Watawala wetu wanatengeneza chuki katika Jamii yetu

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,073
Nianze kwa kunukuu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) ambayo inatamka kuwa nchi yetu itakuwa na mfumo wa vyama vingi na vyama hivyo vinatakiwa vifanye shughuli zake vikiwa huru bila kuingiliwa na chombo kingine chochote.

Sasa kama Katiba ya nchi yetu inatamka hivyo, ni kwanini Rais wetu alitamka kuwa vyama vya siasa vya upinzani visifanye mikutano yoyote ya ndani na nje hadi mwaka 2020 wakati yeye mwenyewe na chama chake cha CCM wanaendelea kufanya kampeni nchi nzima kila siku bila kubughuziwa na Polisi?

Inakuwaje pia Polisi kila siku wanatekeleza amri hiyo ya Rais ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa kwa kuwakamata viongozi wa kisiasa wa upinzani wanapojaribu kufanya mikutano, wakati wakijua kuwa amri hiyo ya Rais siyo halali kwa kuwa inavunja Katiba ya nchi yetu waziwazi?

Hebu pia ninukuu tena Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 18(1) ambayo inatamka kuwa kila mwananchi atakuwa huru kutoa maoni yake nje bila kubughuziwa na chombp kingine chochote.

Iwapo Katiba ya nchi yetu inatamka hivyo, Je Jeshi la Polisi linapata wapi mamlaka ya kuwakamata watu wengi kila siku kwa tuhuma za uchochezi wakati kiuhalisia watu hao walikuwa wakitekeleza haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni yao?

Hivi tangu lini msamiati wa lugha yetu ya kiswahili umebadilika na kuleta tafsiri mpya kuwa kwa yeyote anayeikosoa serikali ya awamu ya 5 kutafsiriwa kuwa ni uchochezi na kutaka kuhatarisha usalama wa nchi?

Hivi ni kwanini pia tumekuwa tukilisikia Jeshi letu la Polisi likijibu mara kwa mara kuwa wanatekeleza amri toka juu ya kuwakamata watu wakati taaluma ya kazi yao hawapaswi kupokea maagizo badala yake wao wenyewe ndiyo wajiridhishe kuwa huyo mtu wanayemkamata ni kweli ana makosa ambayo yanastahili kukamatwa na kuwekwa ndani?

Nimeanza kwa kunukuu Ibara hizo za Katiba ili nionyeshe kuwa vitendo vinavyofanywa na Jeshi letu la Polisi kwa kila siku kuwakamata watu mbalimbali wakiwemo viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa vya upinzani kwa kudai kuwa wametoa lugha za uchochezi wakati kiuhalisia ni kuwa wanetunia haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni yao kuwa ni vitendo ambavyo siyo halali na vinavunja Katiba ya nchi yetu.

Sasa nini kinaelekea kutokea kufuatia Jeshi letu la Polisi kutofanya shughuli zake kwa weledi na badala yake kutumika kupokea maagizo kutoka kwa watawala wetu ni kutengeneza chuki ndani ya Jamii kwa wananchi kuliona Jeshi lao la Polisi kuwa linstumika na watawala kuwanyanyasa raia wasio na hatia.

Inapofikia hatua hiyo inaliweka Taifa katika mazingira magumu kwa kuwa watu wanakuwa wanaishi katika hofu ya wakati wote kuhofia kukamatwa na Jeshi letu la Polisi kila wanapotaka kutumia haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni yao.

Njia pekee ya nchi yetu kuepuka kujenga chuki ndani ya Jamii ni kwa watawala wetu kutekeleza wajibu wao kwa kuilinda na kuitii Katiba ya nchi yetu na Jeshi letu la Polisi kutekeleza wajibu wao kwa weledi wa kazi yao kutotakiwa kujihusisha na kujiegemeza na chama tawala na badala yake wanatakiwa wawe fair kwa vyama vyote bila kufanya upendeleo kwa chama tawala.

Iwapo watawala wetu wataendeleza staili yao ya kutawala kwa kuvitumia vyombo vyake vya dola kuviminya vyama vya siasa vya upinzani na kuendelea kuminya Uhuru wa wananchi wa kutoa maoni yao nje, hakika utawala huu wa awamu ya 5 utakuwa unatengeneza chuki ndani ya Jamii kitu ambacho ni cha hatari sana kinachoweza kuliangamiza Taifa letu.

Mungu ibariki Tanzania na iepushe kuingia kwenye chuki baina ya wananchi na vyombo vyao vya dola.
 
