Watendaji Wa Mahakama watakiwa kujiongeza kimawazo katika Usimamizi wa Utoaji wa Haki

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,612
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Profesa Elisante Ole Gabriel amewataka wajumbe wa menejimenti ya Mahakama kujiuliza thamani yao ndani ya mhimili huo wa usimamiaji utoaji haki, katika kutekeleza majukumu yao.

Profesa Gabriel ameipa menejimenti hiyo changamoto hiyo wakati akifungua mafunzo ya utendaji kazi kwa wajumbe hao, katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki, cha Masuala ya Familia, Temeke Dar es Salaam.

Amesema wao kwa nafasi zao kama wajumbe wa menejimenti wana mchango mkubwa katika mafanikio yanayopatikana katika taasisi hiyo na kwamba wanapaswa kufanya mambo sahihi kwa usahihi ili kuwasaidia Watanzania kupata haki wanayostahili.

Profesa Gabriel amesisitiza kama viongozi katika vitengo vyao, wanapaswa kutoa mchango wa mawazo na kushauri viongozi wakuu ili kujiongezea thamani na si kutekeleza maagizo wanayopewa pekee.

“Elewa hautakumbukwa kwa sababu ya nafasi yako, utakumbukwa kwa mchango wako katika kuboresha uamuzi unaofanywa. Hakikisha uamuzi unaofanya unamsaidia Mtanzania wa ngazi yoyote ambaye anatafuta haki yake,” amesema Profesa Gabriel na kuongeza:

“Onyesha thamani yako, ndiyo utakayokufanya kukubukwa na siyo rangi yako, sura yako wala hata vyeti vyako.

“Utakumbukwa kwa mchango wako katika jamii. Ninyi ndio matairi katika mafànikio ya mahakama, lazima mjiulize mnathamani gani ndani ya mahakama haijalishi una nafasi gani ilimradi unafanya kazi.”

Amewataka washiriki hao wa mafunzom kuwa sehemu ya suruhisho ili watu wanaowasimamia wajivunie kusimamiwa nao na sio washangilie watakapohamishwa au kupandishwa vyeo.

“Nyinyi sio bomba la kupeleka mambo kwa viongozi wenu, bali ni watu wa kusaidia kuchakata na kuyapeleka na maoni na mapendekezo ili kufanya uamuzi,” amesema Profesa Gabriel na kusisitiza:

“Mfano, kama wewe ni mkuu wa idara au mkuu wa kitengo, haitapendeza kuwa mtu wa kupokea mambo na kufikisha kwa kiongozi bila wewe kuweka thamani yako kwenye mchakato wa kufanya uamuzi. Usipoweka thamani yoyote hufai na huna thamani yoyote,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi msaidizi wamafunzo Mahakama ya Tanzania, Patricia Ngunguru alisema mafunzo hayo ya siku tatu yanalengo la kuwajengea uwezo ili kuwawezesha kutekeleza kazi zao vizuri.

"Kupitia mafunzo,o haya tunatarajia yatawasaidia kuleta mabadiliko ya kifikra na kuwapa weledi katika kutekeleza kazi zanu," alisema Patricia.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom