Watanzania wengi hasa vijana wanataka bora mabadiliko

MIDFIELD

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2013
Posts
1,944
Reaction score
703
Great thinkers heshima kwenu. Watanzania ikiwa zimebaki takriban siku 11 kufanya maamuzi ya hatima ya maisha yetu kwa miaka mitano au zaidi ijayo, kuna jambo muhimu sana nimeligundua ktk mtazamo wangu kwa siku kadhaa ambazo nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa hali ya kisiasa/kampeni inayoendelea hivi sasa.

Nimegundua kwamba kwa sasa Watanzania tulio wengi hasa vijana, tunahitaji mabadiliko. Hili ni jambo muhimu sana kwa mustakabali wa maisha yetu na vizazi vijavyo.

Kinachonipa shaka mimi ni kimoja tu, nacho ni; je kwa mhemuko huu wa vijana na wazee wachache wa kuhitaji mabadiliko bila kujali ni MABADILIKO BORA au BORA MABADILIKO tunakoelekea ni kuzuri??? Nasema vijana wanataka bora mabadiliko kwa sababu hawaangalii rekodi za utendaji wa mtu, uadilifu, umadhubuti wa mtu, sera zake/za chama anazozinadi n.k, bali wanachotaka ni kuondoa chama fulani na kuweka kingine tu. Kwa mtazamo wangu haya ndo mabadiliko wanayotaka vijana wengi.

Hii inanipa shaka mimi kwa sababu kweli tunaweza kufanya mabadiliko ya chama/mfumo lakini bila kuangalia ni nani tunaowapa dhamana ya hatima ya maisha yetu??? Je, hawa watu/mtu ana rekodi gani zinazotupa imani ya kumkabidhi dhamana kubwa kiasi hiki? Hatuangalii je, huyu tunayempa dhamana kubwa alipopewa dhamana ndogo alitenda haki au uadilifu?

Mimi kama mtanzania, nawashauri wenzangu hasa vijana tutafakari kwa kina kabla ya kuamua ni mabadiliko gani tunayoyataka ili baadaye tusije tukalia kilio cha kusaga meno kwa maamuzi ya pupa na ya ghadhabu.

Karibuni wadau wenzangu, tujadili kwa hoja bila hasira.
 
....nimetafakari miaka Zaidi ya hamsini....itakua rasi kuanya tena mabadiliko 2020 baada ya kuwa ba katiba tunayoitaka sisi wananchi.....whether mabadiko yatakuwa mabaya au la. Faida ys mabadilko kwangu ni Katiba mpya end of story.
 
Ni kweli kabisa, katiba ndiyo muongozo ambao kiongozi yeyote ataufuata. Naamini hayo ndo yatakuwa mabadiliko ya kweli na ni Bora. Vinginevyo tutapeana ahadi zenye ladha na harufu nzuri, lkn mwisho wa siku hazitekelezwi kwa sababu huna pa kumshitaki kwa kuwa katiba haitoi fursa hiyo
 
Yes tafakuri unayoitaka itatupotezea muda.Jambo la maana kwasasa tufanye mabadiliko yawe mazuri au mabaya.kwa vyevyote vile mifumo mibovu ya CCM itasambaratika.Let say watakaoingia hawafai,mwaka 2020 tutakuwa na uchaguzi mzuri wa vyama vingi vikihusisha a new CCM.
 
Great thinkers heshima kwenu. Watanzania ikiwa zimebaki takriban siku 11 kufanya maamuzi ya hatima ya maisha yetu kwa miaka mitano au zaidi ijayo, kuna jambo muhimu sana nimeligundua ktk mtazamo wangu kwa siku kadhaa ambazo nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa hali ya kisiasa/kampeni inayoendelea hivi sasa.

Nimegundua kwamba kwa sasa Watanzania tulio wengi hasa vijana, tunahitaji mabadiliko. Hili ni jambo muhimu sana kwa mustakabali wa maisha yetu na vizazi vijavyo.

Kinachonipa shaka mimi ni kimoja tu, nacho ni; je kwa mhemuko huu wa vijana na wazee wachache wa kuhitaji mabadiliko bila kujali ni MABADILIKO BORA au BORA MABADILIKO tunakoelekea ni kuzuri??? Nasema vijana wanataka bora mabadiliko kwa sababu hawaangalii rekodi za utendaji wa mtu, uadilifu, umadhubuti wa mtu, sera zake/za chama anazozinadi n.k, bali wanachotaka ni kuondoa chama fulani na kuweka kingine tu. Kwa mtazamo wangu haya ndo mabadiliko wanayotaka vijana wengi.

Hii inanipa shaka mimi kwa sababu kweli tunaweza kufanya mabadiliko ya chama/mfumo lakini bila kuangalia ni nani tunaowapa dhamana ya hatima ya maisha yetu??? Je, hawa watu/mtu ana rekodi gani zinazotupa imani ya kumkabidhi dhamana kubwa kiasi hiki? Hatuangalii je, huyu tunayempa dhamana kubwa alipopewa dhamana ndogo alitenda haki au uadilifu?

Mimi kama mtanzania, nawashauri wenzangu hasa vijana tutafakari kwa kina kabla ya kuamua ni mabadiliko gani tunayoyataka ili baadaye tusije tukalia kilio cha kusaga meno kwa maamuzi ya pupa na ya ghadhabu.

Karibuni wadau wenzangu, tujadili kwa hoja bila hasira.

Mlipewa nafasi ya kuleta mabadiliko kwa kupitia katiba mpya, mlichokifanya ndio leo hii kimegeuka ghadabu dhidi yenu. Na kwa taarifa yako tayari tuliyataka mabadiliko bila hata huyo Lowassa. Nadhani ulifuatilia jinsi watu tulivyojiandikisha kwa shida bila kujali tunaamka saa ngapi. Na kujiandikisha kule lengo letu lilikuwa ni kuitoa ccm, kumbuka huyo EL alikuwa hajaja upinzani, na wala usidhani tunababaika na Lowassa bali Lowassa alichofanya ni kudandia gari la mabadiliko na kwa bahati nzuri au mbaya akapewa usukani. Sasa nyie mkidhani watu tunababaika na Lowassa mnajidanga tu, hapa ccm ilipotufikisha hata Godbless Lema angekuwa mgombea wa urais bado tungempigia kura za kishindo. Kwa hiyo unapotuletea porojo sijui za mabadiliko bora hayo unayesema wewe, kilichowashinda kufuata maoni ya wananchi kupitia rasimu ya Warioba ni nini leo muamue kutujia na maelezo ya kijinga kama hayo yako.

Wewe kajiandae na wenzio kuingiza nchi machafukoni kwa kugomea maamuzi ya wananchi kwa njia ya kura kama jinsi mlivyopuuza maoni yao kwenye katiba mpya. Kumbuka tulitaka katika maoni ya katiba mpya uwakilishi wa ubunge tulitaka mwisho uwe miaka kumi, haturuhusu kiongozi awe ana account nje ya nchi, tulitaka madaraka ya rais yapunguzwe lakini nyinyi ccm mlijifanya kuzuia yale mabadiliko, iweje wewe leo ujifanye utaleta mabadiliko wakati mliyapinga kwa nguvu zenu zote? Tunaomba tuheshimiane samahani, wananchi tumeshaamua lazima tuwaondoe mkajifunze kuheshimu matwaka ya wananchi na sio ya chama, mkirudi baadae ulevi wa madaraka utakuwa umepungua.
 
Ahsante kwa maoni yako..nachelea kusema machache sana juu ya fikra zako uizoziwasilisha hapa jukwaani. Kwa kifupi na wewe mtoa mada hufahamu unataka mabadiliko gani pia ama hujui tubadilishe nini hasa. Tukifuata propaganda za wanasiasa wote wa upinzani na chama tawala hutajua mabadiliko uyatakayo. Ukifuatilia utendaji wa wagombea utajua mabadiliko gani unayoyazungumzia..lakini ukifuata mkumbo basi hautakuja kufahamu ni mabadiliko gani hasa yanayozungumziwa.

Kwa ufupi ushatoa mada well done..lakini amua sasa vijana wahemkwe kubadili mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya au chupa ya zaman waweke mvinyo mpya. Kumbuka vijana huemkwa kutokana na kuhemshwa na mihemsho ya mambo mengi yanayowahemsha (maisha yao asilia)..ushatafakari hilo???? Na kama huishi maisha yao basi ni rahisi kuwashangaa wanavyohemkwa na wale mnaoishi maisha yanayofanana wataungana na wewe kuwashangaa vijana na wazee..because people we differ..mwiba usiokuchoma hauumi kamwe..
 
Very Clear to the point! Hili ni jibu la MWAKA na la kufungia kampeni KUDOS Tindo. You need say no more. Wanafunzi mashuleni mkiulizwa definition ya Mabadliko yanayozungumzwa na UKAWA ndio hiyo. Very good sum up!
 
Great thinkers heshima kwenu. Watanzania ikiwa zimebaki takriban siku 11 kufanya maamuzi ya hatima ya maisha yetu kwa miaka mitano au zaidi ijayo, kuna jambo muhimu sana nimeligundua ktk mtazamo wangu kwa siku kadhaa ambazo nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa hali ya kisiasa/kampeni inayoendelea hivi sasa.

