Watu msibani na makabulini wanalia na mengi

P Didy Wa Tanzania

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
Nadhani kila mtu anajua kuwa makabulini sio sehemu ya furaha . ni sehemu ambayo tumepumzisha miili ya ndugu zetu, marafiki zetu ,naa wapendwa wetu inawezekana tulikuwa tunatamani sana leo hii tungekuwa nao ila mungu kawapenda zaidi.

Japo kiimani tunaamini bado wapo na sisi ila kimwili hatupo nao. tunamiss ushauri wao, story nao , makuzi nao ila ndo hawapo sasa.

Kumbukumbu zao bado zinaishi katika akili zetu. kumbukumbu zinatutesa.

Swala la msiba likitokea watu wakalia ni swala la kawaida tu. maana msibani sio sehemu ya furaha kabisa. lakini mengi tusiyoyajua kuwa watu msibani ulia kwa kuwaza mengi sana kuhusu marehemu.

Nitaandika visa vitatu ambavyo nimewahi kuvishuhudia nadhani utajifunza kitu.

1. Marehemu jose nakumbuka kipindi hiko nipo darasa la kwanza nilipataga rafiki anaitwa jose. tulikuwa marafiki sana yani mda wote nipo nae nikirudi nyumbani nikibadilisha nguo nikila safari kwa jose. mara nyingi nilikuwa nikienda kwa kina jose narudi na matunda maana pale kwao kulikuwa na matunda mengi sana .

Wazazi wangu walikuwa wananikataza sana urafiki na jose kwanza kwa kina jose kulikuwa mbali cha pili dini zilikuwa tofauti nadhani ili la pili ndo wazazi walilitazama zaidi. maisha ya shule kwa kipindi kile yalikuwa magumu kiasi chake na yalisababishwa na mwalimu ambae alikuwa katokea tu kutuchukia mimi na jose.

Zikapita siku kama mbili hivi sikwenda kwa kina jose ila nilienda kwao kinamkuta anaumwa yupo yeye na dada yake. nikamwambia mpelekeni hospital . sikujua kama walimpeleka au vipi lakini taarifa iliyokuja siku ya pili jose kafariki.

Kitu cha ajabu ambacho nilikuona siku ambayo tunachaguliwa watoto wa kwenda kuwakilisha msibani. yule mwalimu alichagua watoto kama 10 hivi lakini mimi akunichagua. lakini wanafunzi wengine wakasema huyu ndo alikuwa rafiki yake sana kwahiyo na mimi nikaweka kwenye list ya kwenda msibani.

Tulivyofika msibani yule mwalimu ambae alikuwa ananichukia mimi na jose alikuwa analia sana msibani. alilia sana lile tukio mpaka leo hii silipatii jibu kwanini alie vile wakati yeye alikuwa apendi hata kutuona .

Nilivyofika nyumbani pia nillivyowaambia jose kafariki nao wakasikitika sana. niliwaambia neno moja munasikitika kwa vile matunda hayatokuja tena au . hawakunijubu.

Mpaka leo hii kwenye lile eneo alilizikwa jose napita lakini sijui kabuli la jose lipo eneo gani. siku anazikwa nilishindwa kusogea eneo la makabulini sijui kabuli la jose lipoje ila ninachojua katika yale makabuli. kuna kabuli moja la rafiki yangu wa utotoni jose

2. Kuna siku nilienda msibani mda wa kumpumzisha ndugu yetu. ila wakati mwili ule unawekwa kwenye mwanandani kuna jamaa alililia sana akataja neno "mama". daah yani na mimi mwili wote ulinisisimka jamaa alilia sana kama mtoto mdogo.

Tukazika pale tukaondoka nilivyofika nyumbani nilimpigia mama yangu kumjulia hali tu nikawasiliana nae nafsi yangu na akili yangu ikatulia. ila jana nikakumbuka lile tukio tena mda uo nilikuwa nipo na baba yangu mdogo. nikamuadithia lile tukio la kule makabulini na yeye siku ya maziko alikuwepo ndo akaniambia " MAKABULINI WATU WANALIA NA MENGI".

Akaniambia yule jamaa wa siku zile aliyekuwa analia makabulini wakati tunazika. ni mtoto wa marehemu ( yani yule ambae tulikuwa tunamzika ).

Jamaa wakati mama yake anaumwa hakuwahi hata siku moja kwenda kumuona. alikuwa busy sana na mambo yake hata alipopigiwa simu na mama yake alipokea lakini aliendelea kupuuzia sasa mama yake kafa lakini hakumuona na hakuwahi kupata neno lolote lile kutoka kwa mama yake.

3. Kisa cha tatu kuna sehemu tulienda kuzika aliyekufa ni mama yake na rafiki yangu nakumbuka kabla ya kifo yule bibi aliumwa sana. mpaka ukamfika umauti. rafiki yangu alikuwa yupo karibu sana na mama yake. lakini wazazi wake waliachana enzi hizo za uiana kwahiyo malezi yake aliyapata akiwa kwa mama zaidi.

