Watoto mabonge

Kaniki1974

JF-Expert Member
Dec 2, 2008
352
22
Sina hakika kama hili limekwishaulizwa hapa awali.

Hivi kwa nini watoto wengi siku hizi ni wanene sana (mabonge) overweight? Tatizo hili husababishwa na nini? Nini madhara yake? Nini chaweza kufanyika kupunguza hali hii na kipi kifanyike kwa mtoto ambaye ni bonge tayari?

Thanks kwa ushauri.
 
Unene husababishwa aidha ni genetic (kwamba unene ni wa kuridhi ) au kula sana vyakula ambavyo ni unhealthy (chokollete, pipi, vyakula vyenye sukari nyingi, vyakula vyenye mafuta mengi). au mtoto kuwa mvivu kucheza yaani yeye ni computer au TV,

Madhara, unene hukizidi hunakuwa Obesity na hapa mtoto wanaweza kupata matatizo mbalimbali kama Kisukari, matatizo ya moyo na nk.

Kitu ambacho unaweza kuzuia ni hakikisha mtoto wako anakula healthy foods, hasile sana vitu kama sweets au vitu vya mafuta mengi, au kama mafuta basi mafuta ya mimea ni mazuri zaidi jaribu kumcontrol (kumbuka mtoto huwezi kumyima chokolate au pipi kabisa) Matunda, samaki, mboga za majani ni muhimu sana kwa mtoto.

Jaribu kumfanya mtoto hawe activ anaweza kukimbia, kucheza mpira, kutembea, kucheza sana na wenzake, hasikae sana kwenye TV au Computer.

Alinda
 
Sina hakika kama hili limekwishaulizwa hapa awali.

Hivi kwa nini watoto wengi siku hizi ni wanene sana (mabonge) overweight? Tatizo hili husababishwa na nini? Nini madhara yake? Nini chaweza kufanyika kupunguza hali hii na kipi kifanyike kwa mtoto ambaye ni bonge tayari?

Thanks kwa ushauri.


95% ya hawa watoto ni kutoka familia ambazo zina pesa, wanawalisha sana junk food toka South Africa/China/India etc. matokeo yake hawa watoto watakuwa mazezeta tu baadaye trust me. Hivi vyakula vya kopo/maziwa/ mkate/ngano/matunda,/ mafuta/nyama (kuku/ng'ombe) toka South Africa/China/India vina kemikali nyingi sana ndo maana watoto wengi wanakuwa wanene sana kulinganisha na umri wao. Tatizo ni ulimbukeni wa wazazi wao kupenda vya kutoka majuu badala ya kula kuku wa kienyeji/ matunda yako mengi, ngano tunayo nyingi, mchele mwingi toka mbeya. Hawa wazazi matokeo watayaona tu baadaye wakati huo itakuwa haa ilikuwaje, hivyo watoto watakuwa mzigo sana kwa familia.
 
Back
Top Bottom