Watoto wa kariakoo mpo jf?

eeh nyamanoro tena?kweli mganga wako haagizi dagaa...mzee tuko kariakoo sasa si "kibororonyi" na chekereni

kaka hata huku kwetu kuna kariakoo bana! shuka kona ya bwiru halafu pandisha ka unakwenda kilimahewa...
 
yeah Kim..
ilikuwa raha na huru.. Hawa wengine wanaongelea Kariakoo ya juzi naona.. Hawaijui ya zamani... Ambapo,mtaa wa Msimbazi ulikuwa na full functional street lights.. Senene wanajaaa magari si mengi,unaruhusu wanao wakakamate senene barabarani.. Kariakoo hiyo nani mwingine anaijua..
 
kaka hata huku kwetu kuna kariakoo bana! shuka kona ya bwiru halafu pandisha ka unakwenda kilimahewa...
Basi kumbe ngoma droo,sisi huku tunacho kilima pia,but si kilima hewa ni kilima nyege o,bay pale,kilima kibaya kile kimeondoa watu wengi sana
 
ukiwambia watoto walikua wanacheza mpira msimbazi street mchana wakuja watabisha mpaka asubuhi
 
Mkuu kwa hapo mie sitakubishia...kwani sisi wengine ni kizazi cha hivi karibuni tu na tulihamia hapo kariakoo tukitokea Bara
 
huamini au...tena mie si wa niliishi kkoo mpaka leo tuna nyumba kkoo,baina ya msimbazi,kongo na kipata umenipata!

Hebu sema sawa sawa,hizo nyumba ziko vipi msimbazi kongo na kipata?elekeza kama mzawa wa kariakoo,mfano unasema kipata,je kipata na living stone,kipata na nyamwezi au kipata na nini sasa,vivo hivyo msimbazi na hiyo congo maana msimbazi na congo kongo kukutana kidogo muhali,weka wazi tukujue kama mzawa au na wewe ulikuja baadae kama kina sie
 
Mkuu,kwani na wewe ni mkazi wa kariakoo? Na unaishi mitaa ipi?
Kwanini unakataa kuwa pale mtaa wa sikukuu kuna watu wanauza chips hadi asubuhi akiwemo Dullah? Chipsi za kwa Muchacho tushazila sana....sema mitaa ile wasomali ni wengi sana hasa mida ya usiku.
 
naona wataka undani wangu...sikuja baadae nimezaliwa na kukulia kipata kama muelewa umenipata baina ya Msimbazi,Kipata na Kongo.
 
sijakata mzee,sema labda nimeongea kikariakoo zaidi hukunisoma,nimesema chips kwa sio?labda nilisahau kuweka hako kakiulizo ndio mana ikakubabaisha lakini nadhani sasa kwa kuwa umeishi kariakoo utaelewa nilimaanisha nini baada ya kuweka kiulizo kwenye sio.
 
naona wataka undani wangu...sikuja baadae nimezaliwa na kukulia kipata kama muelewa umenipata baina ya Msimbazi,Kipata na Kongo.

kipata na nini basi si useme maana kipata kubwa,sema tu kipata na nini tukutajie majirani zako may be tunawajua..au umesahau kidogo?kusahau imo!
 
ukiwambia watoto walikua wanacheza mpira msimbazi street mchana wakuja watabisha mpaka asubuhi

ha ha ha ha ha haaa... Kim umeniacha hoi.. Mpaka asubuhi..ubishi wa aina hiyo si utasababisha na ugomvii...ha ha ha....
 
Kumbe watoto wa kariakoo jf hamtoshi,tatizo nini?access ya mtandao au?tukiweka watoto wa arusha hapa watafunika mbaya kama kwenye ule uzi wa makalio bar kwa mnaokumbuka si mliona wenyewe watoto wa ki R CHUGA walivyofunguka,kariakoo doro!kwaherini
 
kwa nini Arusha..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…