Watatu wafariki baada ya kutumbukia mtoni Tarime

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Drj1.jpg
drj2.jpg

Watu watatu wamefariki dunia wilayani Tarime mkoani Mara kufuatia daraja la mto Msati uliopo katika barabara kuu ya Sirari - Mwanza kuvunjika na kisha kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani hapa.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Tarime/Rorya William Mkonda amesema kuwa tukio hilo lilitokea April 10, 2021 baada ya watu hao kupita katika daraja hilo pasipokujua kama tayari limekwisha vunjika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, William Mkonda amesema miili yote mitatu imekwishaopolewa kutoka mtoni na imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Tarime huku taratibu za kuitambua miili hiyo zikiendelea.

Amesema kuwa kufuatia daraja hilo kukata mawasiliano watumiaji wabarabara hiyo wanalazimika kupita Tarime Mjini ili kuingia na kutoka Sirari.

Kamanda Mkonda ameongeza kuwa tayari jitihada za kurejesha mawasiliano zinaendelea ambapo Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Mara Felix Ngaile pamoja na timu yake wako eneo la tukio kuhakikisha wanarejesha mawasiliano kwa haraka.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom