Watu kwenda kwa Waganga wanapoibiwa badala ya kwenda polisi imeshakuwa kawaida Uswahilini

James_patrick_

Senior Member
Mar 20, 2017
106
194
Habari ndugu zangu

Mimi naishi uswahilini huku sasa kitu nilichokigundua ni kwamba siku hizi kumeongezeka watu kwenda kwa waganga sana pindi wanapoibiwa kuliko kwenda police.

Utasikia tu mimi lazima nimuonyeshe aliyeniibia yaani nitamkomesha na asilimia kubwa uwa wanaenda kweli kwa waganga.

Cha ajabu hatuoni lolote kutokea kwa mtu anayehisiwa. Sasa sijajua kama waganga wenyewe nao nguvu hamna na pia kwanini watu wanapenda kukimbilia uko.

Mtu unamwambia kabisa nenda police watajua la kukusaidia lakini mtu anaona kwa mganga ndio njia sahihi zaidi. Wadau sijui tatizo liko wapi na mbona siku hizi atuoni tena mashipa wala mabusha waganga nao wamekuwaje
 
Kuwa innocence ukimaliza hakuna MTU wa kukuroga

Uchawi upo overrated lakini ni level ndogo in spiritually dimension

That huwa namdharau MTU anayetishia kuwaroga watu
 
Cha ajabu hatuoni lolote kutokea kwa mtu anayehisiwa. Sasa sijajua kama waganga wenyewe nao nguvu hamna na pia kwanini watu wanapenda kukimbilia uko.
Hujiulizi kwanini watu wenye matatizo ya akili wanaongezeka? Huenda wengine ni matokeo ya wizi wanaofanya.

Mi huwa siendi huko kwa waganga, ila kiukweli huwa nawaombea dua mbaya. Wapigwe hata upofu, wachanganyikiwe, wapate hata ulemavu wa viungo, yan wawe mataahira kabisaa. Wanarudisha nyuma sana maendeleo ya wenzao
 
Habari ndugu zangu

Mimi naishi uswahilini huku sasa kitu nilichokigundua ni kwamba siku hizi kumeongezeka watu kwenda kwa waganga sana pindi wanapoibiwa kuliko kwenda police.

Utasikia tu mimi lazima nimuonyeshe aliyeniibia yaani nitamkomesha na asilimia kubwa uwa wanaenda kweli kwa waganga.

Cha ajabu hatuoni lolote kutokea kwa mtu anayehisiwa. Sasa sijajua kama waganga wenyewe nao nguvu hamna na pia kwanini watu wanapenda kukimbilia uko.

Mtu unamwambia kabisa nenda police watajua la kukusaidia lakini mtu anaona kwa mganga ndio njia sahihi zaidi. Wadau sijui tatizo liko wapi na mbona siku hizi atuoni tena mashipa wala mabusha waganga nao wamekuwaje
Chanzo cha watu kwenda kwa Waganga wanapoibiwa ni Elimu Duni (ujinga uliotopea), Imani za Kishirikina na watu kupoteza kabisa Imani na Serikali, hususani Mamlaka zinazohusika na masuala ya Haki Jinai yaani Jeshi la Polisi.
 
Kuwa innocence ukimaliza hakuna MTU wa kukuroga

Uchawi upo overrated lakini ni level ndogo in spiritually dimension

That huwa namdharau MTU anayetishia kuwaroga watu
Kuna mwenzio alikuwa analeta notes za shule ambazo hata sisi tumepitia

Mtoto wake alipandisha shetani likawa linaongea Kingoni wakati Yeye ni wa Kanda ya Ziwa baada ya kurudi kutoka boarding school

Kitaalam na kisayansi hakunipa jibu chanzo ni nini?

alilegea akaletwa 'fundi' na Jirani mwema na muda wowote Fundi akifika analipandisha lile pepo na linazungumza na likishuka kichwani yule Binti hawezi hata kusalimia Kingoni

Hili suala lingemkuta mwingine tofauti na Yeye tungesomewa sana theory za kisayansi kuonesha yale ni mambo ya kufikirika na ya kipuuzi

Halafu kwa uzoefu wangu wa Mazingira yangu wale wengi wanaoigiza kutoyatambua haya Mambo huwa ni ma magwiji kweli kweli

Mambo ya kishirikina na kimazingara yapo kiuhalisia ila ni haramu na ni moja ya dhambi zisizo sameheka lakini kujifanya kuwa hayapo pia ni ama kutofahamu kwa undani au ni ukizabizabina
 
Kuna jamaa wa kigoma hua anafataga mzigo kkoo Kuna majamaa wakamuibia katoni mbili jamaa alisema hao walioiba watarudisha hela yangu...baada ya siku mbili wale wezi sijui walipatwa na nn ila walimtafuta jamaa wakamrudishia Hela yake
 
Kuna jamaa kamaliza kwamba UCHAWI NI OVERRATED
Sio over rated bali tuseme Uchoyo na ubinafsi wa Wachawi umeleta nafuu kwa Ulimwengu kwa kuwa Wengi wameondoka na Taaluma zao kama yule Mtaalam wa kutengeneza AK 47 aliesita kufundisha na kuendeleza taaluma ya kuhujumu Dunia na watu wake

Huenda miaka 100 ijayo Dunia ikawa salama zaid kwa kuwa 'Mafundi halisi' ndio wanaishia ishia tunabaki na wapiga mikwala feki
 
Kuna jamaa wa kigoma hua anafataga mzigo kkoo Kuna majamaa wakamuibia katoni mbili jamaa alisema hao walioiba watarudisha hela yangu...baada ya siku mbili wale wezi sijui walipatwa na nn ila walimtafuta jamaa wakamrudishia Hela yake
Duh

Ova
 
Back
Top Bottom