Watu hawajaelimika kumbe

howard

Senior Member
Feb 21, 2011
188
28
Mkazi mmoja wa Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Erest Khamis (45), anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kushiriki kumuua baba yake mzazi wakimtuhumu kuzuia mvua kunyesha mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zellothe Stephen, amesema tukio hilo limetokea jana saa 2 usiku wilayani humo ambapo mtuhumiwa huyo alimshambulia baba yake, Khamis Hussein (70), kwa kumpiga kwa madai kuwa ndiye aliyesababisha mvua isinyeshe katika mkoa huo.

Ameongeza kuwa zilikuweko taarifa za muda mrefu kuwa marehemu alikuwa akihusika katika uzuiaji wa mvua ambapo baadhi ya wanakijiji walimfuata mtoto wake huyo na kumuelezea kero hiyo. Kutokana na kitendo hicho, mtoto huyo aliamua kumpiga baba yake.

Polisi watamfikisha mahakamani mtuhumiwa baada ya taratibu kukamilika.

from: www.wavuti.com
 
Duh!Huyo father jap imeniuma yey kufarik ila imekaa vizur kwa nin alikuw anazuia mvua isinyesh??
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom