Watu 150 wauawa na Boko Haram Nigeria

Watu 150 wauawa na Boko Haram Nigeria

kazikwanza1981

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
1,577
Reaction score
729
Watu 150 wameuawa baada ya Boko Haram kuvamia kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Walioshuhudia mashambulizi hayo wanasema watu tisini na saba wameuawa siku ya Jumatano katika kijiji cha Kukawa kilichopo karibu na Ziwa Chad.

Habari zinasema pia wanaume 48 wamepigwa risasi na wapiganaji katika mashambulizi tofauti siku ya Jumanne.

Mashuhuda wanaokimbia eneo lililopo karibu na Ziwa Chad wanasema idadi kubwa ya wapiganaji wamevamia vijiji vitatu ambapo wameuwa wanaume, wanawake na watoto.

Baadhi ya ripoti zinasema walipigwa risasi huku wengine wakielezea jinsi wapiganaji hao walivyowachinja watu na kuchoma majengo.
Upande wa Kusini, nje kidogo na mji wa Monguno, kundi la wapiganaji wa Boko Haram wamefika usiku wakati watu walipokuwa wanaswali.

Waliwasubiri mpaka walipomaliza kuswali na kuwatenganisha wanaume na wanawake na baadae kuanza kuwamiminia risasi wanaume.
Mwanasiasa anayewakilisha eneo hilo, Mohammed Tahir amesema awali alitoa tahadhari kwa jeshi la Nigeria kwamba vijiji hivyo viko hatarini kwa sababu Boko Haram wameweka makazi katika maeneo hayo baada ya kutimuliwa katika himaya yao ya msitu wa Sambisa.
Haya ni mashambulizi mabaya zaidi kufanywa na Boko Haram katika kipindi cha wiki kadhaa.

Kundi hilo limekuwa likilipuwa mabomu kadhaa baada ya kudhoofishwa na majeshi ya Nigeria.
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amesema kipaumbele chake ni kuimarisha mapambano dhidi ya Boko Haram.



Chanzo: BBC Swahili
 
Inasikitisha sana, lakini swali langu ni hivi kweli Nigeria na washirika wake kama Tchad na Niger wamewashindwa hawa wanamgambo?
Kwanini nguvu nyingi hazielekezwi huko toka kwa mataifa makubwa ya magharibi?
 
Kuna kitu hapa. Hivi kwanini limekuwa kama limefumbiwa macho?
Watu wengi sana hawa at pa na hakuna hatua zozote yaani...
 
Kuna kitu hapa. Hivi kwanini limekuwa kama limefumbiwa macho?
Watu wengi sana hawa at pa na hakuna hatua zozote yaani...

Hawa Boko Haram kuna support wanayoipata toka kwa mataifa makubwa sana duniani ndio maana husikii chochote kimefanyika kunusuru hali hiyo mkuu
 
Huwa nina hisi kuwa kuna aina flani flani za propaganda ndani ya habari za hawa jamaa wa BOKO haram .
 
Last edited by a moderator:
Huwa nina hisi kuwa kuna aina flani flani za propaganda ndani ya habari za hawa jamaa wa BOKO haram .

Habari ndo hiyo, hizi ni drama japokuwa wapo wanaokufa bila hatia. Hiyo damu itamwaga damu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom