Watu 17 washikiliwa kwa kutaka kuandaa maandamano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watu 17 washikiliwa kwa kutaka kuandaa maandamano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Nov 6, 2010.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,903
  Trophy Points: 280
  Watu 17 washikiliwa kwa kutaka kuandaa maandamano 05/11/2010

  Watu 17 wakiwemo Diwani mteule wa kata ya Mtibwa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tusekile Mwakyoma na Mwenyekiti wa Wilaya chama hicho, Charles Mbaga wanashikiliwa na polisi katika kituo kidogo cha Turiani, wilayani hapa kwa madai ya kutaka kuandaa maandamano ya kupinga matokea ya uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili, Oktoba 31, 2010.

  Viongozi hao pamoja na wafuasi wengine wa chama hicho walipinga mgombea wa ubunge kupitia CCM Amos Makala kutangazwa mshindi wa jimbo la Mvomero mkoani Morogoro. Walidai kuwa ushindi wa Makala hakuwa halali kutokana na kusisitiza kuwa kumekuwepo na wizi wa kura wakati wa zoezi zima la uchaguzi.

  Rehema Oden (67) ambaye ni mama mzazi wa Diwani mteule huyo alimwambia mwandishi wa habari hizi, Juma Mtanda, kuwa polisi walifika nyumbani kwake majira ya saa tisa alasili ya Novemba 3 na kuanza kuwapiga na kuwakamata watu hao. Alisema katika kamata kamata hiyo ilimhusisha pia mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Mvomero, Charles Mbaga, mtoto wa diwani huyo na mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari ya Nasoro Seif , Evarenci Julius (16) ambaye hata hivyo aliachiwa baadaye.

  Baada ya kukamatwa kwa viongozi hao sakata hilo liliendelea kwa jeshi la polisi kukamata watu wengine sehemu mbalimbali ambao wanadaiwa kuwa ni wananchama wa CHADEMA ambao walihusishwa na tuhuma za kutaka kufanya vurugu ikiwemo kufanya maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo.

  Naye mmoja wa wanachama wa chama chicho, White Awadhi mkazi wa kijiji cha Kidundwe ambaye anadai kusakwa polisi alisema kuwa yeye tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu alikuwa muhamasishaji hali iliyosababisha wanachama wengi wa CCM kuhama na kuanza kuiunga mkono CHADEMA. Alidai kuwa kitendo hicho huenda ndicho kilicho sababisha polisi kumsaka sambamba na kuandaa mipango ya kufanya maandamano ya amani kupinga kutangazwa kwa Makala kuwa ndiye mbunge mteule wa jimbo hilo.

  “Mgombea ubunge wa CHADEMA alipata taarifa za kuwa wananchama na wananchi wanataka kuandamana lakini akiwa jijini Dar es Salaam alipiga simu ya kuzuia tusiandamane na sisi tulifuata maelekezo yake lakini cha kushangaza majira ya saa tisa alasiri mji wa Mtibwa tulivamiwa na askari wa kutuliza ghasia na kuwakamata Diwani na Mwenyekiti wa chama chetu,”alisema Awadhi.

  Alisema sababu za kutaka kuandamana kwa wananchama hao pamoja na wapenzi ni kunatokana na mgombe ubunge jimbo hilo kupitia CHADEMA, Matokeo Manyata kugundua kasoro nyingi zilizojitokeza katika karatasi za kupigia kura ikiwemo karatasi bandia.

  “Mgombea wetu wa CHADEMA Matokeo Manyata kwanza amekamata karatasi bandia za kupigia kura na kasoro nyingine iliyojitokeza katika karatasi zile ni kuwepo kwa wino sehemu ambayo mgombea wetu aliwekewa alama ya ndiyo na kuweka wino kwa lengo la kuvuta,” alisema Awadhi.

  Naye Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro, Ahmed Msangi akithibitisha kukamatwa kwa watu hao alisema polisi haikumata wanachama wa CHADEMA isipokuwa wamekata wahuni.

  “Kama unasema tumekamata wanachama wa CHADEMA, lete majina yao na namba za kadi zao sikiliza polisi wamekamata wahuni na si wananchama wa CHADEMA kwani wananchama wa CHADEMA wapo makini” alisema Msangi.

  credit : Juma Mtanda blog


  from: Watu 17 washikiliwa kwa kutaka kuandaa maandamano -
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Nov 6, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  wanajaribu kuzuia nguvu ya umma, hawawezi!!
   
 3. F

  Fishyfish JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Characteristics of a dictatorship.
   
 4. m

  mpitaji Member

  #4
  Nov 6, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hapo haki iko wapi jamani? tutafika wapi na serikali hii inayoigiza uongozi? kikwete na wenzake naweza kuwafananisha na original comedy maana wanaigiza wala si kuongoza. maandamano ni haki ya msingi kikatiba ya kudai haki pale inapoonekana haki haikutendeka.
   
 5. Gwaje

  Gwaje JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 271
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 45
  Kwanini haya yanatokea? Polisi wenyewe wanaishi kwama mbwa, angalia nyumba zao hapo morogoro, osterbay na kwingineko kunatisha lakini hawaoni huruma hata kwao wenyewe.
  Poleni kwa hawa jamaa tupe maendeleo yao, wamepelekwa mahakamani? Kwa makosa yapi?
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hivi kuna tofauti yoyte kati ya :
  CCM
  POLISI
  SERIKALI?
  Mi nijuavyo ishu kama hiyo haizimwi kwa ku'supress maandamano, lakini pia kutafuta ukweli wa hoja (root-causes)za waandamanaji hao kuingia mtaani!
   
 7. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mi naona tuanzishe thread maalumu ya kuwachambua polisi.Tuchambue maisha yao kwa ujumla na jinsi wanavyotumiwa kama mbwa.Labda itasaidia kuwafanya wajione kweli kama mbwa na watataka hadhi ya utu kwa kukataa kutumiwa ovyo.
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Yes this is TYRANNY
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ivi polisi wanavyoamaua kumpiga mtu si sawa na kumhukumu kuwa ni mhalifu
  Nijuavyo unaweza tumia kipigo kwa mtu amabae anakaidi.
  Polisi vihiyo bwana wanakazi ya ziada kujua HAKI ZA RAIA
   
 10. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2010
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,322
  Trophy Points: 280
  Hivi bado wapo ndani ama wameshaachiwa?????
   
 11. BABU KIDUDE

  BABU KIDUDE JF-Expert Member

  #11
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,371
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Da leo wapenda haki wnaitwa waouni? Nchi inakwenda wapi jamani??
   
Loading...