Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,519
- 41,030
Nimeona wengi kwa mihemuko ya umbumbumbu wa kutojua taratibu na sheria zilizopo, wamekuwa wakimlaumu Rais kwa kutochukua hatua mara moja dhidi ya waliotajwa kwenye Report ya CAG.
Watu hao walitarajia baada tu ya report ya CAG, kesho yake Rais afukuze wale wote ambao ofisi zao zimehusishwa ama na upotevu, matumizi mabaya, matumizi hewa au matumizi yasiyofuata taratibu.
Watu hawa wasichojua ni kwa kwamba, kufuatana na taratibu zilizopo za kikatiba na sheria, hawa maofisa ambao ofisi zao zimetajwa na ofisi ya CAG ni lazima waitwe na kuhojiwa na kamati ya Bunge. Ukiwafukuza mapema kwa taarifa tu ya CAG bila ya wao kupewa nafasi au ya kujitetea au kutoa ufafanuzi, hiyo kamati ya Bunge itamhoji nani?
Kumbuka, kamati ya Bunge uwezo wake wa kikatiba kuhusiana na report ya CAG, unaishia kwa wale ambao ni watendaji wa Serikali, na siyo mwananchi ambaye yupo mtaani.
Mambo yale ya overinvoicing, hayapo kwenye report ya CAG. Yale yanaweza kufanyiwa kazi na Rais kwa taratibu zilizopo, lakini Rais hawezi kuanza kuchukua hatua mara moja kwa ofisi zilizotajwa na CAG.
Ikumbukwe kwenye report ya CAG, kuna upotevu, matumizi mabaya, ubadhirifu, kutofuata taratibu, matumizi hewa, n.k. Na hayo yanahusishwa na ofisi, report haitaji mtu specific.
Nadhani baada ya Bunge, kitakachofuatia, ni kuwatambua wahusika wa moja kwa moja. Na hao wahusika itabidi makosa yao yatambulike bayana. Kama ni uzembe, uwezo mdogo au kutojali, huyo kama mimi nikiwa ndiyo ofisi ya uteuze au mwajiri, nafukuza mara moja.
Kama ni wizi, huyo ni kumkabidhi kwa Polisi ili afikishwe mahakamani. Kama ni kutokana na maumuzi yenye uwezekano wa msukumo wa rushwa (kwa mfano utoaji wa tenda zenye gharama kubwa kuliko uhalisia wa gharama), huyu kabidhi kwa TAKUKURU, achunguzwe halafu afikishwe mahakamani.
Japo ni dhahiri tuna Bunge ambalo siyo la wananchi, ni la watu waliopachikwa na mtu mmoja kutoka chama kimoja kwa mapenzi yake, hatuna namna, yatubidi tusubiri.
Hatutegemei makubwa toka Bungeni maana hata hao wabunge wenyewe ni zao la uovu, na wengi wao upeo wao ni mdogo, uadilifu wao ni wa mashaka makubwa, labda pengine mmoja mmoja atajitutumua na kuitafuta hekima.
Ingawa mara nyingi mtu akiwa mwovu, kama walivyo hawa wabunge wengi ambao ni watoa rushwa, wevi wa kura, n.k, dhamira inakosa ujasiri dhidi ya waovu wenzao. Ni nadra sana jambazi akachukua jiwe kumpiga jambazi mwingine, japo kuna wakati anaweza kujitutumua ili kujikosha mbele ya watu wema ili naye aonekane ni mtu mwema.
Tusubiri, hatua zote zipite ili tupate uhalali wa kumlaumu Rais, kama amechukua hatua au hapana.