Freelancer
JF-Expert Member
- Sep 22, 2008
- 2,950
- 2,149
Kuna mada nyingi sana huwa naziona hapa jamii forums kwenye MMU zikianzishwa na wakina dada wengi wakizungumzia kwamba hawawezi kutoka na wanaume wasio na hela au wanaume suruali. Hata wanaume wenye hela wengi sidhani kama wapo tayari kutoka na wanawake wenye mtazamo huo. Kwa hiyo naweza sema hawa wadada wanafukuza upepo tu. Hakuna mwanume aliye na mafanikio atakuwa tayari kuji associate na mwanamke ambaye hajitambui. Tunaongelea mwanume ambaye yupo successful ile kiukweli kweli sio hao mapedeshee wezi wezi ambao hawajui principles za utajiri ndo maana wanafulia baada ya muda. Nilichogundua katika mtazamo wa kisaikolojia ni kwamba wengi wa wadada ambao wapo obsessed na wanaume wenye hela wanatoka kwenye familia za kimaskini with exceptions ya wachache. Katika interaction na baadhi ya ya watu tofauti wa hii jinsia ya kike nimekuja kugundua kwamba wale wenye uwezo au kazi nzuri huwa mara nyingi hawana nyodo za aina hiyo kasoro wachache. Ila wale wenye njaa ndo wenye nyodo na dharau..Anatamanai mwanaume mwenye gari sababu yeye hana gari na pia baba yake hakuwahi kumiliki gari au kama alimiliki basi ni gari mkweche mkweche. Kwenye saikolojia inaelezea kwamba watu mara nyingi hutamani kile ambacho hawana. Wanatamani fedha kwa kudhani wenye fedha wana raha sana. Wanatamani watoto kwa kudhani wenye watoto wana raha sana. Wanatamani wanaume wenye pesa kwa kudhani wenye hao wanaume wana raha sana. Wanatamani kazi ya benki kwa kudhani wanaofanya kazi benki wanakula sana bata sababiu ya uvaaji wao nadhifu teh teh teh. In short they are hallucinating of having a better life without working for it. Kuna msemo huwa wa kidhungu unasema "The grass inside a fence always looks greener especially when you are standing outside the fence". Najua wengi mtachukia na kunitukana kwa kusema haya. Ila jipu ndo lishapasuka pwaaa... Jiwe limerushwa gizanii atakayepanic basi ujue ndo limempata..