Watu 20 wafariki baada ya basi kuanguka Uturuki

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
turkey.jpg


Takriban watu 20 wamefariki papo hapo baada ya basi moja la watalii kuanguka kutoka juu ya mwamba karibu na eneo la kujivinjari lililopo Kusini mwa Uturuki.

Watu wengine 11 walijeruhiwa wakati dereva alivyopoteza mwelekeo wa basi hilo dogo na kugonga kizuizi.

Vyombo vya habari nchini vimesema kuwa hakuna watalii wa kigeni waliokuwemo katika basi hilo.

Takriban watu 400 walikuwa wameabiri basi hilo kulingana na gavana wa mkoa wa Mugla, Amric Cicek ambaye anasema huenda breki zilifeli.

Lakini Meya wa eneo la Marmaris ,Ali Acar aliambia gazeti la Uturuki la Hurriyet nadhani ajali hiyo ilisababishwa na makosa ya dereva.

Vyombo vyengine vya habari vinasema kuwa waathiriwa wengi walikuwa wanawake na watoto.


Chanzo: BBC Swahili
 
Back
Top Bottom