna majina mengine muhimu tuyafahamu? Na zaidi ya yote Upi mchango wao ktk Uhuru na maendeleo ya nchi yetu.

Inasikitisha sana kuona viongozi bora wa nchi hii wanateuliwa kutokana na elimu au umaarufu wao badala ya michango ya watu hao ktk kutuletea mafanikio..wanapoondoka huondoka na kila mazuri yao.
 
Hii Mada Ngumu...Labda na Ukipata Fursa mpgie simu Mzee KK umuulize Namna alivyomuokoa Nyerere na Mapinduzi...!!!
 
Mkuu
Mimi na mtizamo tofauti kidogo wenda tukubaliane huu utofauti kuwepo kulingana na jinsi tulivolelewa na fani zetu mimi kama Engineer sioni haja yoyote wakijulikana ktk historia then what? Hiyo historia inawatosha sana.

Haya mambo kweli mimi binafsi siyapendi na yaniudhi eti utasikia Nyerere angekuwepo ama Nyerere alifanya hivi na vile mara hivi na vile kambona.
 
Mkandara,

Umeleta mada ngumu kweli ambayo kama wadau watakubaliana na ukweli itasaidia kufumbua macho watu wengi, kuna watu hata wasomi ukiwauliza kwanini kuna wodi ya kibasila au sewa haji pale Muhimbili hawezi kukwambia, au watu kama Selemani Mamba, Nkosi Chabruma Tawete wa Gumbiro na mashujaa chungu nzima waliomwaga damu na jasho lao ili mm na ww tuwe watu huru leo, hawatajwi kabisaaa.

Hili ni tatizo la nchi kuwa katika utawala wa kikandamizaji kwa muda mrefu. Honestly blame it to Baba wa taifa ambaye alijali umaarufu wake tu wengine a a a!
 
Lets start making history by telling watu wa makumbusho kuanza kuanda historia za watu mhimu kama magufuli aliyekamilisha ndoa ya kusafiri kwa tax toka ntwara hadi mwanza, JK nayeongoza nchi kwa remote while he in USA or mzee nkapa who made everything in this country for private investors na mtaji wa masikini ni guvu zake etc..
 
Haya ndio matokeo ya mwalim julius aka mchonga,yeye alitaka historia ya tanzania imwimbe yeye kila kona na alifanikiwa kwa hilo
 
nakumbuka mzee sykes(baba wa aliyekuwa wa dar) alishawahi kuhojiwa na gazeti moja bongo(jina limenitoka)akamlaumu nyerere kwa kuipindisha historia ya tanzania na akasema kuwa yeye ni mmoja wa watu waliompokea nyerere tanu akiwa na kaptula,wakamfundisha jinsi ya kuvaa suruali ili akubalike na watu pwani katika harakati za kupigania uhuru,akaongeza kuwa yeye sykes ndie aliyetoa pesa za kuchapa kadi za uanachama wa tanu
 
watu muhimu walikuwa waswahili waliomvalisha Nyerere kaptula na siku uhuru waliachwa chini huku kule juu aliwachukua akina Kambona na wagala wenzie the rest is history

sasa mnaona woga gani kulisema hilo?
 
watu muhimu walikuwa waswahili waliomvalisha Nyerere kaptula na siku uhuru waliachwa chini huku kule juu aliwachukua akina Kambona na wagala wenzie the rest is history

sasa mnaona woga gani kulisema hilo?

kaka,nyerere alikuja na kaptula,waswahili ndio wakamvalisha suruali ili aonekane mstaarabu
 
kaka,nyerere alikuja na kaptula,waswahili ndio wakamvalisha suruali ili aonekane mstaarabu

na katiika hao waliomvalisha kaptula walikuwa ni akina Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Said Omari Abdallah, Tewa Said Tewa, Katibu wa EAMWS enzi hizio Abdul-Aziz Khaki na mzee wa TANU Mzee Mwinjuma Mwinyikambi; Makisi Mbwana, Issa Mtambo, Omari Muhaji na Saleh Masasi

unless bwana Mkandara aataka listi nyingine tofauti
 
na katiika hao waliomvalisha kaptula walikuwa ni akina sheikh hassan bin amir, sheikh said omari abdallah, tewa said tewa, katibu wa eamws enzi hizio abdul-aziz khaki na mzee wa tanu mzee mwinjuma mwinyikambi; makisi mbwana, issa mtambo, omari muhaji na saleh masasi

unless bwana mkandara aataka listi nyingine tofauti

aziz ally..
 
Historia itabadilishwa baada ya CCM kumaliza muda wa kutawala nchi; miaka 15 au 20 inayokuja. Katiba itabadilishwa pia. Watanzania wengi wameshaelimika sasa; hivi kitu ambacho hakikuwepo wakati wa Nyerere.
 
aziz ally..

