Watoto wote wana haki ya kulindwa

Watoto wote wana haki ya kulindwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Kila mtoto ana haki ya kuishi, kuwa salama, kuwa na wazazi/walezi, kusikilizwa, kupata huduma muhimu na kukuwa katika mazingira salama.

Familia ndicho chanzo cha ulinzi wa mtoto. Wazazi au walezi wengine wana jukumu la msingi la kutengeneza mazingira ya nyumbani ambayo ni salama na yenye upendo. Shule na jamii ina jukumu la kutengeneza mazingira ya nje ya nyumbani ambayo ni salama na rafiki kwa mtoto.

Kwa bahati mbaya mamilioni ya watoto hawana ulinzi. Kila siku watoto wengi wanakabiliwa na ukatili, unyanyasaji, utelekezwaji, unyonyaji, utengwaji na/au ubaguzi. Aina hizi za ukiukwaji wa haki za watoto hupunguza uwezekano wao wa kuishi, kukua vizuri na kufikia ndoto zao.

Zaidi ya watoto milioni 160 hutumikishwa badala ya kufurahia utoto wao

Inakadiriwa kwamba zaidi ya watoto milioni 160 wa umri wa miaka 5–14 wanatumikishwa katika ajira za watoto. Mamilioni ya watoto, hususan wasichana wanafanya kazi za nyumbani kwa watu binafsi na zaidi ya watoto milioni moja husafirishwa kila mwaka.
 
Uko sahihi sana. Ila si watoto peke yao. Kila binadamu ana haki ya kujilinda N kulindwa.

Kulindana ndio mpango mzima
 
Ngoja tuwalinde ole wao wengine wapate mimba warudi na shule sasa.
 
Back
Top Bottom