Watanzania wengi ni Ignorant

Watanzania wengi ni Ignorant

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,563
Reaction score
7,321
Kabla ya kuanza tuangalie nini maana ya Ignorant ni mtu anayekosa ujuzi, taarifa, uelewa au ufahamu kuhusu jambo fulani — hasa pale ambapo jambo hilo linatarajiwa kwa kawaida liwe linafhamika au mtu awe na maarifa juu ya mambo hayo. Ignorant kwa Kiswahili tunaweza kusema Mtu asiye na maarifa (mjinga)

Unamwambia mtu kwamba tumekosa fursa fulani kama nchi, yeye anakwambia "inatusaidia nini hiyo fursa" au anasema kwani "ikitupita ndio tunakufa?". Ukiangalia kwa juu unaweza kuhisi katoa mawazo ya kawaida tu, lakini ukifuatilia unakuta mtu huyo ni Ignorant.

Juzi kabla ya IShowSpeed ajaanza ziara yake Afrika, niliandika uzi humu nikasema tumekosa fursa ya Nchi kutangazwa bure kimataifa kupitia Streamer huyo. Watu wakaja na kutoa povu kuwa Kutembelea kwakwe Afrika kunasaidia nini, mara kutabadilisha nini, mara kwani ni lazima atembelee Tanzania. Watu walikuja na Negativity, wakasahau ukubwa wa jambo unafaida gani kwa Nchi husika.

Juzi nimeona Mpaka Rais wa Kenya Bwana William Ruto akituma salamu za kumkaribisha IShowSpeed Kenya. Kibongo bongo watu wangeanza kuweka Siasa, mara mabeberu wanatuonea wivu mara sijui ujinga gani, na ndio maana kwa Afrika Mashariki sasa Rwanda naye amechukua nafasi yetu katika kuvutia wawekezaji. Fursa kama hizi Tanzania kwanza uanza kupigwa vita na watanzania, kisha wanasiasa uingia kati na mwishowe fursa zinapotea. Nchi inabaki gizani kama neno Tanzagiza

Ebu tuangalie faida za huyu IShowSpeed kutembelea Afrika

🌍 1. Kuongeza Kujulikana kwa kina kwa Afrika Ulimwenguni


Faida kuu ya moja kwa moja:
Tour hii inafanyika katika mataifa ya Afrika kutoka maeneo ya ndani kabisa kwenda kwenye macho ya dunia kupitia mamilioni ya watazamaji kila siku kwenye livestream.

Jamaa anaonyesha miji, tamaduni, chakula, vivutio vya kitalii na maisha ya kila siku kwa njia isiyo ya kawaida ya broadcast ya kawaida. Ambapo watalii wengine uchafua au kupaka rangi mambo kuongeza uongo.

Inatoa taswira mpya ya Afrika — sio tu hadithi ya kitendawili cha “continent that needs saving,” bali ukarimu, nguvu ya vijana na utofauti wa tamaduni.

👉 Hii ni branding ya bara zima kwa milango ya utalii, biashara na diaspora kuona thamani halisi ya bara letu.



💰 2. Tourism & Brand Africa – Soko Lisilo Tajwa


Tour hii si tamasha tu; ni kampeni kubwa ya marketing

Katika nchi kama Kenya, ushawishi wa livestream uliwaleta pamoja watalii, serikali na biashara kutangaza “Magical Kenya” miaka ya nyuma na ofcourse walivutia watalii wengi mpaka leo kwa ukanda huu kenya haishikiki kwa watalii— basi pia kupitia IShowSpeed fursa nyingi pia zitafunguka.

Watu wanaona picha halisi ya mbuga, maisha ya jiji, majumba ya kihistoria na maisha ya kila siku. Hii ni fursa kubwa ya kupata watalii zaidi na mapato ya kigeni kwa nchi zinazotembelewa.


📌 Kwa nchi ambazo hazijawahi kushiriki linapokuja suala la marketing ya utalii, hii ni free global exposure isiyopimika kwa gharama ya jadi ya matangazo yani matangazo sawa na bure. Kuliko nchi ingekodi kampuni ya kutangaza utalii kwa mabilioni ya pesa kama hile "Tour ya Mama Samia" inaitwa Royal Tour


📱 3. Kuongeza Fursa kwa watumiaji wa Mitandao ya Kijamii

Tour ya Speed ina uwezo mkubwa wa kukuza wabunifu wa Afrika (Exposure)

Kwa kushirikiana na wasanii, vloggers wa ndani na micro-influencers, nchi hizi zinapata networking, pia kuona na kushirikiana kwa content creators wa kimataifa. Mfano content creator wa Tanzania "Buse Boi" ilibidi aende Rwanda kukutana na IShowSpeed na akapata fursa ya kuzungumza na manager wa wake.

Maeneo kama Lusaka, Harare na Nairobi yameonekana kwenye maelfu ya video , huku zikivutia watazamaji wageni waliosubiri kuona maisha ya Afrika si dhahiri tu kwenye matangazo ya nje kwenye TV za wazungu kama CNN.


📈 4. Kuongeza Kujivunia Kitaifa na Utamaduni

Tayari imeonekana kwamba watu wa ndani ya bara la Afrika wana hisia chanya, ni watu wanaopenda wageni, na fursa mpya huku wakijivunia tamaduni zao.


📊 5. Kuibua Mawazo Mapya ya Biashara kwa Wachanga

Hii ni fursa ya kipekee ya kugundua fursa za kibiashara zinazohusiana na:

Utalii wa kidijitali kama digital travel guides

Uuzaji wa bidhaa za kienyeji kupitia livestream

Huduma za IT/Connectivity kwa streamers wa Afrika

Brand partnerships kati ya wabunifu wa Afrika na mabarani



🔍 6. Kubadilisha Hadithi na Kupinga Stereotypes

Katika nyakati nyingi, Afrika huonekana kupitia macho ya media ya nje kama sehemu ya changamoto, vita na migogoro — tour hii ikionyesha maisha halisi inachukua jukumu la cultural diplomacy, ambapo:

Ulimwengu unaona Afrika kwa macho mapya ya matumaini na uhai.

Inapunguza mapokeo potofu ya bara hilo.
 
Unatukosea sana watanzania kutuita Ignorant kisa mtoto wa ellfu ✌️. Acha umaku
Wewe ni Ignorant wa kwanza

Punguza ku-judge vitu kwa kuangalia umri... wewe na umri wako wa kizee umefanya nini cha maana

Kazi kututengenezea pseudo accounts humu JamiiForums
 
Back
Top Bottom