Miaka ikaenda mama yule akafa siku tunaenda kuzika. tushamaliza kuzika yule rafiki yangu alilia sana pale kabulini tulimsuburi kama nusu saa yani watu wote walikuwa washaondoka tulibakia mimi na yeye tu

Nakumbuka aliniambia nimemkosea sana mama nikamuuliza umemkosea nini akanijibu kuwa wakati mama yupo hai alinipa maagizo nikamchukue baba ana maongezi nae nilimpuuzia lakini siku ambayo nilienda kumchukua baba kwake nikamleta kwa mama. Mama alikuwa hawezi tena kuzungumza chochote kile na kama unavyojua wazee wa zamani hawajui hata kuandika kwahiyo mama alibakia tu kutokwa na machozi mbele yangu maana kuongea na hawezi ila natamani sana mda urudi nyuma ile siku ambayo angeniambia nimfate baba ningemfata mda ule ule.

Kutokana na matukio yote ayo basi tujifunze kujali mda na kuwaheshimu na kuomba msamaha haraka sana pale tunapohisi tumekosea au kumkwaza mtu.
 
Ujumbe mzuri kaka.
Wengi tunakumbuka kuonesha upendo angali tushachelewa. Yanabaki majuto.

Ukiwa hai unaweza kuwapuuza watu wasiostahili kupuuzwa
Kuwachukia wasiostahili kuchukiuwa

Kuna nguvu katika kupenda na kupendana hutokuja kujuta ukifanya hivyo na hata pale ndugu au jamaa yako akitoweka duniani basi utabaki na amani
 
Umenikumbusha kisa kimoja na marehemu bibi yangu wa kambo.
Bibi alikuwa na wajukuu 2 Mimi wa kambo na mmoja Mtoto wa marehemu Binti yake
Basi yule bibi akaanza kuumwa, akamtafuta mjukuu wake akampotezea, akapiga simu weee jamaa haendi!!akamwambambia nataka nije niongee na wewe nifie kwako jamaaa kimyaaa.
Yule bibi akapata option ya pili akanipigia Mimi!!
Siku inayo fuata nikamfuata,wiki Moja kabla hajafa akaomba niwaite viongozi wa Kijiji alikotoka!
Nikawaita, hapo ilibidi nitume nauli!
Bibi akawaambia anaomba mashamba yake, yoote anipe Mimi mbele Yao, walipotoka tu akanambia unajua shamba flani?? Nikasema ndio akanambia mjukuu wangu lile shamba Lina mgodi!! Ndio zawadi yako niliyo kutunzia ileee, na akanielekeza Hadi alama alivyoweka! Siku ya 3 akafa!! Nilienda baada ya mazishi, mambo kweli yapo!!
Msipuuzie mnapoitwa na wagonjwa Kwa kukwepa majukumu
 
Jamaa ajakumaind kwel au hajakuleta usumbufu wowote ule
 
Ujumbe mzuri kaka.
Wengi tunakumbuka kuonesha upendo angali tushachelewa. Yanabaki majuto.

Ukiwa hai unaweza kuwapuuza watu wasiostahili kupuuzwa
Kuwachukia wasiostahili kuchukiuwa

Kuna nguvu katika kupenda na kupendana hutokuja kujuta ukifanya hivyo na hata pale ndugu au jamaa yako akitoweka duniani basi utabaki na amani
🤝🤝🤝 weng tunaonesha upendo kwa mtu wakati mda ambao sio sahihi.
 
Hapana!! Anajutia tu kwa uzembe wake, ila nimetumia busara ya kibinaadamu tu Ili naye anufaike kiasi
aaah jambo zuri sana umefanya mkuu ila nadhan amejifunza sana na mpaka kesh kama yupo hai basi anajutia aliyoyafanya
 
Mtu akiwa anapitia Magumu unabidi usimkimbie you have to wait till final , watu wengi wakisikia Mtu anaumwa Basi wanamkimbia hawataki hata kwenda kumuona na kumjulia Hali

Mbaya zaidi na kubwa kuliko zote ni pale unapomkimbia Mzazi/wazazi or any someone who raised you up
 
Nadhani kila mtu anajua kuwa makabulini sio sehemu ya furaha . ni sehemu ambayo tumepumzisha miili ya ndugu zetu, marafiki zetu ,naa wapendwa wetu inawezekana tulikuwa tunatamani sana leo hii tungekuwa nao ila mungu kawapenda zaidi.

Japo kiimani tunaamini bado wapo na sisi ila kimwili hatupo nao. tunamiss ushauri wao, story nao , makuzi nao ila ndo hawapo sasa.

Kumbukumbu zao bado zinaishi katika akili zetu. kumbukumbu zinatutesa.

Swala la msiba likitokea watu wakalia ni swala la kawaida tu. maana msibani sio sehemu ya furaha kabisa. lakini mengi tusiyoyajua kuwa watu msibani ulia kwa kuwaza mengi sana kuhusu marehemu.

Nitaandika visa vitatu ambavyo nimewahi kuvishuhudia nadhani utajifunza kitu.