Nimegundua kwamba kwa sasa Watanzania tulio wengi hasa vijana, tunahitaji mabadiliko. Hili ni jambo muhimu sana kwa mustakabali wa maisha yetu na vizazi vijavyo.

Kinachonipa shaka mimi ni kimoja tu, nacho ni; je kwa mhemuko huu wa vijana na wazee wachache wa kuhitaji mabadiliko bila kujali ni MABADILIKO BORA au BORA MABADILIKO tunakoelekea ni kuzuri??? Nasema vijana wanataka bora mabadiliko kwa sababu hawaangalii rekodi za utendaji wa mtu, uadilifu, umadhubuti wa mtu, sera zake/za chama anazozinadi n.k, bali wanachotaka ni kuondoa chama fulani na kuweka kingine tu. Kwa mtazamo wangu haya ndo mabadiliko wanayotaka vijana wengi.

Hii inanipa shaka mimi kwa sababu kweli tunaweza kufanya mabadiliko ya chama/mfumo lakini bila kuangalia ni nani tunaowapa dhamana ya hatima ya maisha yetu??? Je, hawa watu/mtu ana rekodi gani zinazotupa imani ya kumkabidhi dhamana kubwa kiasi hiki? Hatuangalii je, huyu tunayempa dhamana kubwa alipopewa dhamana ndogo alitenda haki au uadilifu?

Mimi kama mtanzania, nawashauri wenzangu hasa vijana tutafakari kwa kina kabla ya kuamua ni mabadiliko gani tunayoyataka ili baadaye tusije tukalia kilio cha kusaga meno kwa maamuzi ya pupa na ya ghadhabu.

Karibuni wadau wenzangu, tujadili kwa hoja bila hasira.
Umenena vema sana,japo najua vijana Wengi hawafikiri kama wewe,kinachoendelea kwa sasa ni ushabiki .
 
To a uozo wako hapa, we umejua magufuli ataletamabadiliko yyaliyo bora? Ni nani aijuaye kesho? Ccm imembeba magufuli na ni ccm hiyohiyo tumeipa chance miaka mingi imeshindwa kudeliver quality services sasa tuache tubadili mfumo, ndo tutajifunza kwani Chadema si watz kama sisi? Iweje ccm mjione mna haki milki ya utawala? Never never never ccm again, wametudharau sana nikikumbuka bunge LA lescrow na lile la katiba natamani trh 25 iwe kesho.
 
Mlipewa nafasi ya kuleta mabadiliko kwa kupitia katiba mpya, mlichokifanya ndio leo hii kimegeuka ghadabu dhidi yenu. Na kwa taarifa yako tayari tuliyataka mabadiliko bila hata huyo Lowassa. Nadhani ulifuatilia jinsi watu tulivyojiandikisha kwa shida bila kujali tunaamka saa ngapi. Na kujiandikisha kule lengo letu lilikuwa ni kuitoa ccm, kumbuka huyo EL alikuwa hajaja upinzani, na wala usidhani tunababaika na Lowassa bali Lowassa alichofanya ni kudandia gari la mabadiliko na kwa bahati nzuri au mbaya akapewa usukani. Sasa nyie mkidhani watu tunababaika na Lowassa mnajidanga tu, hapa ccm ilipotufikisha hata Godbless Lema angekuwa mgombea wa urais bado tungempigia kura za kishindo. Kwa hiyo unapotuletea porojo sijui za mabadiliko bora hayo unayesema wewe, kilichowashinda kufuata maoni ya wananchi kupitia rasimu ya Warioba ni nini leo muamue kutujia na maelezo ya kijinga kama hayo yako.

Wewe kajiandae na wenzio kuingiza nchi machafukoni kwa kugomea maamuzi ya wananchi kwa njia ya kura kama jinsi mlivyopuuza maoni yao kwenye katiba mpya. Kumbuka tulitaka katika maoni ya katiba mpya uwakilishi wa ubunge tulitaka mwisho uwe miaka kumi, haturuhusu kiongozi awe ana account nje ya nchi, tulitaka madaraka ya rais yapunguzwe lakini nyinyi ccm mlijifanya kuzuia yale mabadiliko, iweje wewe leo ujifanye utaleta mabadiliko wakati mliyapinga kwa nguvu zenu zote? Tunaomba tuheshimiane samahani, wananchi tumeshaamua lazima tuwaondoe mkajifunze kuheshimu matwaka ya wananchi na sio ya chama, mkirudi baadae ulevi wa madaraka utakuwa umepungua.

Asante sanaaaa,ambaye hajaelewa tutampa elimu,elimu,elimu.
 
Mwana omeonge point nzuri saana, ni kweli watu wali hustle sana kwenye zoezi la uandikishaji na hii ili indicate dhamira ya watu kupiga kura kwa wing mwaka huu ili kuitoa CCM. Wakati wa uandikishaji; LOWASA alikuwa bado haja board in upande wa upinzani. TRUST ME;... KAMA WATANZANIA WATAIPIGIA KURA CCM TENA KWA MARA NYINGINE,.. INABIDI WACHUNGUZWE AKILI ZAO NA UWEZO MZIMA WA KUFIKIRI NA KUDADAVUA MAMBO.
 
Umenena vema sana,japo najua vijana Wengi hawafikiri kama wewe,kinachoendelea kwa sasa ni ushabiki .
Swadakta mkuu daffy, ushabiki umetawala bila kuwa na hoja za msingi kwa anachoki sapoti mtu. Hili ni tatizo na linaweza kutugharimu baadaye
 
Pita sehemu nyingi baadhi ya vijana wanaotaka hayo mabadiliko hewa wengi wao wanatoka kilimanjaro na sehemu zenye walutheri wengi.

Sio sehemu zote za Nchi Kuna vijana wengi wanataka hayo mabadiliko hewa.mtu asikudanganye.Wa sehemiu nyingine wachache mno.Fanya utafiti wako hasa mijini kwenye mikoa yenye watu wa kilimanjaro na walutheri wengi mikoa hii ni ifuatayo

1.Kilimanjaro
2.Arusha
3.Mbeya
4.Dar es salaam
5.Mwanza
6.Manyara
7.Tanga
8.Iringa

Na kagera kwa kiasi kidogo

Nje ya mikoa hiyo Lowasa ni mahututi kisiasa.Tena mahututi hasa.Hata mikoa hiyo Lowasa hana nguvu sana ILA MAENEO MACHACHE TU.
 
Ahsante kwa maoni yako..nachelea kusema machache sana juu ya fikra zako uizoziwasilisha hapa jukwaani. Kwa kifupi na wewe mtoa mada hufahamu unataka mabadiliko gani pia ama hujui tubadilishe nini hasa. Tukifuata propaganda za wanasiasa wote wa upinzani na chama tawala hutajua mabadiliko uyatakayo. Ukifuatilia utendaji wa wagombea utajua mabadiliko gani unayoyazungumzia..lakini ukifuata mkumbo basi hautakuja kufahamu ni mabadiliko gani hasa yanayozungumziwa.

Kwa ufupi ushatoa mada well done..lakini amua sasa vijana wahemkwe kubadili mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya au chupa ya zaman waweke mvinyo mpya. Kumbuka vijana huemkwa kutokana na kuhemshwa na mihemsho ya mambo mengi yanayowahemsha (maisha yao asilia)..ushatafakari hilo???? Na kama huishi maisha yao basi ni rahisi kuwashangaa wanavyohemkwa na wale mnaoishi maisha yanayofanana wataungana na wewe kuwashangaa vijana na wazee..because people we differ..mwiba usiokuchoma hauumi kamwe..

Nimependa sana namna ulivyodadavua kile ulichonacho. Tunataka great thinkers wa namna hii. Thank you very much
 
Pita sehemu nyingi baadhi ya vijana wanaotaka hayo mabadiliko hewa wengi wao wanatoka kilimanjaro na sehemu zenye walutheri wengi.

Sio sehemu zote za Nchi Kuna vijana wengi wanataka hayo mabadiliko hewa.mtu asikudanganye.Wa sehemiu nyingine wachache mno.Fanya utafiti wako hasa mijini kwenye mikoa yenye watu wa kilimanjaro na walutheri wengi mikoa hii ni ifuatayo

1.Kilimanjaro
2.Arusha
3.Mbeya
4.Dar es salaam
5.Mwanza
6.Manyara
7.Tanga
8.Iringa

Na kagera kwa kiasi kidogo

Nje ya mikoa hiyo Lowasa ni mahututi kisiasa.Tena mahututi hasa.Hata mikoa hiyo Lowasa hana nguvu sana ILA MAENEO MACHACHE TU.

Asante sana kaka kwa uchambuzi wako, ila pia umesahau Singida, hasa Iramba kuna KKKT wengi pia
 
Mlipewa nafasi ya kuleta mabadiliko kwa kupitia katiba mpya, mlichokifanya ndio leo hii kimegeuka ghadabu dhidi yenu. Na kwa taarifa yako tayari tuliyataka mabadiliko bila hata huyo Lowassa. Nadhani ulifuatilia jinsi watu tulivyojiandikisha kwa shida bila kujali tunaamka saa ngapi. Na kujiandikisha kule lengo letu lilikuwa ni kuitoa ccm, kumbuka huyo EL alikuwa hajaja upinzani, na wala usidhani tunababaika na Lowassa bali Lowassa alichofanya ni kudandia gari la mabadiliko na kwa bahati nzuri au mbaya akapewa usukani. Sasa nyie mkidhani watu tunababaika na Lowassa mnajidanga tu, hapa ccm ilipotufikisha hata Godbless Lema angekuwa mgombea wa urais bado tungempigia kura za kishindo. Kwa hiyo unapotuletea porojo sijui za mabadiliko bora hayo unayesema wewe, kilichowashinda kufuata maoni ya wananchi kupitia rasimu ya Warioba ni nini leo muamue kutujia na maelezo ya kijinga kama hayo yako.

Wewe kajiandae na wenzio kuingiza nchi machafukoni kwa kugomea maamuzi ya wananchi kwa njia ya kura kama jinsi mlivyopuuza maoni yao kwenye katiba mpya. Kumbuka tulitaka katika maoni ya katiba mpya uwakilishi wa ubunge tulitaka mwisho uwe miaka kumi, haturuhusu kiongozi awe ana account nje ya nchi, tulitaka madaraka ya rais yapunguzwe lakini nyinyi ccm mlijifanya kuzuia yale mabadiliko, iweje wewe leo ujifanye utaleta mabadiliko wakati mliyapinga kwa nguvu zenu zote? Tunaomba tuheshimiane samahani, wananchi tumeshaamua lazima tuwaondoe mkajifunze kuheshimu matwaka ya wananchi na sio ya chama, mkirudi baadae ulevi wa madaraka utakuwa umepungua.

Umetoa maoni yako na umesikika, kitu kidogo tu lakini muhimu sana kinakupunguzia credibility ya maoni yako, ni MATUSI. Bahati nzuri kiswahili ni tajiri sana katika maneno. Kuna maneno mengi sana ungeweza kutumia na kueleweka bila kuweka tusi/neno lenye kuvunja heshima. Hongera kwa mabadiliko, na nakuhimiza kwenda kupiga kura tarehe ikifika ili utimize ndoto yako na utumie haki yako ya kikatiba
 
Great thinkers heshima kwenu. Watanzania ikiwa zimebaki takriban siku 11 kufanya maamuzi ya hatima ya maisha yetu kwa miaka mitano au zaidi ijayo, kuna jambo muhimu sana nimeligundua ktk mtazamo wangu kwa siku kadhaa ambazo nimekuwa nikifuatilia kwa makini mwenendo wa hali ya kisiasa/kampeni inayoendelea hivi sasa.

Nimegundua kwamba kwa sasa Watanzania tulio wengi hasa vijana, tunahitaji mabadiliko. Hili ni jambo muhimu sana kwa mustakabali wa maisha yetu na vizazi vijavyo.

Kinachonipa shaka mimi ni kimoja tu, nacho ni; je kwa mhemuko huu wa vijana na wazee wachache wa kuhitaji mabadiliko bila kujali ni MABADILIKO BORA au BORA MABADILIKO tunakoelekea ni kuzuri??? Nasema vijana wanataka bora mabadiliko kwa sababu hawaangalii rekodi za utendaji wa mtu, uadilifu, umadhubuti wa mtu, sera zake/za chama anazozinadi n.k, bali wanachotaka ni kuondoa chama fulani na kuweka kingine tu. Kwa mtazamo wangu haya ndo mabadiliko wanayotaka vijana wengi.

Hii inanipa shaka mimi kwa sababu kweli tunaweza kufanya mabadiliko ya chama/mfumo lakini bila kuangalia ni nani tunaowapa dhamana ya hatima ya maisha yetu??? Je, hawa watu/mtu ana rekodi gani zinazotupa imani ya kumkabidhi dhamana kubwa kiasi hiki? Hatuangalii je, huyu tunayempa dhamana kubwa alipopewa dhamana ndogo alitenda haki au uadilifu?

Mimi kama mtanzania, nawashauri wenzangu hasa vijana tutafakari kwa kina kabla ya kuamua ni mabadiliko gani tunayoyataka ili baadaye tusije tukalia kilio cha kusaga meno kwa maamuzi ya pupa na ya ghadhabu.

Karibuni wadau wenzangu, tujadili kwa hoja bila hasira.
Tatizo unataka mabadiriko lakini wewe hubadiriki!.
 
Back
Top Bottom