Watoto waliookolewa wasahau majina yao

Watoto waliookolewa wasahau majina yao

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,086
Reaction score
34,883
150214140931_cameroon_troops_army_military_boko_haram_640x360_afp_nocredit.jpg

Jeshi la Cameroon likiwasaka wapiganaji wa Boko Haram,

Takriban watoto 80 waliookolewa katika kambi ya kundi la Boko Haram nchini Cameroon hawawezi kukumbuka majina yao kulingana na afisa mmoja aliyewatembelea.


Watoto hao wenye umri wa miaka 5 hadi 18 hawakuzungumza kiingereza,kifaransa ama lugha nyengine yeyote ile kulingana na Christopher Fomunyoh,ambaye ni mkurugenzi wa kitaifa wa taasisi ya National Democratic Institute {NDI}.

Watoto hao walipatikana katika kambi kazkazini mwa Cameroon mnamo mwezi Novemba.

Kundi la Boko Haram kutoka Nigeria limepanua mashambulizi yake hadi nchini Cameroon.

Wapiganaji hao wanajaribu kusimamisha taifa lenye uongozi wa kiislamu kazkazini mashariki mwa Nigeria.
Wanadhibiti miji kadhaa na vijiji katika jimbo hilo na hivi majuzi waliahidi kuiga mfano wa kundi la Islamic State ambalo limeteka eneo kubwa la Syria na Iraq. chanzo.
www.bbc.co.uk
 
Hakuna taifa la kidini duniani bali dini zote tunategemea makao mapya mbinguni.hawa boka horamu ni majambazi tu.
 
Back
Top Bottom