Watoto ni baraka yahitaji subira kina baba

Watoto ni baraka yahitaji subira kina baba

kichungwaa

Member
Joined
Oct 21, 2014
Posts
70
Reaction score
15
Habari zenu wakuu,

Kina baba tunajua mnapenda sana watoto sio kama kipindi cha nyuma lakini yahitaji uvumilivu na subira pia imekuwa ukiona miezi tu hakuna dalili mnaanza visa na maneno ya kejeli na dharau ndani ya nyumba.

Nimeshindwa namshauri vipi rafiki yangu wanajamvi mnisaidie ana mchumba wake wana mwaka tu na ni vijana tu kiumri hawajifka above 30s.

Lakini mwanaume ameshaanza mdomo jamani na kuchepuka kutafuta mtoto hakuna amani ndani na ni wachumba tu kina baba kuweni kidogo na uvumilivu mbono yakiwakuta nyie mnavumiliwa (mke ana tatozo la mirija kuziba na anatafuta matibabu).

Nimshauri vipi rafiki yangu na anampenda sana mume wake.
 
Kama ni wachumba na wasubili ndoa kwanza alfu suala la watoto ni kwa uwezo wa Mungu, unaweza wapata hata kumi Mwenyezi Mungu akiwapenda anawachukua wooote, Mwambie linalompata mwenzi wake na yeye laweza kumpata hatuna uwezo wa kutambua ni nini kilichondani ya miili yetu
 
Katika moja ya mitihani migumu ambayo wanandoa huwa wanapitia ni hii ya kukosa mtoto.

Kama ni wachumba sina cha kushauri. But kama ni mume na mke tayari wapo ndani ya ndoa, inabidi mdada awe karibu na Mungu sana kwa ajili ya kuombea familia yake na ulinzi wa ndoa yaje pia kwa ajili ya kuomba Mungu amfungue. Mungu anajibu kwa njia ambayo sisi wanadamu hatuwezi hata kuitarajia.

Tatizo la ndoa nyingi, ni watu kukutana fb, insta, badoo, jf, imo n.k. zinapotokea changamoto zandoa hawawesi kustand maana mifumo yao ya maisha haiko either sambamba au haina msingi imara ya kuweza kuvumilia changamoto hizo.
 
Ye mwanaume kafanya sperm analysis??!!!
Yawezekana hata yeye ana shoot blanks tu. . . . . .Waende wote hospitali kwa wataalamu

Halafu uwapeleke ka Kaizer wakapewe ushauri wa kindoa aanze huyo dada akishaelewa somo atamuelekeza huyo mtarajiwa wake
 
Last edited by a moderator:
Kukosa watoto sio kosa la mwanamke pekee, hata mwanaume nae anachangia.
Waende hopsital wote wajue tatizo lipo wapi.
 
Waowane kwanza watoto majaaliwa, na huyo rafiki yako nae hashukuru mungu kumuonyeshea kua huyo mwanamme sie?
Anachepuka anajua na still anataka kuzaaa yuko desparate sana? ana miaka mingapi rafiki yako?
 
Ye mwanaume kafanya sperm analysis??!!!
Yawezekana hata yeye ana shoot blanks tu. . . . . .Waende wote hospitali kwa wataalamu

Halafu uwapeleke ka Kaizer wakapewe ushauri wa kindoa aanze huyo dada akishaelewa somo atamuelekeza huyo mtarajiwa wake

Ewaaaaa....
 
Last edited by a moderator:
Kama bado wachumba...wajue kutafuta mtoto kipindi hicho ni kuzini na Mungu hapendi... kuna wanandoa wanakaa miaka 10 ndo wanapata watoto!! Haya mambo yanashangaza hata sayansi zinashindwa...ni kumwomba Mungu.
 
Mbona lipo wazi????

Huyo mwanaume hamfai.....

Halafu kuzaa kabla ya ndoa ni sifa eeeh???
 
Back
Top Bottom