Si huyo tuu kuna unsung heroes kama akina Ramadhani Mashado Plantan ambaye alivunja ukiritimba baina ya serikali na Wamishionari. Akifuata nyayo za Erika Fiah, Mwafrika wa kwanza kuchapisha gazeti katika Tanganyika, Mashado alianzisha gazeti lake Zuhra.

sasa mkandara sihui kama yupo au ndio kakimbia...maana humu utaona watoto wadogo wanakuja kutaka kuleta ubishi usio na kichwa wala miguuu...hivyo mkae mkijua kuwa kabla ya Mengi alikuwepo bwana RAMADHANI MASHADO
 
Historia itabadilishwa baada ya CCM kumaliza muda wa kutawala nchi; miaka 15 au 20 inayokuja. Katiba itabadilishwa pia. Watanzania wengi wameshaelimika sasa; hivi kitu ambacho hakikuwepo wakati wa Nyerere.

Ndio waTanzania wengi wameelimika na hili ni zuri lakini wengi kati ya hao the so called EDUCATED ELITE ni members wa JAMII FORUMS ambao bado wanaamini kuwa kama si Nyerere tusingepata uhuru

wanasahu kuwa pamoja na waswahili kumsaidia pia walikuwepo watu toka fani mbali mbali kama washairi ambao walitunga beti za kuwasifu Wafalme na Malkia wa Uingereza pamoja na nasaba yao.Lakini Ghafla baada ya kuundwa kwa TANU palitokea mageuzi ya maudhui katika tungo za mashairi na tenzi....
( na hiki ndicho wanachokifanya CUF kwenye mikutano yao ) Washairi waliacha kumsifu na kumtukuza Mfalme na Malkia wa Uingereza wakiongozwa na Saadani Abdu Kandoro walianza kutunga mashairi yenye ujumbe wa kizalendo wakimsifu Juliasi Nyerere na TANU.

Mara tu baada ya marekebisho hayo ya sheria Mohamed Suleiman, mshairi hodari akijulikana sana kwa jina lake la ushairi la - 'Mtu Chake', alikamatwa, akatiwa ndani na kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kilichokuwa na sifa mbaya ya ukatili...ambao apparently unaendelea mpaka leo,

Anyway Mtu Chake alikuwa ametunga mashairi ya kuvutia sana kuhusu Nyerere, TANU, utaifa, mshikamano, udugu, upendo na wakati huo huo kuwakejeli Waingereza.

Nani asiyejua kuwa BANTU GROUP iliundwa mahsusi kuwapiga vita WASWAHILI ndani ya TANU ( halafu leo waswahili waashangaa iweje wamesahaulika kumbe fitna ilifanywa tangu enzi za TANU)

All in all BANTU ilifanikiwa sana katika katika hili hadi kudiriki kupiga marufuku mamkuzi ya Waislamu ya Asalaam Alaikum (Amani iwe juu yako) baina ya Waislamu kwa msingi kuwa ilikuwa inawabagua Wakristo na hivyo inawatenga!!!!


Mkandara upo?
 
na katiika hao waliomvalisha kaptula walikuwa ni akina Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Said Omari Abdallah, Tewa Said Tewa, Katibu wa EAMWS enzi hizio Abdul-Aziz Khaki na mzee wa TANU Mzee Mwinjuma Mwinyikambi; Makisi Mbwana, Issa Mtambo, Omari Muhaji na Saleh Masasi

unless bwana Mkandara aataka listi nyingine tofauti
Nilitangulia kusema kuwa Mkandara kaleta maada hii lakini watu wapo tayari kukubali ukweli?
Nlijuwa majina haya yatakuja tu na aliyeyapoteza au kusabibisha yapotee anajuulikana. Hawa ndo walikuwa wenye mji i.e wazee wa Mujini wakati huo. Mwalimu akaja kuwaita "...Mamwinyi tu hawa....waswahili tu hawa....n.k..." akawatupilia mbali baada ya kwisha tumia makasha yao.
 
Kuna msemo wa Kiingereza usemao "History is written by the winners." Nina uhakika pia kuna Watanganyika na Wazaznibari walio changia kupatikana kwa uhuru wetu nje ya TANU na ASP. Ila kwa sababu ushindi unaonekana ulikuwa wa TANU na ASP basi ni watu wa vyama hivyo tu wanaoongelewa. Na hata ndani ya hivyo vyama napo kuna the "winners" and "losers" na historia ikaandikwa na kusisitizwa na washindi. It may be sad but it's the reality. Endeleeni kutu tajia majina yaliyo sahaulika wakuu.
 
kaka,nyerere alikuja na kaptula,waswahili ndio wakamvalisha suruali ili aonekane mstaarabu
Leta picha



=======

Watu wengine waliosahaulika ni pamoja na Kasela Bantu, Oscar Kambona, Field Marshall Okelo, na yule jamaa mweingien wa Zanzibar aliyekimbilia Guinea Bissau halafu akarudi na kunyongwa (sikumbuki tena jina lake kwa vile kasahaulika kabisa)
 
