Wateja Vodacom kuendelea kupata huduma ya luku kupitia M-Pesa

Vodacom Tanzania

Official Account
Aug 12, 2013
320
107
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc inapenda kuwataarifu wateja wake na Watanzania kwa ujumla kwamba, itaendelea kutoa huduma ya ununuzi wa umeme (LUKU) kupitia mfumo wa malipo wa serikali ujulikanao kama Government e-Payment Gateway (GePG).

Kufuatia mabadiliko yaliyotangazwa hivi karibuni na kampuni ya kuzalisha na kutoa huduma ya umeme nchini (TANESCO) kuhusu kuanza kutoa huduma ya kununua umeme kwa kupitia mfumo wa Serikali wa GePG, Vodacom Tanzania Plc inapenda kuwatoa hofu Wateja wake kwamba wataendela kupata huduma ya kununua umeme ya LUKU kupitia Vodacom M-Pesa kama ilivyokuwa mwanzo.

Mfumo mpya utaiwezesha Tanesco kuunganisha mauzo moja kwa moja kutoka makampuni mengine ya simu na mabenki kwenda GePG ikiwa ni matakwa ya sheria kwa taasisi za Serikali.

Kutakuwa na ongezeko la asilimia moja nukta moja ya gharama halisi (1.1%) anayotozwa Mteja ili kununua umeme pindi atumiapo huduma ya M-Pesa.

Vodacom inawahakikishia Wateja wake kwamba itaendelea kutoa huduma ya LUKU kupitia M-Pesa ambayo pia inapatikana katika App za Apple, na Android.
 
Ahsante kwa kujiunga,ila hawa Tanesco wanasumbua sana,anyway,tutafika tu
 
ilo ongezeko la 1.1% inatoka wapi ...kwanini msifanye conversation btn vodacom na wananchi ...sasa hivi maisha magumu ...kuweni na huruma ...maza f
 
Hapa tu ndo nachoka mm, pamoja na ugumu wa maisha unatukabiri lkn bado tunajengewa mazingira magumu kupata huduma, Nadhan serikali yetu uliangalie hili maana wao ndo wanaotupeleka kwenye mifumo ya namna hii
 
Hana nimenunua umeme usiku,mpaka sasa umeme hamjanipa na pesa yangu pia hamja rudisha,hivi nyie voda mnajua lakini maisha yalivyo magumu?
 
Serikali makini huwapunguzia changamoto za kimaisha wananchi wake...serikali dhalimu huwaongezea changamoto wananchi wake

Ila yule jamaa mwenye kuvaa suti zenye makoti yenye mikono mirefu hadi kwenye vidole akiongea unaweza hisi serikali ipo kwaajili ya kumkomboa mtu mnyonge kweli kumbe anaongea kinyume chake, kila siku wanafanya maisha yanazidi kuwa magumu.
 
Hata tukikutukana au Kukuuliza maswali magumu tutakuwa tunakuonea tu juu ya hiyo 1.1%. Ngoja tuzikusanye tununue Meli ya kubena abiria 5,000 kwa keshi ndugu yangu @vodacome
 
Je hiyo 1.1% ni Vodacom tu au hadi mitandao mingine na benk?
 
Kumbe kuzunguka kote huko ni gea tu ya kutuongezea walaji gharama?
Hakuna namna wacha tuendelee kuisoma namba!
 
hivi yule kigogo wa tanesco aliyeachishwa kazi sababu ya kupandisha bei ya luku anajisikiaje ikiwa sasa umepandishwa kimya kimya na makato juu
 
Kumbe kuzunguka kote huko ni gea tu ya kutuongezea walaji gharama?
Hakuna namna wacha tuendelee kuisoma namba!
Kabisa, ukishaona wanagoma hiki au kile ujuwe muda si mrefu raia anaumia tu! Ngoja niandae maandamano yangu binafsi kwenda TANESCO @TRA na vodacom..
Kama hapo Vodacom Tanzania waligoma ili waongeze 1.1% ya tozo kwenye ununuzi wa LUKU TANESCO !
Hawa watu hawana huruma kabisa na raia..:(:mad::confused:
 
1.1,, kwahiyo ss hv itakuwa ukinunua umeme unakatwa na pesa ya kununulia,, sheeenzy
 
Back
Top Bottom