Da Pretty Huyu Marehemu Mkama Sharp hakufika Upanga ila kwa wale waliokuwa wanaenda Viwanjani haswa Taifa na Karume ndio waliofanikiwa kumfahamu kwani alikuwa ni kama Kituko tu Bastola Kiunoni Mfupi anavaa miwani ya macho yenye lens nzito akizuia watu wasiluke Ukuta kuingia viwanjani so aliuwa ni kama chale chale tu sijui walikuwa wanamuogopea nini Sijui ...Huyo Mkama sharp alifika Upanga? Miaka gani hiyo?
R.IP Mwalimu Mahundi Wjua watoto wa Upanga tukikaa mitaani tuanhadithiana kila kitu cha shule na kusifiana sie tuna uwanja mzuri au nyie haman hichi au kile basi ndio hivyo tena au Tuition pia...Duduwasha ulienda kufanya nini pale CHUMBA CHA KINANDA?
Wakati tupo std 5 nilisomea lile darasa,mwaka uliofatia ndio kikawa chumba cha kinanda.
Mama Mahundi mi nilimkuta UPS tangu std 1 hadi natoka,badae akahamia Muhimbili ndiko alikomalizia kazi hadi alipofariki.
Temeke kulikuwa na Mwarabu anaitwa Hassan Ilibidi apewe jinala Chizi Muhimbili so Hassan Chizi na Kulikuwa na Mbabe Sana Bonge la Jeba kubwa sana Liliitwa Bukaba. na Kulikuwa na kamsopi, Olympio kulikuwa na Mwarabu aliitwa Hashim Mafishi alizidisha uhuni hadi akatumia Drug akaishia kuwa Teja.Majanga yalikuwa kote lakini waliokuwa wanawafundisha ni wa kariakoo. Tatizo la wakariakoo walikuwa wanakuja upanga na kwa kazi ya Kuiba tu utadhania zile movi za ma cowboy so mmoja akishawaona tu watu tunaandaa matawi ya mipapai akibakia mmoja basi fimbo za mipapai zinamuishia mwilini. Pale Don Bosco Father akianzisha mashindano timu za kariakoo tukiwafunga wanaanzisha fujo kha! kuna siku hadi refa mmoja ambaye ni wa kariakoo kwa sasa ni Shehe pia walimchapa.ati ameshindwa kuwabeba.Hizi naona ni personal attacks zaidi ambazo zitaharibu hii mada, naona unawamaidi kinoma watoto wa k'koo, japokuwa baadhi walikuwa hivyo lakini si wote, mbona hukutaja watoto wa temeke?
Mpira nilimaanisha timu zetu tukicheza nao... Wao walikuwa wanazichezea timu zao za mitaani kama Dar fire, Manyema n.k na Pale Uwanja wa Vijana walicheza sana waarabu na Zanaki Wahindi Kila Jioni Wahindi walikuwa wanacheza vizuri sana Mpira. Pia Mnazi Mmoja kulikuwa na timu ya ajabu na mkali wao alikuwa anaitwa Dalla...Hii ni kweli kabisa na inathibitisha kuona K'koo ilikuwa na timu za Simba, Yanga na Nyota Nyekundu (Timu kubwa za ligi kuu ya mpira bara). Enzi hizo kama wewe ni Simba ni marufuku kuvaa njano, watu hata walikuwa hawajui ligi za Ulaya zikoje. Ijumaa (shuleni) kabla ya mechi za jumamosi watoto wa k'koo husimama ubaoni kushindana kuandika list ya wachezaji watakaocheza kesho yake, taifa.
A.Ngdk kaolewa juzijuzi.R.IP Mwalimu Mahundi Wjua watoto wa Upanga tukikaa mitaani tuanhadithiana kila kitu cha shule na kusifiana sie tuna uwanja mzuri au nyie haman hichi au kile basi ndio hivyo tena au Tuition pia...
wewe utakuwa ulisoma kipindi cha kina Pau Kubwa au A. Ngdk Msichana alikuwa Mbabe yule du..
Mpira nilimaanisha timu zetu tukicheza nao... Wao walikuwa wanazichezea timu zao za mitaani kama Dar fire, Manyema n.k na Pale Uwanja wa Vijana walicheza sana waarabu na Zanaki Wahindi Kila Jioni Wahindi walikuwa wanacheza vizuri sana Mpira. Pia Mnazi Mmoja kulikuwa na timu ya ajabu na mkali wao alikuwa anaitwa Dalla...
Kijuso hadi leo anacheza dah!
Ilala... toto na Ilala... mama napika ubwabwa... Ilala
Kumbe watoto wa kariakoo jf hamtoshi,tatizo nini?access ya mtandao au?tukiweka watoto wa arusha hapa watafunika mbaya kama kwenye ule uzi wa makalio bar kwa mnaokumbuka si mliona wenyewe watoto wa ki R CHUGA walivyofunguka,kariakoo doro!kwaherini
R.IP Mwalimu Mahundi Wjua watoto wa Upanga tukikaa mitaani tuanhadithiana kila kitu cha shule na kusifiana sie tuna uwanja mzuri au nyie haman hichi au kile basi ndio hivyo tena au Tuition pia...
wewe utakuwa ulisoma kipindi cha kina Pau Kubwa au A. Ngdk Msichana alikuwa Mbabe yule du..