Awamu hii Kuna upendeleo wa wazi kwa upande wa kijani

Ova
 
Uko sahihi kabisa mkuu.
 
Awamu hii Kuna upendeleo wa wazi kwa upande wa kijani

Ova
Tokea nchi yetu irejee kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, hii ndiyo awamu pekee ambayo mfumo wake wa uongozi unaifanya nchi yetu ionekane kama ipo kwenye mfumo wa chama kimoja..........

Japo theoretically nchi inajihesabu ipo kwenye mfumo wa vingi.

Lakini practically hakika tumerudi kwenye mfumo wa chama kimoja!
 
Tokea nchi yetu irejee kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, hii ndiyo awamu pekee ambayo mfumo wake wa uongozi unaifanya nchi yetu ionekane kama ipo kwenye mfumo wa chama kimoja..........

Japo theoretically nchi najihesabu ipo kwenye mfumo wa vingi.

Lakini practically hakika tumerudi kwenye mfumo wa chama kimoja!
Anataka kuuwa upinzani

Ova
 
Anataka kuuwa upinzani

Ova
Hakuna Taifa lolote duniani lililowahi kuua upinzani kwa kutumia vyombo vya dola kama anavyotaka kufanya Bwana mkubwa wetu.

Kama kweli yeye anaamini yeye ni Rais wa wanyonge kama anavyojinadi na amekuwa wakati wote akipigania maslahi ya Taifa letu.

Sasa ni kitu gani kinachomfanya aogope kupambana kwa hoja na wapinzani majukwaani na wananchi ndiyo waamue MCHELE upi na PUMBA
ipi?

Kwani yeye Mkulu haujui ule msemo unaosema kuwa kizuri chajiuza na kubaya chajitembeza?

Kama kweli wapinzani wameishiwa Sera za kuwaeleza watanzania , awaache WAJITEMBEZE na yeye na CCM yake WAJIUZE na wawaachie wananchi waamue mchele upi na pumba ipi......
 
lipumbaseif.jpg
 
Nimeipenda hiyo.....

Kwa Profeseri kwa kuwa ni mtu 'wao' ruksa kufanya mikutano ya siasa.....

Ika kwa Maalim kwa kuwa ni 'mwiba' mkubwa kwao wanampiga Stop asifanye vikao vyovyote.

Watawala wetu wamekuwa wakitumia muda na nguvu nyingi sana kupambana na upinzani.

Hali inayofanya ile 'njonzi' ya kuigeuza kuwa ya viwanda ifikapo 2025 kuanza kutoweka kwa kasi.
 
kwanza ni aibu kwa nchi yenye watu karibia 50ml kutumia miongozo ya 1977

poor TZ
Ni hao hao CCM waliigomea ile Katiba nzuri iliyoandaliwa na Tume ya Katiba ya Jaji Warioba na badala yake wakatujia na Katiba yao ya Lumumba ambayo waliipitisha kwa mbwembwe nyingi ambayo nayo hivi sasa imebuma......
 
Umesema kweli tupu Mkuu Mystery..

Nchi hivi sasa inapasuliwa vipande vipande na inakopelekwa Sipo ambapo mfumo wa vyama vingi unaelekeza Nchi inavyopaswa kuwa..

Chuki miongoni mwa watanzania ni kubwa.

Nina mashaka sana kwa mfano kama watu wa CCM watakuwa na uhuru mkubwa wa kufanya siasa huko mbeleni bila ya kupata Ulinzi wa Dola/Polisi kwa kuogopa kubugudhiwa maana chuki dhidi yao inazidi kuwa kubwa sana (siombei iwe ivyo though).
 
sad
 
Kibaya zaidi ni watu wanaiona hiyo hali inayotengenezwa na watawala na chama cha CCM lakini wanaamua kukaa kimya kwa kuogopa kuwa wataitwa wachochezi........

Hivi ni nani alitegemea kutokea kwa tukio lile lililotokea hivi karibuni kwa wabunge wa upinzani kugomea kuhudhuria futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa?

Lakini hivi unategemea kweli wabunge wa upinzani waweze kuhudhuria hafla kama ile iliyoandaliwa na PM wakati Spika wa Bunge , Ndugai akifanya upendeleo wa wazi mle Bungeni kwa kuwanyanyasa na kuwaonea wabunge wa upinzani na kuwafukuza mle Bungeni pamoja na kuwafungia kutohudhuria Bungeni wakati wabunge wa CCM wakifanya makosa makubwa zaidi na Spika huyo huyo aliwakingia kifua na kuwalinda wabunge wenzake wa CCM?
 
Back
Top Bottom