Watanzania wengi hasa vijana wanataka bora mabadiliko

Watanzania wengi hasa vijana wanataka bora mabadiliko

Swadakta mkuu daffy, ushabiki umetawala bila kuwa na hoja za msingi kwa anachoki sapoti mtu. Hili ni tatizo na linaweza kutugharimu baadaye
Gharama za CCM toka ianza kututawala 1977 ni kubwa kuliko gharama za kuitoa madarakani, Trust me.
 
Great thinkers heshima kwenu. Watanzania ikiwa zimebaki takriban siku 11 kufanya maamuzi ya hatima ya maisha yetu kwa miaka mitano au zaidi ijayo, kuna jambo muhimu sana nimeligundua ktk mtazamo wangu kwa siku kadhaa ambazo nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa hali ya kisiasa/kampeni inayoendelea hivi sasa.

Nimegundua kwamba kwa sasa Watanzania tulio wengi hasa vijana, tunahitaji mabadiliko. Hili ni jambo muhimu sana kwa mustakabali wa maisha yetu na vizazi vijavyo.

Kinachonipa shaka mimi ni kimoja tu, nacho ni; je kwa mhemuko huu wa vijana na wazee wachache wa kuhitaji mabadiliko bila kujali ni MABADILIKO BORA au BORA MABADILIKO tunakoelekea ni kuzuri??? Nasema vijana wanataka bora mabadiliko kwa sababu hawaangalii rekodi za utendaji wa mtu, uadilifu, umadhubuti wa mtu, sera zake/za chama anazozinadi n.k, bali wanachotaka ni kuondoa chama fulani na kuweka kingine tu. Kwa mtazamo wangu haya ndo mabadiliko wanayotaka vijana wengi.

Hii inanipa shaka mimi kwa sababu kweli tunaweza kufanya mabadiliko ya chama/mfumo lakini bila kuangalia ni nani tunaowapa dhamana ya hatima ya maisha yetu??? Je, hawa watu/mtu ana rekodi gani zinazotupa imani ya kumkabidhi dhamana kubwa kiasi hiki? Hatuangalii je, huyu tunayempa dhamana kubwa alipopewa dhamana ndogo alitenda haki au uadilifu?

Mimi kama mtanzania, nawashauri wenzangu hasa vijana tutafakari kwa kina kabla ya kuamua ni mabadiliko gani tunayoyataka ili baadaye tusije tukalia kilio cha kusaga meno kwa maamuzi ya pupa na ya ghadhabu.

Karibuni wadau wenzangu, tujadili kwa hoja bila hasira.

Kimsingi kwasasa kama nchi sioni kama tunacha kupoteza kuchagua ukawa au ccm, lkn ni bora zaidi kuchagua ukawa kwasababu hawa wameshindwa kwa mda wote tulio waamini.
Pili tunajenga msingi kwa watu wasio jitambua kuwa maisha bila ccm yanawezekana, na tukiweza hili baadae tutapata viongozi wazr kutoka chama chochote kwa wakati huo.
 
Ni kweli kabisa, katiba ndiyo muongozo ambao kiongozi yeyote ataufuata. Naamini hayo ndo yatakuwa mabadiliko ya kweli na ni Bora. Vinginevyo tutapeana ahadi zenye ladha na harufu nzuri, lkn mwisho wa siku hazitekelezwi kwa sababu huna pa kumshitaki kwa kuwa katiba haitoi fursa hiyo

Lakini pia ukumbuke wale wale walioipinga rasimu ya warioba, na kutengeneza ilani ya sisiem ndio hao hao Leo Wako upingazani tunawashangilia waingie madarakani, Je unadhani wataikubali hoyo rasimu hali kwamba warioba anawaponda majukwaani?
 
vijana wengi wanataka serikali iwawekee chakula mdomoni na kijiko.

Hayo ni maneno yako kama wewe wazazi wako walipata neema ukaweza kuwezeshwa hata mtaji ukajiajiri huwezi kuichukia serikali ila hamu ya vijana ni serikali kuweka mfumo rafiki ambao utawezesha vijana kupata kazi mfano idara ya kilimo pembejeo zingekuwa wanakopeshwa angalau baada ya miaka 4wanaanza kulipa .ukija viwanda vimekufa wakati vingesaidia kutoa ajira .mfano tu wachina wakija hata kujenga barabara wanakuja na vibarua wao iyo ni haki inch I hii imekuwa na matabaka yalopitiliza ukienda kwenye huduma za afya ni janga kama mzazi wako kapuku utafia benchi Mimi niliwahi kaenda muhimbili niko vibaya nikaambiwa doctor yuko nafoleni so niweke bed rest adi nitakapo pangiwa bt bro Wangu alipo wahonga doctor alipata nafasi sa hiyo maisha gani BT haikusaidia wakaesema vifaa vyakufanyia vipimo vibovu ikabidi tuhame hospital kufika aghakan docta alotelekeza wagonjwa yuko kule sasa iyo serikali ndo ckivu kweli
 
Mary, wanaofanya vizuri kwa juhudi zao ni wengi kuliko wale wanaosaidia, na sio wazazi tu hata mabenki yanasaidia watu na wengi ya hawa watu hawalalamiki.

Viwanda vimekufa sababu kubwa ni Ujamaa, kama isingekuwa na haya mambo ya ujamaa Viwanda karibia 80% vilivyofungwa visingefungwa, ninaweza kutumia muda sana kuelezea hili lakini tatizo ni ujamaa.

kuhusu Wachina, ni kwamba cha muhimu kutoka kwa watu wa nje ni kodi, ila kuwavutia inabidi kuwaruhusu wawe na uhuru fulani na kuleta watu wao inaeleweka kabisa.

kuhusu rushwa hospitalini, sidhani kama ni tatizo la serikali, wanao haribu na kufanya maskini waumie ni pale wenye pesa na wasio na pesa kukosa uvumilivu na kununua haki, mtu anaona ni bora ampe daktari pesa ili mgonjwa wake atibiwe kwanza, sasa huyu daktari akiona hivyo ndio inakuwa tabia. kwahiyo ni shida inayoanzishwa na wananchi wenyewe.
 
Tunataka mabadiliko yatakayoitoa ccm madarakani hata kama mtayaita bora mabadiliko. Tunataka serikali bora sio bora serikali.
 
Great thinkers heshima kwenu. Watanzania ikiwa zimebaki takriban siku 11 kufanya maamuzi ya hatima ya maisha yetu kwa miaka mitano au zaidi ijayo, kuna jambo muhimu sana nimeligundua ktk mtazamo wangu kwa siku kadhaa ambazo nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa hali ya kisiasa/kampeni inayoendelea hivi sasa.

Nimegundua kwamba kwa sasa Watanzania tulio wengi hasa vijana, tunahitaji mabadiliko. Hili ni jambo muhimu sana kwa mustakabali wa maisha yetu na vizazi vijavyo.

Kinachonipa shaka mimi ni kimoja tu, nacho ni; je kwa mhemuko huu wa vijana na wazee wachache wa kuhitaji mabadiliko bila kujali ni MABADILIKO BORA au BORA MABADILIKO tunakoelekea ni kuzuri??? Nasema vijana wanataka bora mabadiliko kwa sababu hawaangalii rekodi za utendaji wa mtu, uadilifu, umadhubuti wa mtu, sera zake/za chama anazozinadi n.k, bali wanachotaka ni kuondoa chama fulani na kuweka kingine tu. Kwa mtazamo wangu haya ndo mabadiliko wanayotaka vijana wengi.

