Wateule wa Rais mguu nje, mguu ndani

Wateule wa Rais mguu nje, mguu ndani

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Vigogo walioteuliwa na Rais, Dkt. JPM awamu iliyoisha (2015 - 2020) hawaelewi hatma ya nafasi zao hasa baada ya Mhe. Rais kuapishwa leo Jijini Dodoma. Kwa kawaida lazima aunde safu mpya.

Wapo RC, DC, DAS, DED, Mawaziri, Naibu Waziri, Wakurugenzi wa Mashirika ya Umma, Makamishna nk.

Yetu macho
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ana Jambo Lake Muda Wowote Kuanzia Sasa Hivi

Umeona Bendera Iliposhushwa Tu [emoji848][emoji848][emoji849][emoji849]

Waziri Mkuu Akaitwa Mstaafu Hapo Hapo [emoji55][emoji2955]

Hao Wengine, Wanasali Kama Alivyoweza Kusema Sheikh Alhad. Nitaomba Kwa Jina Yesu Na Mohammed!!

Wote Muda Huu Pressure Zipo Juu Usawa Wa Bahari Ila Vyeo Vyao Vya Siasa Vina Pressure

Kuna Watu Wanahaha Kupasha Mwili Moto Wachukue Nafasi Haraka, Wengine Wakiomba Wasiondolewe
 
Hongereni mnao fuatilia majaliwa ya hii illegitimate siri kali?

Tangu lini kwenye hizi transitions:

"Waziri mkuu akaendelea kupeta actively kama waziri mkuu na mawaziri kama mawaziri na yule jamaa wa kamati ya maadili kuniga kanzu la usupika?"
 
Ngwajima kwenye baraza la mawaziri atatoa mchangO mkubwa sana kwa taifa Mueshimiwa Askofu Waziri Ngwajima.
 
Wenye akili zao wanawacheka tu, mnavyojazana ujinga kama mlivyoiba kura, na si mda mrefu mtaanza kutoleana siri zenu.
 
Ngwajima kwenye baraza la mawaziri atatoa mchangO mkubwa sana kwa taifa Mueshimiwa Askofu Waziri Ngwajima
Gwajima abaki kuwa mbunge wa kawaida. Na akiwa mbunge wa kawaida ndo atanoga, akiwa sehemu ya serikali hatanoga.
 
Tofauti na watu wanavyofikiri upinzani umeumia Sana. Wana CCM ndio wataumia Sana na utawala wa Magufuri madna kawapora chama na dola kapeleka Bahima empire.
 
Hii nchi ni yetu wote.

Kila mmoja apewe nafasi ya kuonyesha uwezo wake.

Waliokwisha pata kwa miaka mitano inabidi sasa wapumzishwe ili wengine nao wapate. Uongozi mbali na siasa lakini ni ajira yenye maslahi makubwa ukilinganisha na taaluma nyingine kwenye ajira za umma.

Hivyo kutokana na ukosefu wa ajira basi waliopewa nafasi kwa miaka mitano sasa ni zamu yao kwenda kutumia uzoefu wao kujiajiri mana mitaji wanayo mikubwa.

Mtu kama Makonda tunategemea kumwona akianzisha kampuni yake mbinafsi na kuisimamia kwa wazi kabisa kama alivyo Mo.
Prof. Mwakyembe ana Digrii NNE na Daktari wa Falsafa. Mwalimu wa vyuo vikuu Mbalimbali duniani . Huyu anaweza akaanzisha hata chuo binafsi na kuajiri kuliko kuendelea kufanya uzalishaji na kuchapa kazi mdomoni tu kama Musukuma wa Darasa la Saba.

Tutapata wapi kodi kama wenye mitaji wataendelea kungangania maofisi ya umma huku wasio na ajira wakizidi kuongezeka. Walipwe viinua mgongo vyao wakajiajiri wengine waingie kazini.

Pia spika wa Bunge asipewe mbunge ambaye tayari ameshapata ajira ya ubunge.

Nafasi hiyo apewe mwana CCM mwingine au hata wa upinzani lakini ambaye yupo nje ya Bunge. Uchaguzi umekwisha tuangalie uchumi wa nchi na maisha ya watu sio kujijenga kisiasa tuuuuu kila muda ,tujenge nchi kwa manufaa ya wote.
 
Ninakaa huku karibu na mpakani, naona magari mengi yanaenda kwa mganga.. Jamani kila mtu amloge Magufuli ili amteue si mtafanya mwezenu awe .....sasa .acheni kutafuta cheo kwa ndumba
 
Hamis tabasamu mbunge wa sengerema ,wizara ya elimu inamfaa 💯
 
Back
Top Bottom