Watanzania Wote Bila Kujali Itikadi za Vyama...

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,506
Reaction score
123,777
Ndugu zetu Watanzania wote, bila kujali wewe upo chama kipi au hauna chama kabisa cha kisiasa.

CCM kama chama tawala tutapokea kero za wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa kuhusu maendeleo ya Tanzania katika sehemu uliyopo.

Uongozi wa CCM utazunguka nchi nzima bila kuchoka wala kusita kupokea kero na kuzitatua kwa kuzifanyia kazi papo kwa papo.

Tunapenda ieleweke kuwa CCM kama chama tawala hakitabagua Mtanzania kwa itikadi yake ya kisiasa.

Watanzania wote anzeni kujipanga na kuainisha kero zenu ambazo inabidi zifanyiwe kazi, usijali iwe kero kubwa au ndogo, CCM ipo kwa Watanzania wote bila kujali itikadi za kidini, kisiasa, kijinsia, kikabila wala kiumri.

Na wale wana JF wote mnaweza kutupia kero zenu hapa tuanze kuzifanyia kazi.

Tunataka kutimiza ahadi ya Rais ya #HapaKaziTu.
 
Hawachelewi kuomba Babu..................bahari afungulie!
 
Umeonge vyema dada!

1. Basi kwa kuanzia, ili CCM ionyeshe imekusudia hilo, iwaondoe vizuizini wale wote waliopo sero kutokana na mambo ya kisiasa hasa wa kipindi hiki cha uchaguzi!

2. Kinana na Nape, walizunguka nchi nzima katika kuimarisha chama na kusikiliza kero za wananchi, na rasilimali nyingi zilitumika! Je, zile alizokusanya Kinana zimefanyiwa kazi yeyote ambayo sisi wananchi tunaweza kukiri kuwa tunashudia hilo?
 
Jitahidi unaweza ukawa katibu mwenezi wa itikadi na kero za siasa nchini
 
Naamini kero kubwa now ya Watanzania ni 'tume huru ya uchaguzi'
mngeanza na hilo tu
 
Jitahidi unaweza ukawa katibu mwenezi wa itikadi na kero za siasa nchini

Sipo hapa kwa ajili ya kutafuta cheo, sina uchu wa madaraka kama teja fulani.
 
Umeonge vyema dada!

1. Basi kwa kuanzia, ili CCM ionyeshe imekusudia hilo, iwaondoe vizuizini wale wote waliopo sero kutokana na mambo ya kisiasa hasa wa kipindi hiki cha uchaguzi!

2. Kinana na Nape, walizunguka nchi nzima katika kuimarisha chama na kusikiliza kero za wananchi, na rasilimali nyingi zilitumika! Je, zile alizokusanya Kinana zimefanyiwa kazi yeyote ambayo sisi wananchi tunaweza kukiri kuwa tunashudia hilo?

1) Hakuna mfungwa kisiasa Tanzania.

2) Naam, kero za Kinana zimeanza kufanyiwa kazi papo kwa papo, sasa ni muendelezo na tunaainisha hapa kuwa tutatatua kero za Wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama.

Tanzania ni moja.
 
Kwani mgombea aliyeshinda katimiza ahadi zake?

Mwambieni atimize kwanza ule msururu wa ahadi kabla hajaanza kuparamia mengineyo mapya...
 
Ndugu zetu Watanzania wote, bila kujali wewe upo chama kipi au hauna chama kabisa cha kisiasa.

CCM kama chama tawala tutapokea kero za wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa kuhusu maendeleo ya Tanzania katika sehemu uliyopo.

Uongozi wa CCM utazunguka nchi nzima bila kuchoka wala kusita kupokea kero na kuzitatua kwa kuzifanyia kazi papo kwa papo.

Tunapenda ieleweke kuwa CCM kama chama tawala hakitabagua Mtanzania kwa itikadi yake ya kisiasa.

Watanzania wote anzeni kujipanga na kuainisha kero zenu ambazo inabidi zifanyiwe kazi, usijali iwe kero kubwa au ndogo, CCM ipo kwa Watanzania wote bila kujali itikadi za kidini, kisiasa, kijinsia, kikabila wala kiumri.

Na wale wana JF wote mnaweza kutupia kero zenu hapa tuanze kuzifanyia kazi.

Tunataka kutimiza ahadi ya Rais ya #HapaKaziTu.

Hatutaki kila mtu aishi kivyake i desire maisha yawe magumu kuliko hapa
 
Huenda wewe ndiye mnafiki namba moja aliokuwa anawasema Magufuli jana.
Mbali na hapo ni kugombania madaraka kwa kutumia bilioni nyingi bila kujua mnachotaka kukifanya ikiwa ni pamoja na kujua mahitaji ya umma!
 
Dah... Mara tume ni huru. Hakuna mfungwa wa kisiasa.... Khaaaa. Wapi Green cards... Sio za chama... Za uraia Marekani. Maana kuwa Mtz mh...
 
Nyinyi endeleeni tu kutawala, sisi hatuna shida wa kero yeyote! Tumeridhika na haya maisha yetu, nyinyi tawaleni tu. Hamna shida!! Shida yetu kubwa ilikua tupate UHURU, sasa huo uhuru hauwezekani tena! Tawaleni tu! Tawaleni Tu! Tawaleni Tu! tawaleni tu! tawaleni tu! tawaleni tu! tawaleni tu! sisi ni watumwa wenu.
 
Kwani mgombea aliyeshinda katimiza ahadi zake?

Mwambieni atimize kwanza ule msururu wa ahadi kabla hajaanza kuparamia mengineyo mapya...
Aanze na 50bil per village!!! Then na Laptop kwa kila Mwalimu.
 
1) Hakuna mfungwa kisiasa Tanzania.

2) Naam, kero za Kinana zimeanza kufanyiwa kazi papo kwa papo, sasa ni muendelezo na tunaainisha hapa kuwa tutatatua kero za Wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama.

Tanzania ni moja.

Swali au swala langu ni kuwa, kuna watu wapo ndani au wana makosa yaliotokana na issue za uchaguzi huu ulioisha, sasa ili kuurudihsa umoja wa Tanzania moja, je hamuoni kuna haja ya kuwasamehe na kuwaachilia huru?
 
Back
Top Bottom