Mjema Vushanje
Senior Member
- Sep 24, 2017
- 158
- 355
WATANZANIA MNAMJUA Dr STEPHEN MUNGA?
Sijui kama watanzania wanamjua huyu Dr Stephen Munga vizuri,sina uhakika na swali langu lakini yapo mambo kadhaa ambayo nayajua kuhusiana na watanzania kwa Dr Huyu.
Kwanza najua wapo ambao wamewahi kulisikia hili jina.
Pili najua wapo ambao wanamfahamu kwa kumuona .
Tatu najua wapo ambao wanamfahamu kwa kazi na cheo chake
Nne najua kuna ambao hawajawahi kulisikia hili jina na wala hawamfahamu kwa lolote, hii ni kawaida tu!
Lakini pia wapo ambao wamemjua na wanamjua kwa huduma yake .
Vile vile naelewa kuwa watu wengi wanamjua Dr Munga kwa namna tofauti tofauti lakini hofu yangu iliyonifanya mpaka nikaamua kukaa na kuandika haya ni ile kutokujua kuwa Je?
Watanzania wanamjua huyu mtu vizuri?
Wanamfwatilia?
Wanamtumia?
Wanafikiwa na ujumbe wake?
Wanaijua thamani yake?
Ki ufupi mimi nilianza kumfahamu Dr Munga miaka ya 2004/2005 wakati huo akiwa kwenye harakati za kuhakikisha Chuo Kikuu cha SEKOMU kinajengwa. Nakumbuka jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kuhangaika huku na kule kutafuta wafadhili, kushawishi watu na kuhamasisha kuwa kwa hali yeyote Chuo kikuu kijengwe. Hapo ndipo nilimjua huyu mtu akiwa anashirikiana na mkewe Dr Aneth Munga.
Tangu hapo nilianza kumfwatilia Dr STEPHEN MUNGA mpaka leo namfwatilia sana.
Kwanza kabisa huyu jamaa ni msomi mzuri tu. Ana PhD (Doctor of Philosophy) katika maswala ya Theolojia na kama sikosei kuna Politics kidogo humo. Alisoma LUND UNIVERSITY nadhani ni Ujerumani. Kwa hiyo huyu jamaa ni msomi kwelikweli.
Pili huyu jamaa ndie Askofu wa moja ya Dayosisi kubwa kabisa Tanzania ambayo ni Dayosisi ya Kaskazini mashariki huyu ni Askofu wa hiyo Dayosisi katika kanisa la KKKT.
Tatu Huyu Dr Stephen Munga ni Chancellor wa SEKOMU (SEBASTIAN KOLOWA MEMORIAL UNIVERSITY), Hiki ni chuo kikubwa sana katika vyuo vikuu binafsi hapa Tanzania, ni chuo ambacho kiko kule Lushoto eneo la Magamba.
Ni moja ya Vyuo vikuu pekee vyenye mandhari kama ya Nchi za Uholannzi au Uswizi kulingana na mazingira yake ya ubaridi na ukijani uliotawala uoto wa eneo lenyewe. Ni chuo kizuri sana.
Lakini zaidi ya hayo DR Stephen Munga amejipambanua kuwa askofu tofauti na maaskofu wengine kwa kuwa Mkweli, huyu jamaa ni mkweli na ndio maana hata kama siku nasikia uvivu wa kuhudhuria ibada nikisikia Askofu Munga yupo lazima niende kwasababu lazima nitapata vitu adimu kutoka kwake. Nampenda sana.
Huyu jamaa anafwata nyayo za mitume wa zamani, anafwata nyayo za Yesu kristo.
Nasema hivyo kwasababu baadhi ya Viongozi wa dini wa siku hizi ni waoga, hawasemi ukweli wakati mwingine kwa kuogopa mamlaka lakini Dr Munga ni tofauti yeye anasema ukweli.
Mussa alipokuwa anawapeleka watu wa Mungu Canaan walipopata kiu alihangaika kuwapa Maji, walipopata njaa alihangaika kuwapa Chakula, walipoumwa alihangaika kuwatafutia dawa mfano walipoumwa na nyoka jangwani japo lengo la safari ilikuwa sio kula,kunywa wala huduma kama hizo.
Yesu Kristo alipohubiri kwa masaa mengi na kuona watu wana njaa aliagiza iletwe mikate na samaki wachache akavibariki na maelfu kwa maelfu wakala na kushiba japo lengo la mahubiri yake ni kuuendea ufalme.
Viongozi wengine wa dini wanafikiri kuwa wajibu wao ni kuhubiri habari za kwendaa mbinguni pekee, kufungisha ndoa, kuzika waumini wakifariki, kukusanya sadaka…sio kweli. Ingekuwa ni hivi hata Yesu asingekufa, asingeuawa na watawala wa Roma.
Viongozi wa Dini wanatakiwa wawe mstari wa Mbele kukosoa watawala, kuwaelekeza waumini wao ninini wafanye katika ufasaha na hapo wawahubirie habari za kumuona Mungu, wasipofanya hivyo watawahudumu waumini wachovu, waliovunjika mioyo, wajinga, wenye njaa, wenye mateso, wanyonge na wasiojitambua…wakati huo huo mbinguni hakitaingia kilicho kinyonge.
Asante sana DR STEPHEN MUNGA kwakuwa wewe umekuwa tofauti…
Hivi MEDIA zinakuona?
WATANZANIA wanakujua?
JE WATAWALA?
IBADA NJEMA WAKRISTO WOTE,
WASIO NA DINI SIKU NJEMA
WAISLAM WOTE NA WENYE DINI NYINGINE TUOMBEANE!

Shauri yako