Watu 30 wafa maji kagera... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watu 30 wafa maji kagera...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by RRONDO, Jun 20, 2010.

 1. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,882
  Likes Received: 20,944
  Trophy Points: 280
  Mwanzo » Habari
  Watu 30 wafa maji Kagera


  [​IMG] Wengine 18 waokolewa hai, wasimulia mkasa
  [​IMG] Yadaiwa mtumbwi ulibeba mzigo kupita kiasi  [​IMG]
  Usafirishaji wa watu katika Ziwa Victoria(Picha na maktaba)  Watu zaidi ya 30 wanahofiwa kufa maji baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Victoria.
  Mtumbwi huo unaosadikiwa kuwa na watu 50, ulizama wakati ukitokea kisiwa cha Kerebe wilayani Muleba kuelekea mji wa Bukoba mkoani Kagera.
  Ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa 6 mchana katika eneo la kisiwa cha Makibwa ambapo inadaiwa kuwa ilisababishwa na dhoruba kali.
  Baadhi ya abiria waliookolewa katika ajali hiyo walidai kuwa mtumbwi huo ulikuwa umebeba mzigo mkubwa kupita uwezo wake.
  Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera, Vitus Mlolele, amekiri kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa walikuwa hawajapata taarifa yoyote ya kifo isipokuwa taarifa waliyokuwa nayo ni kuwa waliookolewa ni watu 18 mpaka sasa.
  Alisema wakati wakiondoka Kerebe, abiria waliandikishwa ni 21 na kwamba taarifa hizo amezipata kutoka katika ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini (Sumatra) mkoani Kagera.
  Afisa Mfawidhi wa Sumatra, Kagera, Japhet Ole Semaye ambaye yuko eneo la tukio, alisema kuwa watu waliookolewa mpaka sasa ni 18 na hakuwa na taarifa ya idadi ya watu waliokufa ingawa amekiri kupotea kwa mtumbwi huo.
  Akisimulia ajali hiyo mmoja wa abiria aliyeokolewa katika ajali hiyo, Audax Cleophas (18), alisema mtumbwi huo uliokuwa umebeba zaidi ya watu 50 na kusheheni magunia zaidi ya 30 ya dagaa wakavu, ulikumbwa na dhoruba kali na hivyo kujaa maji hali iliyosababisha abiria waliokuwemo kutaharuki na kuanza kudondoka majini ovyo.
  "Baada ya abiria hao kutumbukia majini, mimi nilikuwa na pacha wangu, Aufasi Cleophace (18) ambaye alijishikiza kwenye dumu dogo la mafuta huku akiwa na wenzake wanne, hawakufika mbali nilishangaa kuona wanaanza kuzama mmoja mmoja na ndugu yangu akazama huku akiniambia mie nitoke katika gunia nilililokuwa nimeshikilia, nishikilie dumu la mafuta ambalo lilikuwa limeshikiliwa na watu zaidi ya 14,” alisema.
  Aliongeza wakati wakishikilia dumu hilo walikuwa wakisukumwa na upepo mkali hali iliyosababisha baadhi ya watu kuishiwa nguvu na kuanguka mmoja baada ya mwingine. “Tulibaki wanne tu kwenye dumu hilo jamani watu wamekufa wengi akiwemo pacha wangu maiti zinaelea juu ya maji tunaomba serikali ifike huko kwenye tukio na kuopoa maiti hizo."
  Alisema kuwa walikwenda umbali mrefu bila kupata msaada na wakati huo waliweza kumuona mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 6 ambaye alikuwa amevaa jaketi la uokoaji akielea juu ya maji ndipo walipombemba na kumuweka juu ya dumu hilo na ilipofika muda wa saa moja jioni waliona boti ya Sumatra ikienda kuwaokoa.
  Aliongeza kuwa watu wote waliookolewa ni wale waliovaa majaketi na kwamba wasiwasi wake ni kuwa waliokuwa hawajavaa majaketi watakuwa wamezama na kufa maji.
  Baadhi ya abiria walionusurika kifo na kutambulika kwa jina moja ni Anitha, Alistides, Danieli, Jakson, Ramadhan na Shafii ambao walidai wenzao wamekufa na maiti zinaelea juu.
  Mmiliki wa mtumbwi huo uliojulikana kama Titanic, Hidaya Adamu (35), alisema kuwa mtumbwi wake ulikuwa na uwezo wa kubeba abiria 25 tu. Alisema kuwa yeye hakujua idadi kamili ya watu waliokuwemo kwa sababu kati ya wale waliookolewa hakuna mfanyakazi wake hata mmoja aliyekwisha patikana.
  Hali ya majonzi kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba na vitongoji vyake, imetawala wakati Rais Jakaya Kikwete, alitarajiwa kuwasili jana saa 11 jioni kwa mwaliko wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi kwa sherehe za kusherehekea jubilei ya miaka 100, sherehe zinazotarajiwa kufanyika leo mjini hapa.
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. M

  Malunde JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Poleni Kagera.

  Ajali Tanzania ni nyingi, usafiri wa nchi kavu ajali ni nyingi sana, usfiri wa anga no mashaka, kwenye maji nako ajali zinakuwapo mara kwa mara. Mamlaka za usafiri zinachukua hatua gani kuwahakikishai watz usalama katika safari??? mbona majirani zetu kama Rwanda hawana ajali nyingi kiasi hicho???
   
 3. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,882
  Likes Received: 20,944
  Trophy Points: 280
  mbaya zaidi imekuwa kitu cha kawaida,watu hata hawashtuki wakisikia watu wamekufa ajalini.............
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Jun 21, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mungu apumzishe roho zao kwa amani. Matatizo ya namna hii ndiyo tunayohitaji kushughulikia kuhakikisha kuwa vifo vinavyoepukika kama hivi tunaviondoa. Viongozi wetu wamelala na kuota misaada tu.
   
 5. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2010
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Poleni sana watu wa Kagera...... Muwe na subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.....
   
Loading...