1. Marehemu jose nakumbuka kipindi hiko nipo darasa la kwanza nilipataga rafiki anaitwa jose. tulikuwa marafiki sana yani mda wote nipo nae nikirudi nyumbani nikibadilisha nguo nikila safari kwa jose. mara nyingi nilikuwa nikienda kwa kina jose narudi na matunda maana pale kwao kulikuwa na matunda mengi sana .

Wazazi wangu walikuwa wananikataza sana urafiki na jose kwanza kwa kina jose kulikuwa mbali cha pili dini zilikuwa tofauti nadhani ili la pili ndo wazazi walilitazama zaidi. maisha ya shule kwa kipindi kile yalikuwa magumu kiasi chake na yalisababishwa na mwalimu ambae alikuwa katokea tu kutuchukia mimi na jose.

Zikapita siku kama mbili hivi sikwenda kwa kina jose ila nilienda kwao kinamkuta anaumwa yupo yeye na dada yake. nikamwambia mpelekeni hospital . sikujua kama walimpeleka au vipi lakini taarifa iliyokuja siku ya pili jose kafariki.

Kitu cha ajabu ambacho nilikuona siku ambayo tunachaguliwa watoto wa kwenda kuwakilisha msibani. yule mwalimu alichagua watoto kama 10 hivi lakini mimi akunichagua. lakini wanafunzi wengine wakasema huyu ndo alikuwa rafiki yake sana kwahiyo na mimi nikaweka kwenye list ya kwenda msibani.

Tulivyofika msibani yule mwalimu ambae alikuwa ananichukia mimi na jose alikuwa analia sana msibani. alilia sana lile tukio mpaka leo hii silipatii jibu kwanini alie vile wakati yeye alikuwa apendi hata kutuona .

Nilivyofika nyumbani pia nillivyowaambia jose kafariki nao wakasikitika sana. niliwaambia neno moja munasikitika kwa vile matunda hayatokuja tena au . hawakunijubu.

Mpaka leo hii kwenye lile eneo alilizikwa jose napita lakini sijui kabuli la jose lipo eneo gani. siku anazikwa nilishindwa kusogea eneo la makabulini sijui kabuli la jose lipoje ila ninachojua katika yale makabuli. kuna kabuli moja la rafiki yangu wa utotoni jose

2. Kuna siku nilienda msibani mda wa kumpumzisha ndugu yetu. ila wakati mwili ule unawekwa kwenye mwanandani kuna jamaa alililia sana akataja neno "mama". daah yani na mimi mwili wote ulinisisimka jamaa alilia sana kama mtoto mdogo.

Tukazika pale tukaondoka nilivyofika nyumbani nilimpigia mama yangu kumjulia hali tu nikawasiliana nae nafsi yangu na akili yangu ikatulia. ila jana nikakumbuka lile tukio tena mda uo nilikuwa nipo na baba yangu mdogo. nikamuadithia lile tukio la kule makabulini na yeye siku ya maziko alikuwepo ndo akaniambia " MAKABULINI WATU WANALIA NA MENGI".

Akaniambia yule jamaa wa siku zile aliyekuwa analia makabulini wakati tunazika. ni mtoto wa marehemu ( yani yule ambae tulikuwa tunamzika ).

Jamaa wakati mama yake anaumwa hakuwahi hata siku moja kwenda kumuona. alikuwa busy sana na mambo yake hata alipopigiwa simu na mama yake alipokea lakini aliendelea kupuuzia sasa mama yake kafa lakini hakumuona na hakuwahi kupata neno lolote lile kutoka kwa mama yake.

3. Kisa cha tatu kuna sehemu tulienda kuzika aliyekufa ni mama yake na rafiki yangu nakumbuka kabla ya kifo yule bibi aliumwa sana. mpaka ukamfika umauti. rafiki yangu alikuwa yupo karibu sana na mama yake. lakini wazazi wake waliachana enzi hizo za uiana kwahiyo malezi yake aliyapata akiwa kwa mama zaidi.

Miaka ikaenda mama yule akafa siku tunaenda kuzika. tushamaliza kuzika yule rafiki yangu alilia sana pale kabulini tulimsuburi kama nusu saa yani watu wote walikuwa washaondoka tulibakia mimi na yeye tu

Nakumbuka aliniambia nimemkosea sana mama nikamuuliza umemkosea nini akanijibu kuwa wakati mama yupo hai alinipa maagizo nikamchukue baba ana maongezi nae nilimpuuzia lakini siku ambayo nilienda kumchukua baba kwake nikamleta kwa mama. Mama alikuwa hawezi tena kuzungumza chochote kile na kama unavyojua wazee wa zamani hawajui hata kuandika kwahiyo mama alibakia tu kutokwa na machozi mbele yangu maana kuongea na hawezi ila natamani sana mda urudi nyuma ile siku ambayo angeniambia nimfate baba ningemfata mda ule ule.

Kutokana na matukio yote ayo basi tujifunze kujali mda na kuwaheshimu na kuomba msamaha haraka sana pale tunapohisi tumekosea au kumkwaza mtu.
Umuhmu wa mtu huonekana pale asipokuepo
 
Kuna vijana wana viburi sana mbele ya wazazi wao,wazazi wakifa wanajifa wanauchungu na kulia nyenye nyenye huwa nachukia sana.
 
Back
Top Bottom