Watanzania watengeneza mtambo kuzalisha umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania watengeneza mtambo kuzalisha umeme

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MziziMkavu, Sep 22, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  TANZANIA imefungua ukurasa mpya wa kuwa na watalaamu wa ndani katika taaluma ya kuzalisha umeme baada ya kikundi cha watu 20 kufanikiwa kutengeza mtambo wa kuzalisha umeme wa upepo.

  Mtambo huo unaojulikana kwa jina la Hugh Piggot Wind Turbine, umetengenezwa mahsusi kupunguza tatizo la umeme vijijini.

  Watanzania hao wameweza kutengeneza mtambo huo baada ya kuhudhuria mafunzo yaliyoandaliwa na Kituo Cha Maendeleo ya Nishati Endelevu na Kisasa (Sadec) cha jijini Dar es Salaam.

  Mratibu wa mafunzo hayo, Emmanuel Yesaya alisema washirki walifanikiwa kutengenza mashine tatu za kuzalisha umeme kwa kutumia upepo huku asilimia kubwa ya malighafi zilizotumika zikitokea hapa nchini.

  “Washiriki wamefanikiwa kutengeneza mashine tatu za kuzalisha umeme, moja inazalisha umeme wa Wati 350-1000,230 V (ukitumia inveta) mashine hizi zina ufanisi kwa asilimia 55 hadi 60”alisema Yesaya.

  Yesaya alizitaja malighafi zilizotumika kutengeneza mtambo kuwa ni mbao ambazo hutumika kutengeneza mapanga,Chuma hutumika kutengeza nguzo na nyaya za shaba na sumaku.

  Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Uholanzi Dk Roland Valckenborg alisema kazi yake ilifanikiwa kwa kiwango kikubwa kwani alifundisha kwa vitendo zaidi kuliko nadharia.

  “Washiriki wamejifunza kwa vitendo zaidi na wamefanikiwa kutengeneza mtambo huu wa Hugh Piggot Turbine,hii ni ishara kuwa sasa nimeacha kitu hapa Tanzania”alisema Valckenborg,mtaamu wa umeme wa upepo kutoka Uholanzi.

  Alisema umeme wa upepo ni jibu mwafaka kwa nchi ya Tanzania ambayo asilimia kubwa ya watu wake wanaishi vijijini huku wakikabiliwa na ukosefu wa umeme unaotokana na gridi ya taifa.

  “Nimekuja kwa lengo moja la kutoa mafunzo hapa Tanzania,nawapongeza wahitimu kwakuwa waliyazingatia mafunzo hayo”alisema Valckenborg.

  na kuongeza “Hii ni ishara kuwa kazi ya kutengeneza na kusambaza umeme katika maeneo ya vijijini ambayo ambayo hayajafikiwa na Umeme wa Gridi ya Taifa itakuwa endelevu”alisema.

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa TaTEDO Leonard Pesambili aliwapongeza wahitimu hao kwa kupata mafunzo hayo na kuwataka kusambaza taaluma hiyo kwa jamii kuhusu umeme wa Upepo.

  Alisema hadi sasa ni asilimi 2 tu ya watu wa vijijini ndio wanaopata huduma ya umeme na kwamba hali hiyo inatokana na eneo kubwa la nchi kutofikiwa na Grid ya Taifa.
  Alisema kutokana namafunzo hayo Aasi yake inayojishughulisha na kazi yakuhifdhi mazingira itaendela kuwatumia katika kusambaza elimu kwa watanzania wengine ambao hawajaipata.

  “Niimani yangu kuwa mafunzo haya yamewapa uelwa juu ya uhusiano uliopo kati ya Nisharti,Maendeleo,utunzaji Mazingira na kupunguza umasikini,mafunzo haya yamewapa wigo mpana wa uelewa juu ya Teknolojia ya kisasa kuhusu nishati endelevu”alisema Pesambili

  Pesambili alitaja faidi za umeme wa Upepo kuwa ni pamoja na kuendelza kuhiofadhi mazingira hapa nchini kuinua uchumi kwa wanchi wanaoishivijijni.

  Alisema TaTEDO wanafanya kazi ya kuhifadhi mazingira hivyo kusambazwa nisharti ya umeme unaotumia nguvu ya upepo kutasaidi kuhifadhi mazingira na kuwaletea maendeleo wakazi wa vijijini.

  Mafunzo hayo ya wiki mbili yaliyoandaliwa na TaTEDO kwa kushirikiana na Dk Roland yalihudhuriwa na washiriki 20 kutoka katika Taaisi mbalimbali za mikao ya Tanzania bara na Visiwani.

  Chanzo: Watanzania watengeneza mtambo kuzalisha umeme

  Nawaunga Mkono hao Watanzania walioweza Kutengeneza Umeme unaotokana na Upepo nawapa Hongera Watanzania kumbe wanao akili ya kuvumbuwa kitu.

  Chanzo. Watanzania watengeneza mtambo kuzalisha umeme
   
 2. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Hugh Piggot?!!! sijaelewa maana ya jina hili wakuu, au ndy jina la sponsor teh teh, ? Hii niliwahi kuiona Mafinga Lutheran wanatoa mafunzo ya kutengeneza kitu kama hiyo.
   
Loading...