Watoto wasilee watoto, wapewe fursa ya kuuishi utoto wao raha mustarehe

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,619
46,259
Watanzania tuzae watoto tunaoweza kuwalea au atafutwe mtu wa kuwalea kwa malipo kama huna muda wa kulea mtoto uliyemzaa, sio sahihi kutumia watoto wengine uliowazaa kama walezi wa watoto wengine unaondelea kuwazaa.

Mara kadhaa katika mizunguko sehemu nyingi hapa nchini nimekutana na watoto wa kuanzia miaka 6 na kuendelea wakiwa wamebebeshwa watoto mgongoni au wanaadhibiwa kwa kushindwa kuwalea watoto wenzao vizuri.

Hali hii ni mjini na vijijini. Hii sio sawa na ni uonevu mkubwa sana kuwatumikisha watoto katika malezi. Watoto wanapaswa kujifunza shuleni, kucheza na kushiriki katika sanaa kuendeleza akili zao na vipaji ili tupate raia bora wenye tija kubwa huko mbeleni, hawapaswi kuwa walezi wakiwa bado watoto.

Watu wazae kwa mpango wakiwa na mpango madhubuti wa malezi walioundaa.

Huo ndio ustaarabu.
 
Well umenena vyema aisee, watoto kuna vitu inabidi wavizoee mapema kwa ajili ya kukua vizuri
 
Back
Top Bottom