Kulikuwa na Mwizi Maarufu alikuwa anaitwa Ali Gulu.. Cha kushangaza alikuwa ana mguu mbovu anachechemea lakini ni mwizi tena yule wa kukaba na anaondoka pole pole hakimbiii alikuwa anakuja hadi mitaa a kwetu kuba na wenzake mitaa tote ya Upanga kawaliza sana wahindi na waswahili...
ukisiikia mtu anataka kwenda kariakoo unamshangaa na kumuuliza wewe humuogopi Ali Gulu
Je na sisi watoto wa rab................?
Dah Huyo Jamaa kama nilisikia Story ila ilikuwa ni kama mtu anatania tu kwani Upande wa pili opp na Shule ya Mnazi Mmoja kulikuwa na Mahandaki ya Miaka Mingi sikuelewa yalijengwa for iddi amin au world war 1 au 2, tatizo pale walikuwa wanaishi vibaka tena umenikumbusha nchi hii ndio imeshasahau kuwa na mahandaki endapo vita itatokea dah! na kile kiwanja sijui kama kishauzwa au lah! nitajaribu kupita nione ni jengo gani na la nani limejengwa pale....mnazimoja shuleni kulikuwa na jamaa linaitwa mungu na wanadamu,lilikuwa lina mohican hair cut,lilikuwa linaishi kwenye shimo underground katika maeneo hayo
Name Calling noma nimekumbuka manake unaweza tokea ukataja na langu pia lol... Nawajua hao na wengine siwajui Kbnde kwa Don alikuwa hakosekani lol Wanaona huwajui jui... lol huyo kwenye red ndiye.. Ila Mh!~ Manake Jamaa alikuwa Ni Mkali wa Kufuatilia Totoz Sana.. Nadhani ile kazi yake keshaacha ya ukonda wa Basi lao nadhani kama nilimuona siku kwenye gari Nissan Patrol...A. Ngdk sijasoma nae,
alikua anakaa mitaa gani?
Kamsopi kama wa Mangengesa Mdimi namfahamu hadi kesho,si walikua wanakaa sea view kwenye lile jengo lilikua refu kuliko yote miaka ile? Mule ndio tumejifunzia kupanda lift..
Pia watoto wa Upanga tulikua tunakutana sana Don Bosco na wengine mafundisho St. IMACULATE kwa Fr. Amadori.
Mi nilikaa mitaa hiyohiyo uliyoitaja ila umesahau Lugalo st. Kwa kina Ephraim Kibonde,Manase Zablon,Mtinangi.
Malik Rd kwa kina Telesphory Ndunguru,Undali kina Togani Ngota, Maria Goyayi, Ray Kasonga...
Alykhan kwa kina Koku yule alipata ajali akiwa na Kenedy Seusi akapoteza macho yote.. Unaikumbuka hiyo?
Dah hayo makundi duh pindi hicho sikuweza fahamu.. ila baadae Yalikuja makundi Mengi na yalikuwa yanapigana na Kuchanjana mapanga kwenye Minanda wanapokutana Kuna kundi Moja lilikuwa linaongozwa na Jms mtoto wa Mama kwao Mambo fresh ila anajua sana Fujo alikuwa anakaa kwenye lile gholofa la Wakimbizi Lumumba.. kuna time wakaibuka wahuni wakijiita mapanga Shaa! aibu wanatembe kundi kubwa la zaidi ya watu 20 hadi 30 kwa mwendo wa kasi wakikukuta ujue hali yako ni mbaya...Huyu atakuwa kundi la kina Chite Spy nini?
Huo Wimbo vipi mbona haujakaa kiupanga upanga? Michezo ya Watoto karibu mingi inafanana ,, Ukuti ukuti wa meme wa meme, Komborela, Tampo, Baba na Mama,Yai Bovu,Maji ya Ndimu,Ana ana ana Do, Gololi Sachi, Kidali Po, Tikbar Tik, Soccer, Karata n.k..Nyie watoto wa Upanga kuna mtu anakumbuka haya maneno...
Huo Wimbo vipi mbona haujakaa kiupanga upanga? Michezo ya Watoto karibu mingi inafanana ,, Ukuti ukuti wa meme wa meme, Komborela, Tampo, Baba na Mama,Yai Bovu,Maji ya Ndimu,Ana ana ana Do, Gololi Sachi, Kidali Po, Tikbar Tik, Soccer, Karata n.k..
Nina Ndoo yangu eeeh! yakuteka Maji eeh!
Maji ya Barafu eeh! Watoto msitizame Nyuma..
Yai bovu linanuka..
Maji ya Ndimu Maji Ndimu!.. Saga! saga! saga! huku kichwa kikiwa Chini
Funika Funua.... Hapo Unapigwa Konzi kabla ujanyanyua Kichwa Juu