Watawala wetu na Siasa za "Vikapanda Vikashuka" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watawala wetu na Siasa za "Vikapanda Vikashuka"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 9, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  shatilavikapandavikashuka.jpg
  Kama kuna vitu ambavyo watu wazima ni wepesi kuvishtukia ni pale ambapo mtu mzima mwingine anapojaribu kukuingiza mjini kwa kukupa story za "fix". Mara nyingi stori hizi hutumiwa kuficha udhaifu na husimuliwa kiasi cha kuzisafanya zionekane zina ukweli wa aina fulani. Unapoenda kurudia stori hizo kwa watu wengine unashindwa hata kusimulia yote unabakia kusema tu " basi akanipa stori za vikapanda vikashuka". Mara nyingi stori za "vikapanda vikashuka" zina sifa zifuatazo:

  a. Zinaanzia kwenye kitu cha kweli. Ili stori za "vikapanda vikashuka" zinoge ni lazima zianzie kwenye kitu cha kweli. Kwa mfano, kiongozi anaweza kuelezea tatizo la ajira kwa vijana, tatizo la barabara n.k Lengo la kuanzia na kitu cha kweli ambacho watu au mtu anatarajiwa kukijua ni kufanya yote yatakayosemwa baadaye yaonekane kama yana ukweli wa aina fulani hivi.

  b. Zinatengeneza mtandao mrefu wa kufanya jambo Sasa, stori za "vikapanda vikashuka" haziji hivi hivi na haziwezi kunoga kama zinaenda moja kwa moja kwenye hitimisho. Ili kumchosha msikilizaji na kumtega asiye mfikiriaji wa kutosha stori hizi huelezewa kwa kuongeza michakato mingi na mambo mengi. Watakuambia suala la leseni, hali ya uchumi, matatizo ya nguvu kazi, - kumbe swali lilikuwa ni "kwanini Tanzania ni Maskini"! Lengo kubwa ni kuficha hasa kitu ambacho kinahusiana na tatizo lenyewe. Kwa mfano, kwenye sakata la mafuriko watawala wetu walikuja na simulizi refu la "watu wanaoishi mabondeni". Sasa, walitumia hilo na kwa kina sana ili kuficha tatizo lenyewe hasa kwamba wameshindwa kuwa na sera nzuri ya ardhi, maji taka na maji ya mvua ambazo zimeshindwa kutekelezwa.

  c. Hutumia takwimu nyingi ambazo hata wakati mwingine hazihusiani na tatizo! Sasa watawala wanajua sana kutumia "takwimu" kuhalalisha jambo lolote lile. Kwa watu wanaojua kanuni ya takwimu wanasema kwamba "takwimu huweza kusema lolote lile". Bahati mbaya sana katika simulizi za "vikapanda vikashuka" takwimu hutumika kuficha ukweli kwa kutumia namba. Kwa mfano, kwenye mtihani wanaposema watoto waliofauliti ni asilimia 60 kati ya hawa tunaambiwa kuwa asilimia 80 wamechaguliwa kujiunga na shule za serikali. Sasa kwa haraka haraka mtu anaweza kufurahia takwimu kuwa asilimia "80" wamechaguliwa kwenda sekondari! Mtindo huu unatumika sana kuelezea ongezeko la shule, zahanati n.k ambapo utaona kuwa namba hutumiwa sana kuficha ukweli!

  d. Zinaanzia kwenye jambo moja na kuishia kwenye jingine kabisa
  Sasa kilele cha siasa za "vikapanda vikashuka" ni kuwa usipoangalia unaweza kujikuta unalazimisha kuzungumzia jambo jingine kabisa badala ya jambo la msingi. Fikiria kwa mfano suala la Katiba Mpya. Watawala wetu walifanikiwa kabisa kubadilisha mjadala baada ya kutufanya watu waamini kuwa wao ndio walikuwa na ajenda ya Katiba Mpya na kuwa njia yao ni bora zaidi. Watu wetu wengi wakasahau kabisa kuwa ni CCM hawa hawa waliokuwa wa kwanza kupiga vita tena kwa kejeli na dharau hoja ya Katiba Mpya! Lakini leo wamejitengeneza kuwa ni mashujaa wa Katiba Mpya!

  Kwa ufupi ni kuwa, unaposikiliza watawala wakizungumza au kujaribu kutetea uwe macho kutambua kuwa kwa kiasi kikubwa stori zao nyingi ni za "vikapanda vikashuka!". Watu wengine tulikuwa tunaita hizi kuwa ni "bla bla"! Uwe makini kuzitambua, kuzipuuza na wakati mwingine kuzikebehi na kuonesha jinsi gani stori hizo zinaweza kuwashawishi walio dhaifu kufikiri, na wale ambao ni goi goi wa kutumia chembe za ubongo walizojaliwa na Mwenyezi Mungu ili kufikiria! Swali ni inakuwaje kama mtu mzima anaamini, kukubali na kukumbatia masimulizi ya "vikapanda vikashuka"? MMM
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Viongozi wetu ni waigizaji na wananchi ni watazamaji. Mpaka sasa hivi watazamaji wamekubali maigizo yanayoendelea, wanapokea ujumbe wanaopewa bila maswali wala kuchuja. Hivyo hizo blah blah ni stahiki yetu, mpaka pale tutakapoamua kusimama kweli na kusema hatukubali kufanywa wajinga.
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ndiyo! tunaona hata Nape kijana mdogo kabisa kaanza na hayo mambo ya "vikapanda vikashuka",,leo anaweza sema hiki,,kesho anasema tofauti kabisa sambamba na kukana yale ya awali,mtu wa sampuli hii kesho akichukua madaraka ya nchi,,acha chama anachotumikia sasa obvious itakuwa ni tantalila tupu!
   
 4. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sioni kama kuna tofauti na lile tangazo la staa times, jinsi kaanumba "anavyojichekesha"! Uko sawa Lizzy.
   
 5. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Ndio maana tukawaita WASANII, uigizaji wa aina hiyo nayo ni fani, na wanasiasa wote wako hivyo!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Unajua nadhani watu wameanza kudh___arau kauli za wanasiasa na hasa viongozi.
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kuna member humu alizungumzia power from within.....

  yaani hiyo ikikosekana ndo unapata hii ya 'siasa za vikapanda vikashuka'
   
 8. F

  Froida JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280

  Kwa kweli ni vikapanda vikashuka hivi sasa Mawaziri na wabunge wa CCM wanapita kila mahara wanaeleza nini kuhusu katiba nasikia tu wakiwaasa wananchi wasiwasikilize viongozi wa upinzani Katiba itakuwa katibia
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ni vigumu sana hawa walaghai kufanikiwa kwa wananchi kama sie wenye uelewa tutatimiza majukumu yetu.
  Sie wenye uelewa ndio tunatakiwa kupita na kuwambia ukweli wananchi kila hawa wezi na matapeli wakipotosha mjadala wa katiba.
  Sisi tu wengi kuliko wao, hivyo tusilale bali tuendelee kusema na kusema na kusema na kusema bila uoga.
   
Loading...