alisema nini shiekh takadir?
Yaani turudi chini ya wakoloni tu!Hakuna cha Nyerere wala Kawawa. Mtu muhimu kwa Tanganyika ni Karl Peter tu. Mtake msitake.
watu muhimu walikuwa waswahili waliomvalisha Nyerere kaptula na siku uhuru waliachwa chini huku kule juu aliwachukua akina Kambona na wagala wenzie the rest is history
sasa mnaona woga gani kulisema hilo?
na katiika hao waliomvalisha kaptula walikuwa ni akina Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Said Omari Abdallah, Tewa Said Tewa, Katibu wa EAMWS enzi hizio Abdul-Aziz Khaki na mzee wa TANU Mzee Mwinjuma Mwinyikambi; Makisi Mbwana, Issa Mtambo, Omari Muhaji na Saleh Masasi
unless bwana Mkandara aataka listi nyingine tofauti
hivi watu wengine mnavyo andika kitu mnakuwa mmekunywa au kuvuta au ndio hivyo tena kuandika ili uonekane umeandika. kama unajua historia tanu ilianzishwa na kuasisiwa nyerere akiwa tayari katika harakati za kuleta uhuru, sasa hiyo ya kusema ilikuwepo tokea akiwa ana nyonya si ni kujidanganya wewe mwenyewe? au ndio huko kutokujua historia go back to you history books uone tanu ilianzishwa lini. au ndio hivyo shule less halafu unataka kupewa uongozi, na ukishindwa unasema una hujumiwa.Wataanzia wapi wanabaki Hi! he! nafikiri kwanza wanalinganisha mtindi ulioutowa hapo juu na ule waliopewa na baba wa taifa kama unalingana, na bado waambiew vizuri kuwa hiyo TANU anayojivunia Nyerere kuiasisi ilikuwapo tokea yeye ananyonya,
Sasa mtoto wa mjini hapo nani? Nani aliyewaingiza mjini wenzie? Mie naona Nyerere ni kiboko, mmemvalisha kaptula akawaacha kwenye mataa! Ahhhh! Akatawala miaka 24 mlikuwa hamtaji hizo kaptula. Kafa mnaanza umbeya.
Mbona huwa hamsemi vile vile mlikuwa mnauza watumwa!!
Lakini kule kwetu Shujaa wa Tanzania tunayemkumbuka ni Mkwawa!! Hata ukipita barabarani pale Lugalo Iringa unaona lile "mass grave" la nyundo!
Kwani hapa tunaangalia Shujaa Mswahili au Shujaa Mtanzania?? Kule huwa hatujali Mswahili, mpagani au nani, kavaa lubega, kaptula au suruali wote twende tu!Kwani Hujui Mkwawa alikuwa Mswahili?
Halafu inaelekea kweli hatufikiri. Nyie huyu Nyerere kasoma lini? Halafu Nyie mmemvika hiyo suruali au sijui, nani wa kuvikwa suruali? Nyerere kasoma kabla hata hamjaanza kudai Uhuru; au kwa sababu kafa ndiyo mnaanza uongo? Wakati ule Elimu yake tu ilibidi kuwa yeye awe kafunguka zaidi ya hao mnaowasema. Hivi hao wazee wote na ile population ya Dar wkati ule ilmshindwa mtu mmjoa aitwaye Nyerere? La, huyu jamaa alikuwa intelligent kuwazidi wengi wakati huo, na mie naamini kwa wakati ule Wengi walimwona wa maana.hivi watu wengine mnavyo andika kitu mnakuwa mmekunywa au kuvuta au ndio hivyo tena kuandika ili uonekane umeandika. kama unajua historia tanu ilianzishwa na kuasisiwa nyerere akiwa tayari katika harakati za kuleta uhuru, sasa hiyo ya kusema ilikuwepo tokea akiwa ana nyonya si ni kujidanganya wewe mwenyewe? au ndio huko kutokujua historia go back to you history books uone tanu ilianzishwa lini. au ndio hivyo shule less halafu unataka kupewa uongozi, na ukishindwa unasema una hujumiwa.
