Wateja wanaleta hela za noti huku wamezichana kwenye kona

Nonpartisan

JF-Expert Member
Dec 15, 2016
278
254
Wadau ninaswali kidogo baadhi ya pesa ninazopokea ofisini kwangu wateja wanazichana kwenye kona kwa makusudi, ni kwanini?
Msaada wa mawazo
9abc3affb4d65545a08d1a7e4f3f8b4e.jpg
 
We jamaa umefanya siku yangu kuwa na furaha, umenifurahisha, (don't mind) ela imekuwa ngumu hadi watu wanaisi chuma ulete ipo kazini, biashara imekuwa ngumu, pesa haionekani
Hapa kazi tu.
 
We jamaa umefanya siku yangu kuwa na furaha, umenifurahisha, (don't mind) ela imekuwa ngumu hadi watu wanaisi chuma ulete ipo kazini, biashara imekuwa ngumu, pesa haionekani
Hapa kazi tu.
watu mna majibu mujarabu kwa kweli
 
Iyo anayechana huwa ni muuzaji baada ya kuipokea toka kwa mteja.Nia huwa ni kuzuia chum ulete(morogoro wanaita bukula).Muuzaji baada ya kuipokea toka kwa mteja kabla ya kuichanganya na zingine ndio huichana kidogo hapo akiwa na maana anaondoa uchawi wa chuma ulete....Kuna anayeweka kipande cha mkaa katika mfuko/droo/pochi ya makusanyo ya mauzo(hela) kama kizuia chuma ulete....Mbinu zote sina uhakika nazo mana sijawahi kutumia na sina imani iyo..UKINIIBIA NAKUJIA NDOTONI
 
Mi sipokei noti ilyochanwa kwenye kona kwa sababu imechanwa makusadi lakini kama imechakaa ni sawa.
 
Hiyo ni kuzuia Chuma Ulete.

Huwa wanachana kwenye pembe ama wanachora kupiga mstari kwa kalamu nyekundu katikati ya noti.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom