Ndahani
Platinum Member
- Jun 3, 2008
- 18,119
- 9,049
Nionavyo mimi, hakuna dini inayoruhusu kufanya mambo ya hovyo ambayo ni dhambi. Mimi ni mkristu mkatoliki, na nimesoma vitabu vitatu vinne hivi ambavyo vinahusisha moja kwa moja Vatican na biashara haramu za mafia kwa mfano Vatican Connection, In God's name, Costra Nostra na hata Godfather ya Mario Puzo. Does it mean Catholism allows what mafias are doing? No way!! Ni collaboration ya mafia na corrupt church officials wachache ambao wwalikuwa kwenye position za kuongoza. Kwa mantiki hiyo ntaliangalia hili tatizo kama liko general kuliko ku base ktk influence ya dini.
Mazingira ya watu wa pwani ambayo wengi wao ni waislamu, ni ya ubaharia, kilimo na uvuvi. Umaskini upo sana na mazingira hayo yalichochea vijana wengi kurubuniwa kuwa utajiri wa haraka ni kudandia meli na kuenda mtoni.
Tukumbuke pia umwinyi miongoni wa watu wa maeneoa hayo huendana endana na katabia ka uvivu ambacho hakawezi kumkwamua mtu kutoka katika umaskini. Ndio maana hata shule watu wengi wa pwani hawakutulia umaanani..leo wengine wachache wanaendesha kampeni kuwa walidhulumiwa kitu ambacho nionavyo sio sahihi.
Lakini hata hivyo kama Taifa leo kuna mambo mengi yanayotishia mustakabari wetu na ni aibu kubwa machoni kwa watu wa mataifa mengine.Kwa mfano, kuua albino kwa ajiri ya utajiri, rushwa kubwa kubwa za viongozi waandamizi yote haya hayatoi picha nzuri huko nje.Nigeria iko hivyo hivyo ndo maana wanajulikana dunia nzima mana kuanzia viongozi walio wengi ni wezi na matapeli mpaka watu wa chini kabisa.
Hili linatugharimu sana sio tu kwa wauza dawa bali sisi kama taifa mana tunajiharibia.
Imefikika wakati sasa nionavyo mimi, tuhimize watu kuwa na skills ambazo zitatufanya tuuzike sehemu nyingi za dunia na kufanya kazi kutupatia utajiri kuliko hizi short cut tunazochukua.
Tupende kuheshimiana pamoja na tofauti za dini zetu badala ya kuanzisha malumbano ambayo hayatakuja kupata mshindi. Imani ni kitu kigumu sana kukibadili kwa malumbano mana kimejishika pale mtu roho yake ilipo.
Hizi mindset zetu zinahitaji mabadiliko, vinginevyo tutakazana kufanya mambo yasijo na tija ya wizi na kuuza dawa halafu wajanja wanatuibia kwa kujiita ma investor. Ni kunuia kupata elimu bora tu ndio utakuwa msaada wetu nionavyo mimi.
Mungu Ibariki Tanzania