Watu 42,000 wapona Korona nchini Iran

Watu 42,000 wapona Korona nchini Iran

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,601
Watu karibu 42,000 wapona corona nchini Iran

Huku idadi ya kesi mpya za ugonjwa wa Covid-19 (corona) ikiendelea kushuka kwa siku kadhaa sasa, kufikia leo mchana watu karibu 42,000 walikuwa wamesharuhusiwa kurudi nyumbani kutoka mahospitalini baada ya kupata nafuu kikamilifu.

Daktari Kianoush Jahanpour, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Umma na Upashaji Habari ya Wizara ya Afya ya Iran amesema leo Jumamosi kuwa, katika watu wote 70,029 walioambukizwa virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 kufikia sasa hapa nchini, 41,947 wamepona

Aidha amesema kuwa, watu wapatao 1,837 wameambukizwa virusi vya Corona katika masaa 24 yaliyopita, huku idadi ya waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo katika kipindi hicho ikiwa ni watu 125.

Kadhalika Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Umma na Upashaji Habari ya Wizara ya Afya ya Iran amesema wagonjwa 3,987 wa Covid-19 hapa nchini wapo katika hali mbaya.

Wataalamu wa Iran wazalisha vifaa vya kupima kiwango cha kinga dhiai ya vidudu maradhi katika mwili wa mwanadamu

Katika hatua nyingine, takwimu mpya za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins zinaonesha kuwa, zaidi ya watu 103,500 wameshafariki dunia kwa ugonjwa huo kote ulimwenguni.

Aidha watu milioni moja na laki saba wamethibitishwa kukumbwa na Corona kote duniani, huku wagonjwa karibu laki nne wa virusi hivyo wakipona.

4bv8622563dcfa1msjb_800C450.jpg
 
Sio kama China but afadhali sana coz wamechukua tahadhari, kutokana na maambukizi yalivyokua mengi na mpaka sasa jinsi walivyodhibiti wanastahili hongera, inawezekana shughuli ktk miji mingi zikarejea ispokua Tehran tu watasubiri kwanza kidogo
Ina maana wao ni kama China tu maana wanaelekea kumshinda Corona. Hongera kwao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom