Watu 43 wanaodhaniwa kuwa ombaomba wakamatwa Zanzibar, RC Ayoub atoa msimamo mkali

Bedui la bongo

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
297
306
[http://img2]

Jumla Ya watu 43 wnaosadikiwa kuwa omba omba wamekamatwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi kati hao 13 wanatoka Tanzania Bara na wengine wanatoka katika Wilaya ya Magharibi “A”: na “B” Kisiwani Unguja.

Zoezi hilo limefanyika kufuatia kuenea kwa omba omba wengi katika viunga vya Mkoa wa Mjini Magharibi na baadhi yao kuonekana kukaidi kuachana na biashra hio ya omba omba kufuatia maagizo mbali mbali ya yaliyotolewa hapo awali na uongozi wa Mkoa huo .

Akizungumza na watu hao katika ukumbi wa sebleni kwa wazee Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amesema zoezi la kuwakusanya omba omba katika Mkoa wake limefanikiwa na kusisitiza shughuli hiyo ya omba omba haikubaliki katika maeneo hayo na endapo mtu yeyote antakaehusiaka anafanya shughuli hiyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
 
Hee kumbe ombaomba mi niliona video Jana walikamatwa Dada na Kaka Poa kibaao tu
 
Zanzibar bwanaaa kama Oman eti ukumbi wa sebleni kwani kuna ukumbi wa chumbani?
 
Kuna Kibanda Maiti, Mfereji Maringo , Mkamasini, Kijito upele, Bububu, Bumbwini, Makunduchi, Maharibiko, Jia la uzi, kiembe samaki, Mwana kwerekwe n.k
Jaani, Kidmni, Koani, Unguja Ukuu, Kichangamle, Kizimkazi, Dimbani, Fuoni, Tunguu, Jozani nk.
 
Chanzo cha hayo majina huwa ni kipi? Eti Kijito Upele, sijui mchamba wima, mfereji maringo dah.

Ha ha haaaa
 
Umemaliza kabisa. Hili sio swala la muungano. Warudi kwao. Dah! Uislam sasa ni wa kimkoa
Jeremy Bentham : Hata kama Mungu asingekuwepo, au awepo lakini akawa hana Muda na matendo ya binaadamu bado wangekuwepo watenda mema na watenda mabaya. Kwa maana nyingine watu hawatendi mema kwa ajili ya dini zao, bali ni kitu cha asili alichozaliwa nacho ama kimuongozacho kwenye akili yake. Hapa anapinga kauli kama hizi za mtu akitenda wema anaoanisha na dini yake mara umetenda uislam mara umetenda ukristo mbona wapagani saa nyingine wanatenda mema kuliko wenye dini?
 
Kutokunielewa ni kubaya sana. Mnyaazi Mungu Subhanah Taalla ametuagiza kuwatendea mema tena ya hisani wale wote waliopungukiwa. Sasa utawapata wapi kama hawajakuja karibu na weye?? Kule kuwafurusha maanake ni kuwa; Hutaki kubughudhiwa weye ulapo mema ulopewa na Mola. Huo sio uislamu
 
Usipunguze ukuu wa Mungu kwa kumpa kisifa kisichoeleweka kwa Lugha ya kiswahili

1. Ni Mwenyenzi Mungu .......wala si Mnyanzi Mungu..... Mwenyenzi ni muunganiko wa maneno mawili fasaha ya Kiswahili ..... Mwenye.....na ..... Enzi.... ndio likaunda sifa ya Mungu kuwa alikuwepo kabla ya enzi na yeye ndio mmiliki wa hizo enzi........ ''MWENYENZI MUNGU''
 
[http://img2]

Jumla Ya watu 43 wnaosadikiwa kuwa omba omba wamekamatwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi kati hao 13 wanatoka Tanzania Bara na wengine wanatoka katika Wilaya ya Magharibi “A”: na “B” Kisiwani Unguja.

Zoezi hilo limefanyika kufuatia kuenea kwa omba omba wengi katika viunga vya Mkoa wa Mjini Magharibi na baadhi yao kuonekana kukaidi kuachana na biashra hio ya omba omba kufuatia maagizo mbali mbali ya yaliyotolewa hapo awali na uongozi wa Mkoa huo .

Akizungumza na watu hao katika ukumbi wa sebleni kwa wazee Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amesema zoezi la kuwakusanya omba omba katika Mkoa wake limefanikiwa na kusisitiza shughuli hiyo ya omba omba haikubaliki katika maeneo hayo na endapo mtu yeyote antakaehusiaka anafanya shughuli hiyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Kwani kuwa omba omba ni kosa ki sheria......Omba Omba wapo tokea enzi za mitume na haijawahi kuwa kosa kisheria.
 
Jaani, Kidmni, Koani, Unguja Ukuu, Kichangamle, Kizimkazi, Dimbani, Fuoni, Tunguu, Jozani nk.
Mtu haliwa(mtu haliwi) mzuri hendi (mzuri haendi) mwembe mimba mwembe njugu kiinua miguu kilima nyege
 
Back
Top Bottom