Filipo
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 9,342
- 5,536
Imetokea huko Longido, mkoani Arusha. Watoto wa kiume wakimsaidia mama yao aliamua kumfuata baba yao ambaye alikuwa nyumba ndogo kwenda kumfumania baba yao. Kwa bahati mbaya mzee akachoropoka na kutokomea ila bibie alikamatwa na bi mkubwa akisaidiana na watoto, tena akiwa mtupu wakampeleka kituoni. Kituoni wakashindwa kumfungulia mashtaka wakaamua kumwacha huru. Bibie akawa kama amepatwa na uchizi. Katoka nje ya kituo kaipasua vioo gari ya hao watoto aina ya suzuki na kuiacha na side mirror tu! Walipojaribu kumkamata hawakufanikiwa. Hivi ninapoandika si baba wala bibie anayejulikana alipo!
Ninachojiuliza mimi ni je ingekuwa ni mama yao, wangemsaidia mshua kwenda kwenye fumanizi? Na je wangemkuta mtupu? Kumbuka hawa ni watoto wa kiume. Na je watoto hawa wapo sahihi ama la?
Ninachojiuliza mimi ni je ingekuwa ni mama yao, wangemsaidia mshua kwenda kwenye fumanizi? Na je wangemkuta mtupu? Kumbuka hawa ni watoto wa kiume. Na je watoto hawa wapo sahihi ama la?