Hii inanipa shaka mimi kwa sababu kweli tunaweza kufanya mabadiliko ya chama/mfumo lakini bila kuangalia ni nani tunaowapa dhamana ya hatima ya maisha yetu??? Je, hawa watu/mtu ana rekodi gani zinazotupa imani ya kumkabidhi dhamana kubwa kiasi hiki? Hatuangalii je, huyu tunayempa dhamana kubwa alipopewa dhamana ndogo alitenda haki au uadilifu?

Mimi kama mtanzania, nawashauri wenzangu hasa vijana tutafakari kwa kina kabla ya kuamua ni mabadiliko gani tunayoyataka ili baadaye tusije tukalia kilio cha kusaga meno kwa maamuzi ya pupa na ya ghadhabu.

Karibuni wadau wenzangu, tujadili kwa hoja bila hasira.

Kama ni kilio cha kusaga meno tumekichoka, ccm imetusagisha meno sana ni muda sasa wa fisccm kupita hivi
 
Lowasa atosha na babu kingunge jana mwanza alithibitisha
 
Maji .Umeme.Muhimbili hovyo.daladala shida.mfumuko WA bei.police rushwa.nataka mabadiliko ya chama.
 
Umetoa maoni yako na umesikika, kitu kidogo tu lakini muhimu sana kinakupunguzia credibility ya maoni yako, ni MATUSI. Bahati nzuri kiswahili ni tajiri sana katika maneno. Kuna maneno mengi sana ungeweza kutumia na kueleweka bila kuweka tusi/neno lenye kuvunja heshima. Hongera kwa mabadiliko, na nakuhimiza kwenda kupiga kura tarehe ikifika ili utimize ndoto yako na utumie haki yako ya kikatiba

Taja matusi niliyotukana, sidhani kama wewe unaweza kunihimiza kwenda kupiga kura wakati suala hilo nalijua bila kufuata ushauri wako.
 
Maji .Umeme.Muhimbili hovyo.daladala shida.mfumuko WA bei.police rushwa.nataka mabadiliko ya chama.

Sababu unazo na bila shaka nia pia unayo. Swali, je unauhakika upande unaoutaka utaweza kuleta neema juu ya matatizo yanayokukera???
 
Midfield Midfield Midfield. Unapokuwa unakufa maji unataka nani akuokoe. Utataka aje mtu wa Navy ili uokolewe? Akija bibi kizee lakini ni life guard mzuri tu na anaweza kukuokoa huku bubbles zikitokea puani na macho yamekutoka ukisubiri pumzi ya mwisho ukate roho unajali nani anakuokoa? Utasema sitaki nasubiria mwanajeshi mwanamaji!!??

Huo msemo wa Nyerere mnautumia kijinga kwa elimu hizi za CCM za shule zisizo na waalimu. Kuhusu kuokolewa ni kuokolewa tu hakunaga kuokolewa bora.

Pata fundisho kidogo;

Kwenye wokovu - bora kuokolewa kuliko kusubiri kuokolewa bora..utakufa we mjinga

Kuhusu ajira - wakati mwingine tunaanza na bora ajira halafu kwa kujituma unapata ajira bora.

Bora mabadiliko kwanza CCM itoke halafu tutapata mabadiliko bora.

Labda hujawahi kupitia hali tete maishani. Ndipo utagundua kuwa wakati mwingine hilo neno bora halichagui upande wa unachokitaka kwamba ni kushoto au kulia.

Kama wewe ni mkristo nadhani umewahi kutembelea mji wa biblia na kumsikia Yesu akisema ni aheri kuingia mji mpya na nchi mpya ukiwa huna kiungo chako kuliko kuwa mzima na viungo vyote halafu ukatupwa motoni. Yaani hapo Yesu anawaambia wakristo bora uzima ni better kuliko kuukosa uzima. Sasa wewe unataka uzima bora!!!?

Msikariri tu falsafa bila kuangalia 'practicability'.

Nahitimisha kuwa hii mada haina maana.
 
Yaite utakavyo as long as it helps us ditch this sh*t so called ccm we don't give a damn f*ck.
 
Back
Top Bottom