Watch "Clean beautiful STREETS of KIGALI, RWANDA" Tuache maneno

ka nchi juzi tu kalikua na mtifuano leo kanavutia sisi tumekalia maneno na majungu tu
 
RC Makonda kataka kuleta wachina mijitu nusura ipasuke kwa hasira, huu uchafu wetu unaneemesha watu, tunamafunza watu yananawiri kwenye uchafu.
 
RC Makonda kataka kuleta wachina mijitu nusura ipasuke kwa hasira, huu uchafu wetu unaneemesha watu, tunamafunza watu yananawiri kwenye uchafu.
Bila ya kuwashirikisha wenye mji wao?? Yeye anayo bajeti ya kuwalipa au nguvu ya kisheria (Mandate) ya kuingia mkataba na hao wachina?
 
Niliwahi kuisifu Rwanda ya Kagame, nikaitwa mtutsi, nikaambiwa kwamba ninaisaliti Tanzania. Katika mazingira masafi kiasi hicho kunaweza kuwepo ule ugonjwa wa kipindupindu?. Anayekwambia kuwa nguo yako ya ndani inaonekana kwa kila mtu anasema hivyo kwa sababu anakupenda na sio kuwa anataka kukukejeli.

Tuna miaka 55 ya kuwa huru lakini ugonjwa unaohusiana na uchafu bado unatutesa!. Rais Magufuli aongeze kununa, aongeze utemi ili ujuaji wetu usiendelee kuwa kikwazo cha ustawi wetu.
 
Ndio tatizo letu, midomo mirefu kama chuchunge
Huo ndiyo ukweli, hao mwaka 1994 walichinjana mpaka wakafikia karibia milioni moja na leo ndiyo huo mji wao unavyooneka. Sisi tunaoishi kwenye "kisiwa cha amani" tunao mji wowote ambao kwa usafi na unadhifu wake angalau unafikia nusu ya huo. Hiyo amani na utulivu vimetusadia nini kupiga hatua ya maendeleo?
 
Back
Top Bottom