Watoa huduma ndogo ya fedha watakiwa kujisajili na kukata leseni

rose mzalendo

Member
Mar 5, 2019
71
114
Watoa huduma hiyo wanatakiwa kujisajili kabla ya tarehe 31 Oktoba, 2020. Aidha Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamwaja, alisema lengo la kusajili na kutoa leseni kwa watoa huduma hao ni kuiwezesha Serikali kuwatambua ili kuboresha usimamizi na udhibiti wa Sekta Ndogo ya Fedha nchini na kuwa na Sekta ya Fedha iliyo endelevu na yenye kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini kwa kuwa sekta hiyo ni muhimu katika uchumi wa nchi.

Sekta hii inatoa huduma za fedha kwa wananchi wa kipato cha chini, zinachangia kuinua uchumi na kuongeza kipato, kwa mujibu wa utafiti wa Finscope wa mwaka 2017, 55.3% ya nguvukazi ya Taifa wanapata huduma za fedha kutoka Taasisi za Huduma Ndogo za Fedha.
 
Back
Top Bottom