WATOTO NJITI: Njia salama za kumuweka Mtoto ili awe salama wakati wote

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Zifuatazo ni njia zinazotumika ili kuhakikisha kuwa mtoto anawekwa katika mazingira ambayo yatamwezesha kuishi vizuri.

Kuhakikisha ngozi ya mtoto inakuwa imegusana na ngozi ya mama ( skin to skin contact/ kangaroo mother care). Hapa mama anashauriwa kumbeba mtoto kwa kumgusisha katk ngozi ya mama uda mwingi ili kumkinga mtoto kupoteza joto.

Kumfunika mtoto kwa nguo nzito iliasipoteze joto. Nguo hizo lazima ziwe safi muda wote ili mtoto asipate homa itokanayo na vijidudu kama vile bacteria nk (sepsis)

Njia nyingine ni kuwaweka watoto hao katika mashine maalum yenye hewa iliyopashwa joto(Air-heated Incubator) ambayo ina joto kadri ya mahitaji ya mtoto njiti.

Njia nyingine ni kutumia matandiko ambayo yana mzunguko wa maji yaliyopashwa joto(Heated water-filled mattress)

Mashine nyingine ni ile inayotoa joto ambalo humfikia mtoto mfano wa joto la jua linavyotufikia(Overhead Radiant warmer).Ambayo picha yake imeonyeshwa hapa chini. Mashine hizi zote zinahitaji uangalizi wa karibu sana muda wote mtoto awekwapo katika mashine hizo ili kugundua mabadiliko yoyote kwa mtoto na kuchukua hatua mara moja

Njia nyingine ni kumpaka mtoto mafuta(Oil application) mafuta husaidia kuziba vitundu vidogovidogo vilivyo katika vinyweleo katika ngozi ya mwili ili kuzuia joto kupttea kupitia vitundu hivyo

Njia nyingine ni kumfunika mtoto kwa mfuko maalum unaojulikana kama polythene sheet.mfuko huu ni maalumu kwa watoto lakini unafanya kazi sawa na mifuko mingine wanayotumia mama ntilie kufunikia vyakula visipoe kama vile maandazi na wali,kwa sababu unazuia joto kupotea

mtoto azaliwapo mwili wake huwa umefunikwa na kitu mafuta mazito kama girisi,( Vernix caseosa) wengine huona kama ni uchafu la! Kama mtoto amezaliwa njiti usijaribu kutoa maana utasababisha ngozi ya mtoto kuwa wazi hivyo kupoteza joto kwa wingi.

Mtoto njiti asiogeshwe mpaka siku aliyo tarajiwa kuzaliwa ifike, hivyo hakikisha mazingira ya kumhudumia yanazingatia usafi wa hali ya juu(Neonatal Intensive Care Unit Protocol)

Hakikisha mtoto anapata lishe kwa mujibu wa taratibu za kulisha watoto njiti(Neonatal and low birth weight feeding schedule
 
Points nzuri Sana. Lakini hapo kwa kuogeshwa Inategemea na mtoto alizaliwa katika hali gani, Kuna mtoto mwingine anazaliwa premature lakini anaweza kucontrol joto lake la mwili.
Na anakuwa Hana complications nyingi sema tu anakuwa Hana uzito unaotakiwa kwa mtoto wa 2.5kgs,

Baada ya kujifungua watamwangalia kwa siku chache mnaruhusiwa. Hapo nyumbani mama atafanya kangaroo skin to skin mother care. Huyo unaweza kumwogesha ama kusponge bath baada ya wiki Kama mbili sababu joto la mwili wake liko sawa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom