Watoto Uingereza kuanza kufundishwa zaidi kukabiliana na ‘likes’ za mitandao ya kijamii kuanzia shule za msingi

maforce

JF-Expert Member
Mar 18, 2017
660
615
Kamishna wa Elimu nchini Uingereza Anne Longfield ameweka msisitizo watoto kuanzia shule za msingi nchini humo kufundishwa zaidi kuhusu uelewa wa masuala ya digitali ili kuwasaidia kuepukana na shinikizo la mitandao ya kijamii.

Hii imetokana na uchunguzi uliofanywa nchini humo na kugundua kuwa watoto wengi chini ya miaka 13 kutokana na mitandao ya kijamii akili na muda wao hujikita katika kupata likes na kutengeneza mwonekano wao wanaotaka uonekane kwenye mitandao hiyo.

Uchunguzi huu umebaini pia kuwa matumizi yaliyokithiri ya mitandao hii kwa watoto yanawafanya wajishushe kwenye nyanja mbalimbali kutokana na watu wanao wa-follow kuonekana wako juu zaidi yao kwa namna tofauti tofauti husuani watu maarufu.

ebcc75251cf83d48019c63ddaba14220.jpg
 
Hii mitandao ya kijamii inaharibu sana sio watoto peke yao, bali hata watu wazima wasiojitambua.
 
Duuuh,

Huku kwetu ndo majanga,

Watoto wanaongia mpaka na simu shuleni,

Ukimuiliza atakwambia Dad kanipa zawadi ya birthday
Ni hizo shule zenu za Wnglish medium, huku kwetu Kwamtogole mwalimu hata maana vya dad haelewi
 
Tunahitajika wazazi tubadirike. Tuwaandalie watoto wetu zawadi ambazo zina tija kwao.
ukirudi home mtoto mpelekee game ambalo liatahangisha kichwa chake kwa muda kama ni mkubwa mpeleke hata mbuga za wanyama najua hamshindwi kwa sababu watoto wenu wanawaita dad
 
Back
Top Bottom