Nilitangulia kusema kuwa Mkandara kaleta maada hii lakini watu wapo tayari kukubali ukweli?
Nlijuwa majina haya yatakuja tu na aliyeyapoteza au kusabibisha yapotee anajuulikana. Hawa ndo walikuwa wenye mji i.e wazee wa Mujini wakati huo. Mwalimu akaja kuwaita "...Mamwinyi tu hawa....waswahili tu hawa....n.k..." akawatupilia mbali baada ya kwisha tumia makasha yao.

ukweli unauma lakini huwezi kuzungumzia historia ya nchi yetu bila kumtaja Sheikh Suleiman Takadir then kulikuwa na akina Mzee Fundi Muhindi mwanasiasa mkongwe, muasisi wa African Association Tabora, kulikuwa na Idd Faiz Mafongothen kulikuwa na Ali Mwinyi Tambwe (sina hakika kama ana uhusiano wowote na balozi Tambwe bba yake abdurabi lakini FMESanaweza kuniweka sawa)....leo hii watu wanashangaa ilikuwaje wamanyanyema waliikamata Kariakoo lakini ukweli ni kuwa huwezi kuzngumzia hilo bila kujua chombo kilichokuwa kinaitwa BATETERA UNION (Congo Association) chama kilichokuwa kikiwaunganisha Wamanyema wa Tanganyika na Mzee bin Sudi ndie inasemekana alikuwa muasisi wa chama hiki unless Mkandara aje kunikosoa lakini ukweli ni kuwa Batetera Union kilikuwa chama kilichoshikamana na chenye nguvu sana miongoni mwa vyama vya kikabila. Wamanyema ni kabila la Waislam watupu na kwa sababu hii hakukuwa na pingamizi katika kuunga mkono TANU enzi hizo

mnataka zaidi? hamuwezi kupata zaidi kwa kukaaa kwenye computer zenu na kwenye mapango mkienda Dar..mambo haya adimu lazima upite pale nje ya msikiti wa MANYEMA jioni baada ya swala ya ALAASIRI ndio utakjua kama historia toka kwa wazee wetu pale

watoto wa KARIAKOO wanajua historia hii na angekuwepo MSWAHILI angekuwa anawapa viapnde adimu kabisa

anyway kwa kuendelea ni kuwa BATETERA UNIONBatetera Union ilikuwa na nguvu sana kiuchumi kwa kuwa kilikuwa katika wafuasi wake, watu waliomiliki majumba na walihodhi takriban nusu ya nyumba zilizojengwa mjini Dar es Salaam kati ya vita kuu mbili za dunia...(sitozungumzia WARAMO tulivyongizwa mjini na wanawake wa kimanyema) hapa lakini nayo inahitaji muda kuizungumzia


Anyway, Uuwezo huu wa kiuchumu uliwafanya Wamanyema kuwa wapinzani wagumu wa serikali ya kikoloni na uliwanyanyua hadi kufikia kuwa mbele katika siasa mjini Dar es Salaam na katika miji mingine ya Tanganyika ya enzi hizoooooooooooo. Kwa msiojua tuu ni kuwa Umoja wa Wamanyema ndiyo uliojenga msikiti maarufu wa Wamanyema mwaka 1912 uliokuwa karibu na makao makuu ya African Association...msio jua msikiti huu uko wapi basi si kazi sana upo pale karibu na Lumumba CC lakini kwa nyuma kidogo...

Zaidi ya kuwa na wanawake wazuri , ukweli ni kuwa wamanyema wanajulikana kama watu wenye damu ya kali na wana sifa ya ushujaa....unaambiwa Mmanyema anaweza kuulipia fedha ugomvi ili na yeye awemo, na kadri mpinzani anavyokuwa na nguvu na hodari, ndivyo Mmanyema anavyofaidi ugomvi wake na unaambiwa katika siku hizo Wamanyema walikuwa wameshikwa katika magomvi.

nimetoka kidogo nje ya topiki lakini huwezi kutaja watu bila kutaja struggles za enzi hizo

Mambo adimu kama haya huwezi kupata mapaka ukae na kina mzee KATUNGUNYA ndio mntajua
 
Leta picha



=======

Watu wengine waliosahaulika ni pamoja na Kasela Bantu, Oscar Kambona, Field Marshall Okelo, na yule jamaa mweingien wa Zanzibar aliyekimbilia Guinea Bissau halafu akarudi na kunyongwa (sikumbuki tena jina lake kwa vile kasahaulika kabisa)
unazungumzia watoto wa jana hao...lakini kabla ya hao kulikuwa na akina Abdu Kandoro, Japhet Kirilo na Abbas Sykes na Ramadhani Mashado Plantan katika gazeti lake Zuhra. Mtambo wa gazeti wa Mashado uliokuwa Mtaa wa Ndanda, Mission Quarters kama unapajua hapo mission quarters kwenyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom