Watanzania wapuputika

Bowbow

JF-Expert Member
Oct 20, 2007
541
30
Ndugu wanaJf,

Watanzania ni wakati sasa umefika wa kudhamini maisha yetu zaidi kuliko pesa. Ugumu wa maisha usiwe ni chanzo cha kurisk maisha yetu kwa sababu ya hela za haraka haraka.

Nikianzia kwa wale ndugu zetu walio njee ya Tanzania: huko umatumbini kazi ni nyingi mno za kujipatia kipato, kuanzia proffessional job to non proffessional. Ukifagia utapata hela, ukibeba mabox utapata hela, haiiingi akilini eti tunapigana kuuuza madawa ili upate utajiri. Yeyote anayesupport hili NASEMA HANA AKILI; ANASTYLE KUWA DEPORTED HUKO ALIPO NA ASIRUDISHWE TANZANIA bali apelekwe Colombia au Afganistan

Sasa hivi Netherlands, Denmark, Sweden, Germany, UK, Belgium watanzania tunajulikana kama wasambazaji ama wauzaji madawa kwa kushirikiana na wanigeria. Lakini wanaofanya hiyo biashara ni wachache hivyo wanaharibu reputation ya watanzania wengine.

Pili, kwa ndugu zetu mlio nyumbani, msidanganywe kutumiwa kubeba, kusambaza, kutumia au hata kusaidia kwa namna yeyote kusambaza madawa hayo. Najua kwenye jamii yeyote kuna watu waliofanikiwa kupata fedha kwa njia hiyo lakini tuangalia yafuatayo.

Moja hiyo hela yake aliyoipata kutokana na hiyo biashara imekuwa sustainable ama imeisha ghafla baada ya kusimama au kukamatwa na pilisi?????

Pili, Kwa nini unaangalia walipata utajiri tu usiangalie waliotumia hayo madawa leo wako kwenye hali gani? wanaweza kufanya kazi za kawaida tena au ndio mwisho wao, hawana nguvu tena??

Tatu, Ni wanajamii wangapi wamefariki kutokana na madawa hayo either kwa kutumia kiwango kikubwa kupita kiasi, kupasukiwa kwa kete za madawa hayo tumboni wakiwa njiani katika harakati za kusafirisha ama kurushana fedha zitokanazo na biashara hiyo????

Ni watu wangapi wametamani kujinasua kutoka kwenye biashara/matumizi ya mdawa hayo sasa wameshindwa matokeo yake wamekuwa mzigo kwa wana familia husika?????

Madawa ya kulevya yapo aini nyingi kuanzia bangi, mirungi, kuberi, heroine, cocaine n.k. wengi tumezoea kufukiria cocaine au heroine na kidogo bangi. Lakini vyote vina madhara na vyote vinasababisha vifo vingi katika process zote(kuzalisha, kusambaza, kuuza, kutumia, na hata kugawana mapato yatokanayo na biashara hiyo). Mimi sijui kuandika makala, lakini napenda kutoa ombi kwa wanajamii

Tuache unafiki, narua tena watanzania tuache unafiki na kutoa sifi za kijinga eti ni mpiganaji alikuwa anatafuta fedha. Umasikini tulionao pia unachangiwa na watu hawa. Mfano

Anapoathirika mwanajamii tunatumia fedha nyingi kumsaidia muathirika huyo wa madawa either kwa fedha aweze kupata dozi, tunatumia muda wetu mwingi kuhakikisha hatuiibiii, haibi kwa majirani. Pindi anapokamatwa tunatumia muda kufuatilia kesi mahakani, gerezani na kwingineko badala ya kutumia resources hizo kwa ajili ya vitu vingine

Hela hizo chafu hazitumiki kihali kwenye system, so alot of foreign money zinaenda nje kinyemela na kusababisha kushuka kwa thamani ya shillingi yetu which to economic difficulties

pale inapotokea kifo tena inapokuwa nje ya nchi inawagharimu wanandugu, watanzania wengine pamoja na taifa kwa ujumla na wakati mwingine hata watu kupoteza kazi.

Hiki ndio chanzo kikubwa cha coruption hapa Tanzania, na pale mtu anapokataa kupokea rushwa zao hufanya juu chini kummaliza, ingawa haiwekwi wazi nini chanzo zh mtu kuuwawa(sina uhakika lakini linasemwa Amina chifupa chanzo cha kifo ni madawa hayo)

So watanzania tuendelee kufa hadi lini????
Tutaacha huuu unafiki wa kuwatetea watumiaji, wasambazaji, wauzaji wa madawa hadi lini?????

kama wewe unamfahamummojawapo kwa nini usiwape polisi tips iwe ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania. Tena walio nje ya Tanzania ndio chanzo kikubwa cha matatizo Tanzania. Hivyo tuchukue hatua sasa
watazania wanaokufa kila kukicha kwa sababu ya madawa ya kulevya kwa sababu ya kuingia kwenye hiyo biashara
 
Hivi hii biashara lini itaisha? na kwa nini ni watu wale wale tu

Meanwhile, police in Dar es Salaam have arrested five people suspected of dealing with narcotic drugs.

They were nabbed on Saturday at Kinondoni Mkwajuni area in Kinondoni Municipality within the city.

Kinondoni RPC, Jamal Rwambow named the suspects as Ahmed (30), Fred Sanda (30), Athumani Kasim (25), Mohamed Hasani (28) and Nurudin Athumani (29). They will all appear in court tomorrow.

Source:http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2008/04/07/111896.html

Last week niliorozesha matukio ya watu wa dini fulani na kusema )95% wanatoka kwenye hiyo dini watu wakasema mimi napenda udini.

But as time goes bado tunajionea wenyewe.

Swali je ni lini dini zitashirikiana na serikali kuufundisha, kuonya na baadae serikali kukamata wahusuka? Ama serikali nayo inatetea watu wa dini fulani?????
 
Swala la udini can be a bit too general lakini nakumbuka kuna mtu alisema wengi ni watu wa pwani au visiwani ambao wengi wao ni waislamu ambao wengi hufanya kazi mabandarini, uvuvi etc more likely to be prone to the drug business (to make a quick buck)but Islam has nothing to do with it!!! Pia tuangalie issue ya elimu tukumbuke ndugu zetu waislamu wengi wao hawajasoma kama wakristu tanzania (open to debate) upande wangu naona kutokuwa na elimu ya kukufanya uwe specialised na utafute ajira halali itakufanya utake kutajirika haraka..Wanajf mnaonaje hili??
 
Pia tuangalie issue ya elimu tukumbuke ndugu zetu waislamu wengi wao hawajasoma kama wakristu tanzania (open to debate) upande wangu naona kutokuwa na elimu ya kukufanya uwe specialised na utafute ajira halali itakufanya utake kutajirika haraka..Wanajf mnaonaje hili??

Hiyo habari ya kudai kuwa waislamu hawajasoma ilikuwa zamani, siku hizi wamesoma sana. Tembelea maeneo ya usomi utawaona na kuwasikia. Tusitake kuendekeza donda la zamani kujifanya halijapona ili tusingizie matatizo yote hapo! Kuna mfano wa kuruta aliyeumia kidole chake akawa hawezi kuvaa buti, kwa hiyo akasamehewa jukumu zito la parade, sasa kwa kufurahia hali hiyo, kila siku akawa anafunga tambara kidoleni kuonesha hajapona, ili aendelee kufaidi kula "shushi"! Sasa mie naona hii tabia ya kusingizia kuwa watu hawajasoma inafanana na hiyo, na athari zake ni kuhalalisha kuwatenga kwenye majukumu kwa madai kuwa "hawajasoma". Huu ni upumbavu mtupu, na tena ni mbaya kuliko ufisadi. Kila kundi katika nchi yetu lina wasomi, na wote wanastahili haki, na wanao wajibu wa kufuata.

Acha tabia ya kutoa sababu rahisirahisi kwenye matatizo magumu.
 
Yaleyale,tunakwenda hatua moja mbele then tunarudi hatua mbili nyuma.Waislamu hawajasoma,waislamu wamesoma what is this?Jamani udini hapa hautatusaidia hata siku moja kwa sababu hatujui ni kwa kiasi gani kila mtu ameishiba dini yake.

Unajua haya mambo ni sawa na wewe uliyeoa mke ambae unaamini kabisa kwamba huyo ndio chaguo lako na wewe umemuona ndio mwanamke mzuri kuliko wanawake wote duniani then anakuja mtu kukuambia kwamba mke wako ni mbaya.Hebu fikilia wewe ndio umeambiwa maneno hayo huo moto wake utakuaje?

Kutamka fulani hajasoma,fulani kasoma ili iwaje hapa JF,msituchafulie uwanja huu jamani,mbona hapa ni mahali patakatifu na tunamheshimu kila mtz,haya mambo ya kuchefuana yanatoka wapi jamani?Hapa sio mahali pa kugombanisha watu,hebu tuheshimu kila imani ya mtu.Hivi kati ya waislamu na wakristu ni nani anao uhakika kwamba yeye ndio yuko right katika imani fulani na mwenzake yuko wrong?Tusidanganyane kwa hili.
 
Mbona matusi mengi ukiangalia jinsi nilivyoandika hiyo issue utaona kwamba sina uhakika na nilikuwa nauliza!!..badala ya kunielewesha unatukana..thats not the way to handle hoja!!
 
Mimi ndo niliye andika issue ya elimu..na niliandika kwa kuuliza!!..na ukisoma comment yangu utaona nimesema ISLAM kama dini has nothing to do with issue ya madawa ya kulevya na vijana wakiislamu..tuelimishane sio kujibu kwa asira bila kuelewa comment kwa undani zaidi!
 
Mbona matusi mengi ukiangalia jinsi nilivyoandika hiyo issue utaona kwamba sina uhakika na nilikuwa nauliza!!..badala ya kunielewesha unatukana..thats not the way to handle hoja!!

Nimeipenda Signature yako. Ikuze fanya maandishi yake yawe makubwa zaidi.
 
Acheni Ufala Wa Kuandika Mambo Ya Dini Gani Imesoma Ipi Aijasoma Tuwakane Kabisa Watu Hawa Kama Wanaooua Maalbino Na Mshindwe Mlegee Jibu Hoja Si Kioja
Ahsanten
 
Acheni Ufala Wa Kuandika Mambo Ya Dini Gani Imesoma Ipi Aijasoma Tuwakane Kabisa Watu Hawa Kama Wanaooua Maalbino Na Mshindwe Mlegee Jibu Hoja Si Kioja
Ahsanten

LOL...anzisha thread utoe malalamishi..watu wengine bwana!
 
Acheni Ufala Wa Kuandika Mambo Ya Dini Gani Imesoma Ipi Aijasoma Tuwakane Kabisa Watu Hawa Kama Wanaooua Maalbino Na Mshindwe Mlegee Jibu Hoja Si Kioja
Ahsanten

TAIKUBWA

Mimi sizungumzii udini kwenye hii thread bali nazungumzia hali halisi ya madawa ya kulevya. Sipendi kutasema majinaya watu wakubwa wanaoshukiwa kuwa drugs dealer(untouchables) maana hata mimi sina uhakika lakini wote wana majina yanayofanania huko huko.

Inawezekana kana walivyosema wengine watu wa Pwani ndio wanaopenda kushiriki kwenye hiyo biashara, sawa. Mbona tuna walaumu sana wasukuma kwa kuuwa vizee kwa tuhuma za kishirikina? Mbona tunawalaani sana wachaga tunasema wezi, mbona tunawalaaani sana wahaya tunasema wakabila na mengine mengi lakini linapokuja hili la madini ni watu wa Pwani na sio uislam.

Ninachokifanya ni kuraise awareness ili mashekh, Imam na wengine watie msisitizo ili vijana wasiendelee kupotoka.

Swali najiuliza kwanini siku za karibuni cases za madawa nchini inazidi kuongezeka??????

Je inamaana watu wa Pwani wakishika madaraka basi biashahara hii itashamiri zaidi maana wao ndio wanaipenda zaidi?????? Naombeni Jibu
 
Ubishani Wa Kidini Hauna Maana Yeyote Kwani Ni Mwenyezi Mungu Peke Yake Ajuae Nani Afuatae Dini Ya Haki
 
Jeshi la Polisi linamshikilia mtu mmoja Jijini kwa tuhuma za kumkuta akiwa amemeza pipi kibao za dawa za kulevya. Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Bw. Bernard Nzowa, ameliambia Alasiri kuwa mtu huyo ametambulika kama Abdallah Hassan , 27, mkazi wa Jijini.

Akasema amekamatwa baada ya kushuka kwenye meli eneo la Bandari Jijini Dar.

Akasema, Mwakondo amekamatwa majira ya jioni wakati akitokea Komoro, ambako ndipo alipochukua madawa hayo aina ya Heroin

http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2008/04/21/112863.html

Jamani kuna tatizo hapa kwa nini watu wale wale majina yale yale. Majibu yaliyotolewa bado hayana ukweli wowote. Maana Dar es salaam yenye watu 3million ina maana dini moja ni 95% na miji mingine ya yote Pwani 98% ni dini mmmoja.

Mimi naendelea kuchunguza ila nahitaji kujibiwa
 
Wakuu,

Inabidi kidogo we should step "outside the box" on this issue.
Je unadhani people from other countries wanasemani...The word
is Tanzanians and to a further extent "these Africans".

Kwa hivyo hata tukiendelea kupigana makonzi humu ndani we simply
look like a dog chasing its own tail.We need to suport each other and help one another get away from the world of drugs and
such.

On the flip side shida ipo pale tunaposikia kua hata viongozi wetu wanashiriki katika dili za mihadarati...walalhoi nao huona "aah why not kama vigogo serikalini wanacheza mchezo!
 
Suala la waislam kuwa ndio wengi katika biashara ya madawaya kulevya ni sahihi 1 kwa sababu moja ya msingi,mfano ukienda nchi ya USA ukitembelea katika correction instutes zao wengi wa wafungwa wao ni jamaa wa kizungu hiyo ni kutokana na ukweli kwamba wenye nchi hiyo ni wazungu ambao ndio majority na issue ya waislam Tanzania ni hivyo hivyo wao ndio wengi na wenye nhi.Wao ndio wanao wachagua viongozi nani awe rais na nani asiwe kingozi yote ni kwa sababu ya number yao kuwa kubwa sana zaidi ya waumini wa dini zingine,kesho wakiamua kumfuata Freeman Mbowe na kuachana na CCm tutamuona Mbowe yuko ikulu ni hivyo tuu ,very simple issue.
zee la kiujiji
peace
 
Hawa hapa tena.

The suspected drug traffickers, Yahya Abdulkadir and Yosuf Said, had been arrested by Ethiopian police after they collapsed while on board two separate Ethiopian airline flights from Tanzania to China and China to Tanzania via Addis Ababa

Mimi mwanzoni nilidhani Bowbow ana ajenda fulani lakini ukweli ni kwamba Sisi waislam tunabidi tukatae either kweli vijana wa kiislam wanatumika vibaya ama ni wahuni wanatumia majina ya kiislam na kuficha majina yao halisi.

Huu ni wakati wa kukemea, sasa itafika mahali sisi waislam hatutaweza kusafiri ugaidi sisi, madawa sisi, kujilipuwa sisi Nasema huu ni wakati wa kusema hapana
 
Ukweli lazima usemwe hata kama ni mchungu. Proportion ya waislam waliosoma hata mpaka form six tu hapa Tanzania ni ndogo ukilinganisha na wenzao wakristu. Swala hili lazima liongelewe na ikiwezekana litafutiwe ufumbuzi kwa manufaa ya nchi yetu siku za usoni.
 
Hawa hapa tena.

The suspected drug traffickers, Yahya Abdulkadir and Yosuf Said, had been arrested by Ethiopian police after they collapsed while on board two separate Ethiopian airline flights from Tanzania to China and China to Tanzania via Addis Ababa

Mimi mwanzoni nilidhani Bowbow ana ajenda fulani lakini ukweli ni kwamba Sisi waislam tunabidi tukatae either kweli vijana wa kiislam wanatumika vibaya ama ni wahuni wanatumia majina ya kiislam na kuficha majina yao halisi.

Huu ni wakati wa kukemea, sasa itafika mahali sisi waislam hatutaweza kusafiri ugaidi sisi, madawa sisi, kujilipuwa sisi Nasema huu ni wakati wa kusema hapana

Una hakika haya ni majina yao halisi? Wengi hutafuta pass kwa majina feki kwa ajili ya biashara haramu.

Jiulize kuna kina Juma na Shaban wangapi kule usukumani lakini sio waislamu? Usenene huo!
 
nilipokuwa A level moja kule kanda ya kati wakati. aliingia form five mmoja akiitwa Jaafar Ramadhani huyu alikuwa si muislam, alitumia jina hilo kwa ajili ya kusoma(sina hakika alianzia wapi kulitumia, ila alisema ni jina la kusomea) sote mwanzoni tulifikiri ni Muislam ila ilipofika wakati wa masuala ya dini hakushiriki na waislam bali alishiriki na wakristo. nimetoa mfano huu ambao ni halisi na wakweli ili tuelewe kwamba majina si lazima yaeleze dini. pia imekuwa mara nyingi ni rahisi kwa wakristo kutumia majina ya kiislam kuliko waislam kutumia majina ya kikristo. utasikia baadhi ya wakristo wakiji a.k.a. mufti ama ustadh ama hata shehe ila ni nadra kumkuta muislam kaji a.k.a padre, mchungaji, askofu. haya mambo ya wakrito kutumia majina ya kiislam kujificha si jambo geni japo huko nyuma pia wakati elimu ikitolewa kibaguzi kidini waislam wengi walitumia majina ya kijadi ama kikristo ili kusoma.
 
Hiyo habari ya kudai kuwa waislamu hawajasoma ilikuwa zamani, siku hizi wamesoma sana. Tembelea maeneo ya usomi utawaona na kuwasikia. Tusitake kuendekeza donda la zamani kujifanya halijapona ili tusingizie matatizo yote hapo! Kuna mfano wa kuruta aliyeumia kidole chake akawa hawezi kuvaa buti, kwa hiyo akasamehewa jukumu zito la parade, sasa kwa kufurahia hali hiyo, kila siku akawa anafunga tambara kidoleni kuonesha hajapona, ili aendelee kufaidi kula "shushi"! Sasa mie naona hii tabia ya kusingizia kuwa watu hawajasoma inafanana na hiyo, na athari zake ni kuhalalisha kuwatenga kwenye majukumu kwa madai kuwa "hawajasoma". Huu ni upumbavu mtupu, na tena ni mbaya kuliko ufisadi. Kila kundi katika nchi yetu lina wasomi, na wote wanastahili haki, na wanao wajibu wa kufuata.

Acha tabia ya kutoa sababu rahisirahisi kwenye matatizo magumu.

Thank you! You made my day. Have a great weekend.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom