Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,059
- 79,406
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
1. Watu waache dhulma. Watu waache utapeli. Watu waache kula jasho la watu wengine.
2. Asilimia kubwa ya wanaume huoa/kuishi na wanawake wakiwa bado hawajajipata. Yaani vijana wengi almost chini ya miaka 35 maisha yao bado yanakuwa yakuunga unga.
3. Wanapata Wanawake katika umri huohuo wakiwa apeche Alolo. Wanaishi kama Wenza, Mke na mume, wanajenga nyumba na familia yao.
4. Yawezakuwa mwanamke kipato chake kikawa kidogo kuliko mwanaume au hata asiwe na kipato kabisa ila ule uwepo wake tuu ni mchango tosha kwa mwanaume.
5. Wanachuma mali kwa pamoja kwa miaka labda kumi na tano.
6. Watoto wanazaliwa hapo. Baadhi ya miradi na kazi za uzalishaji watoto wanafanya. Kama kwenda shamba, kuchunga mifugo, kuuza duka, kutengeneza bidhaa, kuuza bidhaa n.k. watoto wa ndani ya ndoa wanafanya kazi hizo.
7. Baadaye Mungu amejalia, angalau maisha yanaonekana. Nyumba na vijimali vipo. Mwanaume ikatokea amezalisha mwanamke mwingine huko.
8. Yule mtoto hawezi kuwa Sawa na hawa watoto wa ndani ya ndoa. Yaani hata kimahesabu ya kawaida haiwezekaniki kuwa sawa. Hakunaga haki ya hivyo.
9. Hata ndani ya ndoa tuu watoto sio Sawa. Kuna maeneo kamwe hawatalingana.
10. Mfano. Mtoto mkubwa yaani wakwanza kuna wakati alibeba majukumu ya Mzazi kuwalea ndugu zake.
11. Kuwabeba, kuwaangalia wakati mama na Baba hawapo, kuwaogesha, kuwalinda ndugu zake, na majukumu mengine. Ndio maana zamani mtoto wa kwanza hupewa nafasi ya Mzazi pale wazazi hawapo. Kutokana na majukumu yake. Na yeye ndiye huwa mrithi kwa jamii nyingi.
12. Watoto wa ndani ya ndoa na nje ya ndoa wanachofanana ni suala la DNA zao zote ni za Baba mmoja.
13. Lakini kiuchumi hawawezi kufanana.
14. Kwenye haki, Wale waliozalisha au waliochangia uchumi wanahaki kupata zaidi kuliko wale ambao hawakuchangia Sana.
15. Mwanamke ambaye umekaa naye muda mrefu tangu ukiwa down ukiwa huna maisha, mkapigana tough mpaka ukafika hapo ulipo watoto wake wanahaki ya kupata zaidi kuliko watoto wa wanawake wengine.
16. Vinginevyo hakuna faida ya mwanamke kuolewa na mwanaume fukara, maskini, ambaye Hana maisha,
Kama mambo yenyewe mwishoni yanakuwa yanaenda kama hivyo.
17. Sisi Watibeli tunazingatia Sana suala la Haki, ukweli, upendo na Akili.
18. Yaani mwanaume wa Kitibeli aoe akiwa maskini, kisha akishatajirika amfananishe mkewe na watoto wa mkewe Sawa na wanawake wengine na watoto wa wanawake wengine hao sio watibeli.
19. Kijana usimsahau mke wa ujana wako. Kumaanisha mke ambaye alikustahi ukiwa bado Mdogo kwa Kila kitu, Mdogo kiuchumi, kiuzoefu wa maisha, karibu Kila kitu.
20. Na unapoambiwa usimsahau mke ea ujana wako wanamaanisha hata Watoto wake.
21. Nabii Ibrahim kama Watibeli wengine alifanya hivyo. Alijua wapi alipotoka na Sarah Mkewe, Alijua mchango wa Sarah katika utajiri wake. Hata Kama Sarah alikuwa hana kazi ya uzalishaji lakini uwepo wake kama mwanamke anayempenda ulitosha kuwa nguzo ya utajiri wa Ibrahim.
22. Ndio Maana Ibrahim hakusita kumfukuza Hajiri na Ishmael kwa ajilli ya Sarah mkewe na Isaka mwanaye.
23. Ni kweli mtoto hachagui azaliweje. Lakini ni Jambo la asili mtoto kubeba matokeo iwe hasi au chanya ya wazazi wake hasahasa Mama.
24. Desturi hii pia itafanya wanawake kufikiri mara mbilimbili kuzaa na wanaume waliooa(waume za watu) lakini pia kuzaa kabla hawajaolewa kwa kujua matokeo kuhusu watoto kupata shida.
25. Watibeli mfumo wetu ni uleule. Mtoto hurithi kwa Mamaake ikiwa ataishi upande wa mamaake. Na mtoto atarithi kwa Babaake ikiwa ataishi na Babaake.
26. Isipokuwa kama kuna Makubaliano kati ya mwanaume na mwanamke. Kwamba mwanaume akubali kwa hiyari yake, mbele za mashahidi na maandishi kwamba mtoto Fulani kwa jina Fulani aishi na Mamaake Kwa ruhusa ya Baba na atapata haki zote kwa mwanaume.
27. Mtoto anaweza kuishi kwa Mama lakini Baba yake akaamua kumrithisha Mali kwa hiyari ya Baba.
Kwani ni kweli watoto wa ndoa pia wanaweza wasiwe watoto wa mwanaume na watoto wa nje wakawa wa mwanaume.
28. Siku hizi wanawake nao wanatafuta Mali hivyo Sheria za Kitibeli zipo mbele ya muda.
29. Sheria hizi za haki ni Sheria za watu wenye Akili, wenye Utu, wapenda Haki. Na wenye Upendo.
30. Halikadhalika Mtoto ambaye amelelewa na Baba hatakiwi kurithi Mali za mama yake ambaye hakumlea. Isipokuwa kwa hiyari ya Mamaake.
31. Kwa Sisi watibeli, Urithi upo kwaajili ya kuendelezwa sio kutumiwa uishe. Ndio maana watoto uliowalea wewe mwenyewe ndio wanatakiwa Warithi Mali zako. Kwa sababu maadili uliowafundisha utawafundisha kutokana na future unayoiona wewe Kama Baba.
32. Mtoto ambaye hujamlea hana uwezo wa kuendeleza urithi wako kwa sababu Hana mafundisho yako, hajui ulikuwa unataka nini practical, hajui ulikuwa unafanyaje kazi zako, hajawahi kukuona ukifanya kazi za uzalishaji.
33. Mrithi anatakiwa kuwa karibu Yako. Akuone, akuige, ajifunze, awe wewe katika version mpya.
34. Waarabu na jamii za mashariki ya Kati, wahindi wanajua haya. Ndio maana hakuna jamii inayoweza jamii za mashariki ya Kati kwenye suala la mambo ya familia na urithi.
35. Sheria hizi hazilengi kumpendelea mtu. Zinalenga ustawi na haki.
Kufikia hapo sina la ziada.
Ijumaa Kareem
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam