Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Mwarabu mmoja(sayeed) kabla ya kufariki aliwaachia wosia wanawe watatu arkhad,khalfan na nadir kuhusu kugawana ngamia wake.alisema arkhad(first born) apate 1/2 ya ngamia wote,khalfan(second born apate 1/3 ya ngamia wote na nadir(last born) apate 1/9 ya ngamia wote.Baada ya kufariki,mzee sayeed aliacha ngamia 17..Watoto walijaribu kila jinsi kugawana lakini ikashindikana.Mzee jabir alipokuwa akipita na ngamia wake akiwa safarini,aliukuta mkanganyiko huo.Mzee jabir alitumia busara zake na kuwagawa vizuri kabisa wale ngamia 17 kwa watoto watatu na kwa ratio ile ile.Tuelezane,alifanyaje?(hint;makadirio ya desimali hayaruhusiwi!)