Watoto waende Shule hata bila Sare-Serikali!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Sasa ni kweli kwamba tumejitambua na tumeweza kuelewa ni kipi Kipaumbele nchini mwetu ni jambo la ajabu sana na dhambi kubwa kubwa kwa Mungu huko nyuma mtoto alikuwa ananyimwa Elimu kwa kukosa sare za shule tu, sasa Serikali imesema kwamba kitendo cha mtoto kukosa sare kisimfanye akose Elimu kwani siyo kosa lake!
Hongereni Sana Serikali yetu kwa kulitambua hilo, hata kama mtoto amevaa majani lkn lazima asome kwani ndiyo muhimu!

Habari kamili hiyo hapo chini!

,,MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Magalulla Said Magalulla amewataka wazazi na walezi mkoani humo kuhakikisha watoto wao wenye sifa za kuanza masomo wanakwenda shule mara tu zitakapofunguliwa hata kama hawana sare.

Magalulla alisema kuwa hakuna visingizio tena vya watoto kushindwa kuhudhuria masomo kwa madai wazazi hawana uwezo kwa sababu tayari Rais John Magufuli ametangaza elimu bure kuanzia elimu ya awali hadi sekondari.

“Mahitaji mengine mtoto atayapata akiwa tayari shuleni lakini sio mzazi au mlezi asubiri mpaka amtimizie mahitaji yote. Wazazi kwanza wapelekeni watoto wote waliofaulu kuanza kidato cha kwanza pia walioandikishwa kuanza darasa la kwanza,” alisema. “Hata kama hana sare ya shule mvishe nguo zake za nyumbani aende shule (na kumtafutia taratibu). Sio haki hata kidogo kumkataza au kumzuia mtoto kwenda shule kwa sababu tu hana sare kwani hilo sio kosa la mtoto,” alisisitiza Magalulla.

Aliwakumbusha wazazi na walezi kutambua kuwa kazi ya mtoto ni kusoma tu ambapo mzazi kazi yake ya msingi ni kumpelekea mtoto wake shule na kuhakikisha anahudhuria masomo na kumpa mahitaji mengine ya lazima.

Mkuu huyo wa mkoa pia amewaagiza maofisa elimu kuhakikisha watoto wanapokewa shuleni na kama kuna masharti hayajatimizwa basi wabaki wakiwadai wazazi kuyatimiza huku watoto wakiwa tayari wanaendelea na masomo.

“Pia ni wajibu wa wazazi na walezi ambao watoto wao wako shuleni wanasoma kushirikiana na walimu wao kuhakikisha kuwa kweli wanakwenda shuleni, maana baadhi ya watoto wanavaa sare lakini hawafiki shuleni, tuhakikishe watoto wana kwenda shule,” alisema.

Magalulla alisema ni kosa la kisheria kwa mzazi au mlezi kusababisha mtoto asiende shule au kumshawishi kukatiza masomo ili aweze kujihusisha na ajira.

Alionya kuwa mtu huyo akikamatwa atashtakiwa kwa sababu sheria inataka mtoto akianza shule lazima amalize. Kwa mujibu wa matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mkoa wa Rukwa mwaka jana, mkoa huo umefanya vibaya kwa kushika nafasi ya tatu kitaifa kutoka mwisho.

Halmashauri ya wilaya ya Kalambo ilishika nafasi ya 165 kati ya halmashauri 166 nchini"
 
Je, wanaruhusiwa pia kuvaa kanzu na hijab?
 
bila viatu? nimegundua kwanini jamiii flani huchukiwa sana humu jf ni gap la kimaendeleo
 
Back
Top Bottom