Watishia kuacha kulima miwa

Watishia kuacha kulima miwa

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
WAKULIMA wa miwa kutoka vyama sita wa Bonde la Ruhembe, wilayani Kilosa , wameazimia kuacha kulima miwa kufuatia hatua ya Kampuni ya Sukari ya Ilovo, kupunguza ya bei ya miwa kutoka Sh 69,000 hadi kufikia Sh 62,889 kwa tani.

Wakulima hao walitoa msimamo huo juzi katika mkutano wa pamoja ulifanyika katika Kata ya kidodi na kushirikisha viongozi wa vyama hivyo vya wakulima wa miwa.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Muungano wa vyama hivyo,Wenslaus Gwira, alisema anguko hilo la bei kwa tani moja ya miwa, ni sawa na asilimia 10 ya bei ya miwa iliyopo awali.

Alisema jitihada za kutaka kuonana na uongozi wa Kampuni ya Ilovo, ili kutatua tatizo hilo zimegonga mwamba.

Mwenyekiti huyo alisema Meneja wa kampuni hiyo amedai kuwa kushuka kwa bei ya miwa kumetokana kutokuwepo kwa soko hapa nchini na kwamba hali hiyo, imechangiwa na Serikali kutoa fursa ya kuingiza sukari kutoka nje ya nchi.

Alisema wakulima wamefikia uamuzi hao kutokana na kilimo cha zao hilo kuendelea kuwapa umasikini wa kipato.

Omary Abdallah ambaye ni kiongozi wa Chama cha Wakulima wa Miwa cha Kidodi, alisema wameamua kufanya hivyo ili kulinda maslahi ya wakulima wa miwa hapa nchini.

Alisema kuwa suala hilo sasa limeingiliwa na siasa na kwamba kama hatua za haraka hazitachukuliwam wakulima wataacha kulima miwa.

Akijibu malalamiko ya wakulima hao, Meneja Mkuu wa Ilove, Don Carter, alisema kushuka kwa bei hiyo kumetokana na Serikali kuruhusu kuingizwa kwa sukari kutoka nje ya nchi.

Alisema kwa sasa kuna zaidi ya tani 40,000 za sukari zikiwa zimerundikana.

Source: Mwananchi
 
Wasiishie kutisha tu - iwapo hakuna tija waache!
 
Back
Top Bottom