Honestly blame it to Baba wa taifa ambaye alijali umaarufu wake tu wengine a a a!!![/QUOTE] [/B]
Mwacheni Mtumishi wa Mungu apumzike kwa amani. Tukishamlaum baba wa Taifa so what! Lets stop the blame game jamani! Mwalimu alikiri mara kadhaa kwamba kamwe hakuwa malaika kuna aliyoharibu na aliyojitahidi. Wajibu wetu ni kuendeleza mazuri na kuyaacha ya kijinga. kwa kuwa unajua udhaifu wa mchonga, anzia hapo kurekebisha.
Mkandara,Wakuu zangu,
Kusema kweli nimeileta mada hii kwa mtazamo wazi kabisa na sio ule unaoitwa NDIVYO TULIVYO kwani mara nyingi tunajaribu kuvuta hoja za kidini ktk WATU washuhuri ambao waliweza kubadilisha historia ya nchi yetu..Tuklumbuke tu utukufu wa mtu ni kwa yale alofanya na sio kwa majina au dini zao..Hivi kweli Mkandara hapa ningekuwa sina dini ningekuwa na mtazamo tofauti wa viongozi wetu?..Ningemsifia Lowassa na Mkapa kwa sababu wao ni Wakristu na kutupilia mbali madai yote ya Ufisadi! I don't think so.....
Sisi sote hapa ni matunda ya nguvu za hawa wazee, iwe, isiwe kwani navyoelewa mimi hiyo Magomeni Mikumi ndiko chanzo cha nguvu zote za uhuru na walikaa watu wa kila dini na makabila.
Ndiko alikokuwa akikaa Kawawa, Kambona, Saadan Kandoro, Nyerere na wengine wengi tu ambao kwa njiaq moja ama nyingine walichangia sana ktk Uhuru wetu... Jamani hatujafika hata miaka hamsini, watu hawaoni umuhimu wa watu wale isipokuwa wale waliopanda mlima Kilimanjaro na kutembea kwa miguu kuunga Azimio la Arusha..mbona hao hamwatambui kwa dini zao?..
Tuwe makini sana ktk maswala haya wakuu zangu tafadhalini kwani JK leo anayafanya anayoyafanya sii kwa sababu ni Muislaam wala Lowassa kwa sababu ni Mkristu. hawa watu hata kama wasngekuwa karibu na Mungu kiasi gani bado wangeyafanya waloyafanya kwa sababu ndio upeo wa AKLI zao ktk Ufahamu walizopewa...
Kuna majina mengine ambayo yamepewa ward za Wagonjwa Muhimbili kina ambao pia walikuwa muhimu sana isipokuwa leo hii tunabakia na majina bila kuelewa vizuri mchango wao..
Waswahili wanasema usipojua ulikotoka ni vigumu sana kwenda mbele... na hakika sababu zote za kushindwa kwetu kuendelea zinachangiwa na kutofahamu tulikotoka, hivyo tunapuyanga tu bila Malengo.. Kila mtu akianza safari huwa na fikra ya wapi anakwenda na mara zote hufuata njia ambayo itamfikisha ktk safari yake...Sasa sisi kama tunaenda mbila dira hatujui tumetoka wapi tumerukia bandwagon katikati ya safari maadam linasafiri inawezekana kabisa kuwa tunarudishwa nyuma..Na ndio maana Wadanganyika wengi hawakubaliani na data za maendeleo yetu hata kidogo...kwani hatujui tulikotoka.
Hawa watu tunaowazungumza humu ni muhimu sana na hakika ningependa sana kuelewa maisha na michango yao ktk nchi yetu..
Hakuna cha Nyerere wala Kawawa. Mtu muhimu kwa Tanganyika ni Karl Peter tu. Mtake msitake.[/QUOTE]
Una haki ya kutoa maoni yako kaka.